focusmedia Search This Blog

Friday, December 23, 2016

MARUFU KUOZESHA WASICHANA WA UMRI MDOGO;SERIKALI YA TANZANIA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wazazi na walezi wa Tanzania Zanzibar waache tabia ya kuwaoza wasichana wa kike wakiwa na umri wadogo bali wawasomeshe kwa ajili ya manufaa yao ya jamii kwa ujumla.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti wakati akizindua madrasa ya kisasa iliyojengwa kwenye eneo la kilimani na kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa na ujenzi wa msikiti mkubwa kuliko yote nchini Tanzania unaojengwa katika eneo la Ijitimai kidoti katika Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa michango ya wananchi katika siku yake ya kwanza ya ziara ya Kikazi Kisiwani Unguja.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kama wazazi na walezi watasomesha watoto wa kike elimu watakayopata itasaidia kwa kiasi kikubwa wasichana hao kufanya maamuzi sahihi na yenye tija katika jamii.
Amesisitiza kuwa pamoja na elimu kuwa ni haki ya msingi kwa mtoto wa kike hivyo ni muhimu kwa jamii nzima ya Zanzibar ihakikishe watoto wa kike wote wanapata elimu kwani watakuwa na uwezo wa kuchagua na kuandaa mustakbali wa maisha yao ya baadaye ikilinganishwa na hali ilivyo sasa kwenye baadhi ya maeneo.
Kuhusu elimu ya dini, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewahimiza wazazi na walezi kuwalea watoto katika maadili mema kwa kuzingatia maandiko matakatifu ya Mtume Mohammad (S.A.W).
Amesema vijana wengi wanaolelewa kwa kufuata misingi ya bora ya dini ni vigumu kurubuniwa na kujiingiza katika matendo yasiyofaa katika jamii.




Saturday, December 17, 2016

SERIKALI YA TANZANIA YASEMA VIWANJA VYOTE VYA MICHEZO NCHI NZIMA VIREJESHWE NA KILA JUMAMOSI YA PILI IWE SIKU YA MAZOEZI KWA AFYA ZETU

Miezi mitatu kwa Halmashauri zote nchini ziwezimerudisha serikalini haraka maeneo ya michezo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa muda wa miezi mitatu kwa Halmashauri zote nchini kurudisha serikalini haraka maeneo ya michezo yaliyovamiwa na watu kwa ajili ya kufanya shughuli zao binafsi.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo baada ya kushiriki matembezi na kuzindua wa kampeni ya Kitaifa ya kudhibiti Magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwenye viwanja wa Leaders Club jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais ameonya kuwa kama watendaji wa mikoa na halmashauri watashindwa kurudisha maeneo hayo basi watenge haraka maeneo mengine kwa ajili ya wananchi kufanya mazoezi kama hatua ya kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Katika kuunga mkono utaratibu wa kufanya mazoezi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewaagiza viongozi wa mikoa na wilaya zote kuweka utaratibu wa kufanya mazoezi angalau kwa mwezi mara Moja.

Kila Jumamosi ya pili ya mwezi
“Nitamke kuwa kila Jumamosi ya pili ya mwezi itakuwa siku ya mazoezi kwa afya kwa sababu mazoezi ni afya na nawaasa wananchi kufanya mazoezi na kuanzisha na kujiunga na vikundi vya mazoezi na serikali itatimiza wajibu wake wa kuweka mazingira mazuri ya kufanyia mazoezi kote nchini”

Mchakamchaka mashuleni
Makamu wa Rais pia ameagiza watendaji wa Wizara ya elimu, Sayansi na Teknolojia kurudisha mchakamchaka mashuleni kulingana na maeneo yalivyo.
Amesema mchakamchaka utasaidia kuimarisha afya za wanafunzi na kukabiliana na magonjwa mbalimbali.

“Natoa rai utaratibu wa mchakamchaka katika shule zetu urudishwe mara Moja katika Muda ambao utaonekana ni mwafaka kwa shule husika”.
Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais ameiagiza Wizara ya Afya kukamilisha haraka mchakato wa kuunda kamati ya kushughulikia magonjwa yasiyo ya kuambukiza itakayojumuisha wadau kutoka wizara mbalimbali nchini.

Amesisitiza kuwa mchakato huo ni lazima ukamilike tarehe 1 machi mwaka 2017.
Kwa upande wake, Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema magonjwa yasiyo ya kuambukiza yamekuwa yanaongezeka sana duniani kote hasa kwenye nchi zilizo chini ya Jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania ambapo magonjwa hayo mpaka sasa yanachangia asilimia 27 ya vifo Duniani.

