focusmedia Search This Blog

Thursday, August 31, 2017

RAIS DKT.JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA VIONGOZI MBALIMBALI WA ULINZI NA USALAMA WASTAAFU NA WASASA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM 31 AGOSTI 2017.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wasasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam 31 agosti 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wasasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya mazungumzo yao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, Omar Mahita(IGP Mstaafu), Said Mwema(IGP Mstaafu) pamoja na Ernest Mangu(IGP Mstaafu) Ikulu jijini Dar es Salaam,31 agosti 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu Omar Mahita Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Mstaafu Cornel Apson pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu Omar Mahita Ikulu jijini Dar es Salaam,31 agosti 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wasasa na wastaafu wa Magereza Ikulu jijini Dar es Salaam,31 agosti 2017.
Mkuu wa majeshi mstaafu Jenerali Mrisho Sarakikya akibadilishana mawazo na Bw. Omary Mahita(IGP mstaafu) pamoja na Bw. Cornel Apson (DGIS mstaafu) kabla ya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ikulu jijini Dar es Salaam,31 agosti 2017.

Friday, August 25, 2017

RAIS MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI ASALIMIA WANANCHI WA FERRY KIGAMBONI WAKATI AKIELEKEA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE KWENYE UFUNGUZI WA KAMBI YA MAFUNZO YA VIJANA WA CCM ILIYOANDALIWA NA UMOJA WA VIJANA NA VYUO VIKUU.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akichukua Tiketi zake pamoja na chenchi mara baada ya kulipia huduma ya Kivuko wakati akielekea katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni jijini Dar es Salaam.25 Agosti 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana pamoja na kuzungumza na abiria mbalimbali wakati akisubiri kuvuka kwa kutumia usafiri wa Pantoni kuelekea katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni jijini Dar es Salaam 25 Agosti 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Yusuph Ndemango ambaye ni mlemavu wakati alipomkuta ndani ya jengo la abiria lililopo upande wa Magogoni kabla ya kuvuka na Pantoni kuelekea katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiingia katika kivuko cha MV Kigamboni pamoja na abiria wengine wakati akivuka kuelekea upande wa pili wa Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ndani ya Kivuko cha MV Kigamboni pamoja na abiria wengine wakati akivuka kuelekea upande wa pili wa Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili ferry upande wa Kigamboni mara baada ya kushuka pamoja na abiria wengine kwenye pantoni la MV Kigamboni.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mama mmoja mara baada ya kuvuka upande wa Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akinunua chapati mara baada ya kuvuka upande wa Kigamboni wakati wa asubuhi 25 Agosti 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Minazini Kigamboni jijini Dar es Salaam 25 Agosti 2017.
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiimba pamoja na wanachama wa CCM waliopo katika kambi ya mafunzo ya vijana iliyoandaliwa na Umoja wa vijana wa vyuo na Vyuo vikuu(CCM) katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam 25 agosti 2017.

Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanachama wa CCM waliopo katika kambi ya mafunzo ya vijana iliyoandaliwa na Umoja wa vijana wa vyuo na Vyuo vikuu(CCM) katika ukumbi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam 25 Agosti 2017.

MAKONDA AZIDI KUBORESHA MAZINGIRA YA KAZI     KWA JESHI LA POLISI DAR ES SALAAM


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amepokea Pikipiki za kisasa 10 kwaajili ya Askari wa Usalama Barabarani zenye thamani ya Shilingi Million 400 kutoka kampuni ya utengenezaji wa Pikipiki ya TONGBA ya China.

Hatua hiyo inakuja baada ya RC Makonda kutafuta kampuni hiyo na kuwasilisha ombi la kupatiwa Pikipiki za kisasa kwaajili ya kuongoza Misafara ya Viongozi, Misiba na kuwahisha Wagonjwa waliozidiwa Hospitalini ambapo kampuni hiyo ilipokea kwa mikono miwili ombi hilo kwa kutoa Pikipiki hizo.

