focusmedia Search This Blog

Wednesday, March 8, 2017

WILL SMITH NA FAMILIA YAKE WAMEITENDEA HAKI TANZANIA


Tanzania ni urithi wa ulimwengu kimazingira. Hifadhi za Taifa Kumi na sita  zenye uasili  wa kimazingira tangu karne na karne Zinawaleta watu maarufu Duniani. Kuna mengi zaidi ya kusema kuhusu uzuri wa Tanzania kuliko eneo lolote ulimwenguni. Kuna maeneo machache sana Duniani ambayo yanatoa taswila bora ya ikolojia kwa zaidi ya matarajio yako eneo hili ni Tanzania,hapa ndio utaona wazi Jamii ya Paka wakubwa ulimwenguni,utaona uhamiaji wa wanyama  wakisafiri kila msimu wa maisha yao,Utaona sakafu ya Ngorongoro kama urithi wa Kihistoria wa maisha ya viumbe wote sehemu moja, maelfu ya flamingo,Sokwe wa Mahale au fukwe  Mwanana za maziwa na Bahari ya Hindi ziiubeba ukanda wa pwani, maziwa ya Victoria, Tanganyika na Nyasa,Will Smith anaamini yeyote ajae Tanzania atabaki na alama ya kumbukumbu ya urithi wa ulimwengu wa mazingira na viumbe wake,eneo lenye maumbile ya amani na utulivu kila kona,Utafika kileleni mwa Afrika Kilimanjaro,visiwa mwanana vya Zanzibar,eneo lenyeshamba kubwa la mauwa kiasili linaitwa bustani ya mungu Kitulo, Hii ni Tanzania
Fresh Prince a.k.a will smith baba yake Jada smith na Willo smith na wengine wakiwa katika Moja ya mbuga zetu Tanzania


Rubani Abed na mzee wa Men In Black Will Smith







Mwanamitindo maarufu wa marekani aitwaye #chaneliman ameitembelea serengeti .

Mwanamitindo maarufu wa marekani aitwaye #chaneliman picha ya pamoja na Will Smith wakiwa Serengeti .

Mwanamitindo maarufu wa marekani aitwaye #chaneliman



No comments:

Post a Comment