focusmedia Search This Blog

Monday, May 29, 2017

AMIR JESHI MKUU RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AMUAPISHA KAMISHNA WA POLISI SIMON SIRRO KUWA KAMISHNA GENERALI WA JESHI LA POLISI NCHINI MEI 29,2017 IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Amir jeshi mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimvua cheo cha Kamishna wa Polisi Simon Sirro na kumvalisha cheo cha Kamishna Generali wa Jeshi la polisi nchini Mei 29,2017 Ikulu jijini Dar es salaam




Kamshina Jenerali wa Polisi nchini Simon Sirro akila kiapo cha maadili ya utumishi wa Umma mara baada ya kumuapisha  na Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  kuwa Kamshina Jenerali wa Polisi nchini Mei 29,2017 Ikulu jijini Dar es salaam

Amir jeshi mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mkuu wa Jeshi la Polisi Mteule, Kamishna wa Polisi Simon Sirro kuwa Kamishna Generali wa Jeshi la Polisi Nchini Mei 29,2017 Ikulu jijini Dar es salaam

Amir jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Kamshina Jenerali wa Polisi nchini Simon Sirro mara baada ya kumuapisha Mei 29,2017 Ikulu jijini Dar es salaam

Kamshina Jenerali wa Polisi nchini Simon Sirro  akisaini hati ya kiapo cha maadili ya utumishi wa Umma mara baada ya kuapishwa

Kamshina Jenerali wa Polisi nchini Simon Sirro  mara baada ya kupandishwa cheo

Amir jeshi mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Hassani Suluhu, Waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchema,Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Jaji Prof. Ibrahim Hamis Juma, Mkuu wa Jeshi la Polisi Mteule Simon Sirro, aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Erenest Mango, katibu Mkuu kiongozi Balozi John Kijazi, pamoja na Makamishna mbalimbali wa Wizara ya mambo ya ndani katika picha ya pamoja



Amir jeshi mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akisalimia na makamanda mbalimbali wa polisi na Jeshi la wananchi wa tanzania mara baada ya kumuapisha  Mkuu wa Jeshi la Polisi Mteule Simon Sirro Ikulu jijini Dar es salaam



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Hassan Suluhu akimpongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi Mteule, Kamishna Jenerali wa Jeshi la polisi nchini Simon Sirro mara baada ya kuapishwa Mei 29,2017 Ikulu jijini Dar es salaam

Wednesday, May 24, 2017

MUHTASARI WA KAMATI YA UCHUNGUZI WA MCHANGA WA MADINI

Muhtasari wa kamati ya uchunguzi wa mchanga wa madini kama ulivyowasilishwa na mwenyekiti wake Prof Abdulkarim Hamis Mruma  Ikulu!.



HADIDU ZA REJEA!.

1.Kamati ilikuwa na kazi ya kuchunguza aina na kiwango cha madini yaliyopo ndani ya mchanga wa madini unaosafirishwa nje!.

2.Chimbuko la utafiti huo ni kutojulikana kwa kiwango cha makinikia na mikataba yake!.

3. Hadidu za rejea zilikuwa ,Kufanya uchunguzi wa makinikia kwenye bandari ya dsm na migodini,Kufanya uchunguzi wa kimaabara ili kujua thamani na aina ya madini yaliyopo kwenye makilikia,kuchuza uwezo wa scanner zilizopo bandarini,kuchunguza uwezo wa TMAA katika kusimamia makinikia,

4.Kamati ilitembelea bandari ya Dsm,bandari kavu na kwenye migodi ya Bulyanhuru na Buswagi,yapo makontena ambayo kamati ilichukua sampuli ya juu na chini,sampuli nyingine ilikuwa zigzaga!.

5.Kamati ilichunguza uwezo wa scanner kupima makinikia!.

6.Kamati ilikokotoa thamani ya madini yaliyopatikana kwenye makinikia!.

MATOKEO YA UCHUNGUZI

1.Kamati imebaini uwepo wa dhahabu kiasi Kikubwa cha dhahabu kwenye makinikia,katika makontena 277 yaliyozuiliwa kulikuwa na tani saba za dhahabu!.
2.Makontena 277 yaliyozuliwa yalikuwa na dhahabu yenye thamani zaidi ya shilingi Trilioni moja nukta moja nne saba!.

3.Kamati ilibaini uwepo wa madini ya shaba,Silver,surpher,chuma.

4.Copper pekee ilikuwa ya thamani ya shilingi Bilioni 23.3,hapa kulikuwa na tofauti kubwa na ripotibya serikali ambayo ilionesha kuwa na thamaninya Bilioni 13.

4.Upande wa silver kamati ilibaini uwepo wa silver ya thamani ya bilioni 2.1.tofauti na ripoti ya Serikali ilionesha thamani ya Bilioni 1.

5.Upande wa surpher kamati ilibaini uwepo wa surpher ya thamani ya shilingi bilioni 1.9,kamati ilibaini madini madini haya hayapo katika mrabaha

6.Kamati ilibaini uwepo wa madini ya chuma yenye thamani ya shilingi Bilioni 2.3,

7.Kamati ilibaini uwepo wa madini mkakati ambayo kwa sasa yanahitajika sana duniani yenye thamani kati ya bilioni 129.5 mpaka  bilioni 261.5

Thamani ya madini yote katika makinikia kwenye makontena 277 yaliyochunguzwa kamati imebaini yana thamani ya triloni 1.339,ambazo serikali haipati hasa senti moja na hayapo kwenye mrabaha!.

8.Kamati imegundua uwepo wa madini mengine mengii ambayo hayarekodiwi kwenye nyaraka za serikali!.

9.Kamati imebaini wakala wa madini Tanzania hawafungi utepe kwenye makontena kuonesha viwango vya madini,kamati imebaini ufungwaji huu kufanyika wakati wa kusafirisha makontena.

10.Kamati imebaini scanner za bandarini kutokuwa na uwepo wa kubaini utotoshwaji wa mali!.

MAPENDEKEZO YA KAMATI

1.Serikali isitishe usafirishaji wa mchanga nje ya nchi

2.Serikali ihakikishe mitambo ya kusafisha makinikia unafanyika nchini

3.TMAA ifunge utepe mara baada ya mchanga kupakiwa kwenye makontena!.

4.TMAA ipime metal zote kwenye makininia

5.TMAA ipime viwango vyote vya makinikia na madini kwenye mbar bila kujali ripoti ya msafirishaji hii itasaidia Serikali kupata mrabaha!.

6.Serikali iwachukulie hatua watendaji wa TMAA na wizara husika.

7.Serikali iweke mfumo kushtukiza kwenye udhibiti wa madini!.

8.Serikali itumie wataalam wa mionzi kwenye scanner za bandarini!.



Thursday, May 11, 2017

MVUA NCHINI TANZANIA ZALETA MAAFA,MAPOROMOKO YAFUNGA BARABARA

Maporomoko ya mawe Lushoto eneo la Vuga






RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AMPOKEA RAIS WA JAMHURI YA AFRIKA KUSINI MHE. JACOB ZUMA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM MEI 11,2017



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli     na Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Jacob Zuma wakiwa wamesimama huku Nyimbo za Mataifa mawili zikiimbwa Ikulu jijini Dar es salaam mei 11,2017

Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Jacob Zuma akikagua gwaride lililoandaliwa kwa heshima yake na kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es salaam mei 11,2017



Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Jacob Zuma akiteta jambo na mwenyeji wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es salaam mei 11,2017


Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Jacob Zuma zawadi mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es salaam mei 11,2017

PICHA NA IKULU