Makonda amesema lengo lake ni kuboresha Mazingira ya utendaji kazi wa Jeshi la Polisi kwa kuhakikisha Askari wanakuwa na vifaa vya kutosha ambapo hadi sasa amefanikiwa kupata Baiskeli 500, Pikipiki za kawaida 200 Computer 100 , Pikipiki za Trafic 10 na kufanya maboresho ya Magari ya Jeshi hilo yaliyokuwa yameharibika.

Aidha Makonda amemuagiza aliekuwa Kaimu Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam kuwakamata Askari wote waliobainika kushirikiana na wauzaji wa Dawa za kulevya na wale wanaobambikizia Wananchi kesi kukamatwa ndani ya masaa Masaa matano.

Agizo hilo limekuja baada ya hivi juzi Msamariamwema kutoa taarifa za uwepo wa muhusika wa Dawa za kulevya kwenye moja ya Hotel na Askari walipofika kwenye Hotel hiyo wakamkamata na kupewa Rushwa baada ya muda Mtuhumiwa akaachiliwa na kurudi kwenye Hotel kisha kufanya fujo kumtafuta alietoa taarifa na baada ya Makonda kufika na kuangalia Camera za CCTV wakawabaini Askari hao.

Pamoja na hayo amesema wapo Askari waliomkamata Mwananchi akiwa Mpenzi wake kwenye Gari kisha kuwapiga Picha za Utupu na kuwalazimisha watoe kiasi cha Million Tano iliwasisambaze Picha hizo kitendo ambacho ni kinyume Sheria ambapo Mheshimiwa  Makonda amesema hawezi kuruhusu vitendo kama hivyo vitendeke kwenye Mkoa wake na kuongeza kuwa  anataka kuona Sheria na Haki vinatendeka kwa Wananchi.

Makonda pia amebaini uwepo wa Askari wa Uwanja wa Ndege wanaoshirikiana na Raia wa China kusafirisha Kobe na Wanyamapori na Askari wanaowabambikia kesi wananchi ikiwemo wale wanaowakamata watu kwenye sehemu za mapumziko.

Amesema hatokubali kuona Askari wachache wanaotumia Magwanda kuwanyanyasa Wananchi na kuchafua taswira ya Jeshi la Polisi na kufanya Wananchi kushindwa kutoa ushirikiano. 






Wednesday, August 23, 2017

            TTCL YAPEWA CHANGAMOTO KUFIKA VIJIJINI


NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Mhandisi Edwin Ngonyani, ameitaka Kampuni ya Simu Tanzania TTCL kuongeza juhudi za kutoa huduma kwa Wananchi hasa waliopo katika maeneo ya Vijijini ili kuwawezesha Wananchi kupata Mawasiliano ya uhakika kutoka katika Kampuni yao Umma.

Mhe Ngonyani ametoa maelekezo hayo alipofanya ziara fupi ya kutembelea Makao Makuu ya TTCL ambapo amepata fursa ya kuzungumza na Bodi na Menejimenti ya TTCL ambapo alitumia hadhatra hiyo kutoa mrejesho wa ziara yake ya kutembelea maeneo mbali mbali ya Tanzania Bara na Visiwani kukagua huduma za Taasisi zilizo chini ya Wizara yake.

Mhe Ngonyani amesema, pamoja na mafanikio makubwa ambayo TTCL imeyapata katika Viwango vya ubora wa huduma, kuongeza idadi ya Wateja, usimamizi na uendeshaji wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB) na Kituo cha Kutunzia Kumbukumbu za Kimtandao( NIDC) bado TTCL inakabiliwa na changamoto kubwa ya kufikisha huduma ya Mawasiliano Vijini hasa katika maeneo ambayo kwa sasa hayana Mawasiliano kabisa baada ya kuzimwa mwa mitambo ya Mawasiliano iliyokuwa ikitumia teknolojia ya CDMA.