 26% ya wananchi ni wanene kupita kiasi
Amesema utafiti uliofanyika mwaka 2012 uliohusisha wilaya 53 hapa nchini umeonyesha viashiria hatarishi vya magonjwa hayo ambapo asilimia 26 ya wananchi ni wanene kupita kiasi,asilimia 26 wana lehemu nyingi mwilini na asilimia 25.9 wanashinikizo kubwa la damu.
Utafiti huo pia ulionyesha kuwa asilimia 15.9 ya wananchi wanavuta sigara na asilimia 97.2 ya wananchi wanakula mboga mboga na matunda chini ya mara tano kwa siku.

Waziri wa afya Ummy Mwalimu amesema watanzania wanaweza kukabiliana na magonjwa hayo kwa kufanya mazoezi ya viungo angalau mara tatu kwa wiki kwa muda wa nusu saa, kuzingatia ulaji wa vyakula unaofaa,kupunguza matumizi ya pombe kupita kiasi na kujiepusha na matumizi ya tumbaku.

 'Mazoezi nikuepukana na magonjwa’ Mzee Mwinyi miaka 91 sasa
Kwa upande wake Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi katika nasaha zake amewahimiza Watanzania kufanya mazoezi kwa ajili ya kulinda afya zao.
Amesema kama watanzania watafanya mazoezi wataepukana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwemo ugonjwa wa moyo,kisukari,uti wa mgongo na mifumo ya neva na figo.

Friday, December 16, 2016

KIWANDA KIKUBWA KUSINI MWA JANGWA LA SAHARA KITAKACHOZALISHA MARUMARU KINAJENGWA WILAYANI MKURANGA,MKOA WA PWANI

Kampuni ya Goodwill(Tanzania)Ceramic Co.Ltd ina milikiwa na Wangkang-Group ya nchini china inajenga kiwanda kikubwa kusini mwa Jangwa la Sahara kitakachozalisha Malumalu za aina zote katika wilaya ya Mkuranga,Mkoani Pwani KM 90 kutoka Dar es Salaam,kwasasa kiwanda hiki kina wafanyakazi wakitanzani 1000 na Wachina 100 mafundi na vibarua katika ujenzi huo,kitakapo kamilika kitatoa ajira kwa Watanzania zaidi ya 3000 na Wageni zaidi ya 300 hapo mwezi wa tatu.


                                                       Haya tunayaita MatokeoChanyA+








Tuesday, November 22, 2016

TAJIRI DAR ES SALAAM ABOMOA NYUMBA MBILI ZA WAALIMU,DC AAMURU WAHUSIKA WOTE WAKAMATWE MARA MOJ

Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mhe Hashim Mgandilwa aamuru akamatwe mara moja

Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mhe Hashim Mgandilwa, tarehe 22/11/2016 akiwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ametembelea shule ya Sekondari Kibada kujionea uharibifu wa kuvunjwa nyumba mbili za Walimu.

Uvunjaji wa nyumba hizo za Walimu Unadaiwa kufanywa na tajiri mmoja ambaye inasemekana amemilikishwa eneo hilo na anataka kuliendeleza.

DC Mgandilwa ameagiza waliohusika na uharibifu huo kukamatwa mara moja na kumtaka Mkurugenzi wa manispaa ya Kigamboni kufanya tathimini ya gharama za uharibifu huo ili zilipwe haraka na ujenzi mpya kuanza kwenye eneo ambalo halina mgogoro.

".....hata kama angelikuwa amemilikishwa eneo hilo kihalali, kitendo cha kujichukulia Sheria mkononi na kuvunja bila Utaratibu hakikubaliki.... ", alisema Mgandilwa.

Pia amesisitiza kuwa yeyote atakaye vamia eneo la shule au taasisi nyingine za kijamii serikali haitamfumbia macho.



WAKUU WA WILAYA 20 WANAJENGEWA UWEZO NCHINI CHINA

Mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo katika utendaji yameandaliwa na Wizara ya Biashara ya Watu wa China (Ministry Of Trade People's Republic of China),Mafunzo  yanachukua wiki mbili kuanzia tarehe 21 Novemba hadi Desemba 4, 2016.China na Tanzania ni ndugu tangu enzi Za waasisi wa Mataifa haya mawili.
Wakuu wa Wilaya 20 kutoka Wilaya mbalimbali Nchini, wakiwa katika Picha ya pamoja na wakufunzi wao huko Nanchang China.