Aidha, Mhe Ngonyani ameiagiza Bodi na Menejimenti ya TTCL kuongeza kasi ya kusambaza huduma za TTCL 4G pamoja na kufanyia kazi kilio cha muda mrefu cha Watumishi wa TTCL kuomba kuboreshewa Maslahi yao.

“Pote nilipopita Bara na Visiwani, Watumishi wa TTCL wameniomba nifikishe kilio chao kwenu, wamekaa kipindi kirefu sana bila kuboreshewa maslahi yao huku gharama za maisha zikiwa juu. Ninashauri msikie kilio hiki ili pamoja na kuboresha huduma zenu, mazingira ya kazi na maslahi ya Watumishi pia yapewe kipaumbele,”

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Mhe Mhandisi Omari Rashid Nundu amesema, Bodi na Menejimenti ya TTCL zimepokea maelekezo ya Mhe Naibu Waziri na kwamba mpango mkakati wa muda mfupi uliowekwa na Kampuni hiyo, changamoto hizo zitafanyiwa kazi.

“Mhe Naibu Waziri, tunayo nia ya dhati ya kuibadilisha TTCL na kuifanya iwe kweli Kampuni ya Umma inayowaunganisha Watanzania. Tumedhamiria kuwafikia Wananchi wote kwa huduma za kiwango cha juu na unafuu sana wa gharama sambamba na kuimarisha vitendea kazi na maslahi ya Watumishi. Tunaomba Serikali iendelee kutuunga mkono na kutuwezesha kutimiza mipango hii,” amesema Mhandisi Nundu.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bw Waziri Waziri Kindamba amesema, TTCL mpya imejipanga kikamilifu kujiendesha kibishara na kufikia lengo la kutoa gawio Serikalini. Bw Kindamba ameongeza kuwa, TTCL kupitia kauli mbiu yake ya Rudi Nyumbani imekusudia kuhakikisha kuwa Watanzania wote wanapata huduma za Mawasiliano kwa Teknolojia za 2G/3G na 4G LTE sambamba na huduma za kifedha za TTCL PESA ambayo imezinduliwa hivi karibuni.

Mapema mwezi ulipita, TTCL ilizindua huduma za kifedha kwa njia ya Mtandao ijulikanayo kama TTCL PESA. TTCL PESA itawawezesha Wananchi kupata huduma mbali mbali kama Kutuma Fedha, Kulipia Ankara za huduma kama vile Maji, Umeme (LUKU), Ving’amuzi na Kununua vifurushi vya TTCL huku huduma nyingine zikiendelea kuongezwa.

Aidha,TTCL PESA itasaidia katika kufanya makusanyo ya tozo za Serikali pamoja na kuongeza usalama na kupunguza hatari ya kupotea kwa fedha kupitia vitendo vya uhalifu kama ujambazi wanavyofanyiwa Wananchi (Wakulima na Wafugaji) wanaotembea na fedha nyingi katika maeneo mbali mbali wanapofanya biashara zao za mazao na mifugo.



Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bw Waziri Waziri Kindamba (kushoto) akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Mhandisi Edwin Ngonyani (kulia) mara baada ya kuwasili katika ofisi yake kusaini kitabu cha wageni.
Sehemu ya menejimenti ya kampuni ya TTCL ikiwa katika kikao hicho na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Mhandisi Edwin Ngonyani alipowatembelea.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Edwin Ngonyani (kulia) akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) leo Makao Makuu ya kampuni hiyo alipotembelea na kuzungumza na Bodi hiyo katika ziara yake ya kutembelea taasisi zilizo chini ya wizara yake. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Mhandisi Omar Nundu. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Mhandisi Omar Nundu (kushoto) akitoa maelezo mafupi kuhusiana na utendaji kazi wa kampuni hiyo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Mhandisi Edwin Ngonyani (kulia) alipotembelea na kuzungumza na Bodi ya TTCL leo Makao Makuu ya TTCL jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Bw Waziri Waziri Kindamba akiwa katika kikao hicho
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Mhandisi Omar Nundu (kushoto) akitoa maelezo mafupi kuhusiana na utendaji kazi wa kampuni hiyo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Mhandisi Edwin Ngonyani (kulia) alipotembelea na kuzungumza na Bodi ya TTCL leo Makao Makuu ya TTCL jijini Dar es Salaam.

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA SIKU 2 WA TAIFA WA URUTUBISHAJI WA CHAKULA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata keki iliyopikwa kwa unga wa mahindi wenye vitamini A na ngano mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Taifa wa Urutubishaji wa Chakula uliofanyika kwenye kituo cha Mikutano Cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar Es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata keki iliyopikwa kwa unga wa mahindi wenye vitamini A na ngano mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Taifa wa Urutubishaji wa Chakula uliofanyika kwenye kituo cha Mikutano Cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar Es Salaam. Picha na OMR

Tuesday, August 22, 2017

MKUU WA WILAYA YA GAIRO MHE. SIRIEL SHAIDI MCHEMBE TAREHE 22/8/2017 AMEFANYA ZIARA YA KUKAGUA BAADHI YA WANUFAIKA WA PESA ZA TASAF

Kupitia pesa za TASAF, wamefanya yafuatayo:-
Wameweza kutoka kwenye nyumba za tembe (full suite) na kujenga nyumba zilizoezekwa na mabati.

Wameweza kujenga vyoo hivyo kuacha kujisaidia porini.
 Wameweza kufuga mifugo na mifugo inazaliana.
 Kuna wanawake waliokuwa na vigenge vya mbogamboga na sasa wameweza kuanzisha viduka vya wastani.
 Wameweza kulima hata kama ni kwa kukodisha nusu eka na hivyo kupata mazao kama mtama, mahindi na alizeti.Wameweza kununulia watoto nguo za shule na madaftari.

 Asilimia 80 ya Kaya masikini zaidi ya 1,000/- alizotembelea Mkuu wa Wilaya wamekata Bima ya Afya ya Jamii (Community Health Fund). Hivyo basi badala ya kuuza kuku au mbuzi anapougua sasa wanatibiwa moja kwa moja. Pia wamama wajawazito na watoto wanapata huduma bila shida. 







NUKUU MUHIMU ZA RAIS WA TANZANIA DR.JOHN POMBE MAGUFULI






RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI AKUTANA NA RAIS WA SHIRIKA LA KIMATAIFA LA MAENDELEO LA JAPAN (JICA) IKULU JIJINI DAR ES SALAAM 21 AGOST 2017


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea jambo  na  Rais wa shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) Bw. Shinichi Kitaoka aliyekutana na kufanya mazungumzo naye  Agosti 21, 2017 Ikulu jijini Dar es salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo  na Rais wa shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) Bw. Shinichi Kitaoka (kushoto) na Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshida Agosti 21, 2017 Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Joseph Nyamhanga na Mtendaji Mkuu wa Tanroads Mhandisi Patrick Mfugale kwa Rais wa shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) Bw. Shinichi Kitaoka aliyekutana naye Agosti 21, 2017 Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo  na Rais wa shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) Bw. Shinichi Kitaoka (kushoto) na Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshida Agosti 21, 2017 Ikulu jijini Dar es salaam.
PICHA NA IKULU

Saturday, August 19, 2017

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AHUDHURIA UFUNGUZI RASMI WA MKUTANO WA 37 WA SDC KATIKA UKUMBI WA O.R TAMBO, MJINI PRETORIA AFRIKA KUSINI


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 19 Agosti 2017, amehudhuria  ufunguzi rasmi wa Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika – SADC mjini Pretoria Afrika Kusini akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Mhe. Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa taarifa fupi kuhusu majukumu ya SADC Organ kwa kipindi cha Agosti 2016 - Agosti 2017 kwa niaba ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa SADC Organ anayemaliza muda wake.