focusmedia Search This Blog

Tuesday, November 22, 2016

TAJIRI DAR ES SALAAM ABOMOA NYUMBA MBILI ZA WAALIMU,DC AAMURU WAHUSIKA WOTE WAKAMATWE MARA MOJ

Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mhe Hashim Mgandilwa aamuru akamatwe mara moja

Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mhe Hashim Mgandilwa, tarehe 22/11/2016 akiwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ametembelea shule ya Sekondari Kibada kujionea uharibifu wa kuvunjwa nyumba mbili za Walimu.

Uvunjaji wa nyumba hizo za Walimu Unadaiwa kufanywa na tajiri mmoja ambaye inasemekana amemilikishwa eneo hilo na anataka kuliendeleza.

DC Mgandilwa ameagiza waliohusika na uharibifu huo kukamatwa mara moja na kumtaka Mkurugenzi wa manispaa ya Kigamboni kufanya tathimini ya gharama za uharibifu huo ili zilipwe haraka na ujenzi mpya kuanza kwenye eneo ambalo halina mgogoro.

".....hata kama angelikuwa amemilikishwa eneo hilo kihalali, kitendo cha kujichukulia Sheria mkononi na kuvunja bila Utaratibu hakikubaliki.... ", alisema Mgandilwa.

Pia amesisitiza kuwa yeyote atakaye vamia eneo la shule au taasisi nyingine za kijamii serikali haitamfumbia macho.



WAKUU WA WILAYA 20 WANAJENGEWA UWEZO NCHINI CHINA

Mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo katika utendaji yameandaliwa na Wizara ya Biashara ya Watu wa China (Ministry Of Trade People's Republic of China),Mafunzo  yanachukua wiki mbili kuanzia tarehe 21 Novemba hadi Desemba 4, 2016.China na Tanzania ni ndugu tangu enzi Za waasisi wa Mataifa haya mawili.
Wakuu wa Wilaya 20 kutoka Wilaya mbalimbali Nchini, wakiwa katika Picha ya pamoja na wakufunzi wao huko Nanchang China.





























Wednesday, November 16, 2016

HII NDIO TASWIRA YA RAIS WA TANZANIA DR.JOHN POMBE MAGUFULI


Novemba 30 mwaka jana Rais John Magufuli aliagiza kiasi cha shilingi bilioni nne kilichopangwa kutumika katika shamrashamra za siku ya Uhuru kitumike katika kazi ya upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco jijini Dar es salaam yenye urefu wa kilometa 4.3 ili kuiunganisha barabara hiyo na ile ya Mwenge – Tegeta yenye urefu wa KM 12 .Huu ni muonekano wa sasa baada ya maamuzi ya Rais Dr. Pombe Magufuli pamoja na kupendeza kumerahisha sana foleni iliyokuwa ikisumbua siku zote.

Thursday, November 10, 2016

WAANDAMANAJI WAPINGA USHINDI WA TRUMP MAREKANI

Maandamano ya kumpiga rais mteule wa marekani Donald Trump yanafanyika katika karibu miji saba ya Marekani siku moja tu baada ya ushindi wake kwenye uchaguzi ulokua na ushindani mkubwa katika historia ya karibuni ya taifa hili.
Maelfu ya watu wanaandamana New York, Chicago, Washington na miji mingine mitano Jumatano usiku ili kupinga kauli za kudhalilisha za rais mteule Trump aliyokua anatoa wakati wa kipndi cha kampeni za uchaguzi mkuu.
Huko Austin Texas wanafunzi wa chuo kikuu cha Austin waliandamana hadi bunge la jimbo wakibeba mabango yanayosema "yeye si rais wangu."
Mjini Nashville wanafunzi wengine wengi weusi wamekua wakisema wamechoshwa na ubaguzi na wanastahiki kupata maisha bora zaidi.
Maandamano mjini New York na Washington na Chcago yanafanyika mbele ya majengo ya Trump, yakifanyika kwa amani huku polisi wakihakikisha usalama usalama unadumishwa.
Waandamanaji wakiwa katika mtaa wa Fifth Avenue nje ya jengo la Trump Tower, New York.
Waandamanaji wakipita katika mtaa wa 57th Street mjini New York wakilekea hadi jengo la Trump Tower, Nov. 9, 2016.
Maandamano ya kumpinga Donald Trump mjini Los Angeles.
Waandamanaji wakifurika mtaa wa Fifth Avenue wakipinga ushindi wa Donald Trump nje ya jengo lake laTrump Tower in New York City, Nov. 9, 2016

Wednesday, November 9, 2016

TRA IMEFANIKIWA KUSHINDA KESI 9 DHIDI YA WAKWEPA KODI NCHINI

Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) imefanikiwa kushinda kesi 9 kati ya 10 zilizokuwa zikiendelea katika mahakama mbalimbali nchini dhidi ya walipa kodi wake na kufanikiwa kupata kiasi cha takribani Bilioni 16.9. Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi Richard Kayombo amewapongeza Mawakili na wanasheria wa ndani kwa kuonyesha uzalendo wa dhati kwa Taifa “Tumeshinda kwa juhudi za kizalendo za Timu nzima ya Wanasheria na watumishi wa TRA

Monday, November 7, 2016

TUOKOE TEMBO WETU

Miaka hamsini iliyopita, kulikuwa na Tembo 300,000 nchini Tanzania. Mwaka 2009, kulikuwa na Tembo 109,000. Leo, inakadiriwa kuna Tembo 43,000 tu waliobaki – upungufu wa asilimia 60 ndani ya miaka mitano tu
Utafiti mkubwa kuwahi kufanywa unaonyesha kuwa Idadi ya tembo barani Afrika inazidi kupungua kutokana na kuongezeka kwa vitendo vya ujangili ambavyoo vimewaangamiza tembo zaidi ya 140,000 kati ya mwaka 2007 na 2014
Kupatikana kwa miili ya tembo waliokufa ni ishara ya kupungua kwa idadi ya tembo huku ripoti hiyo ikizitaja nchi zinazoongoza kuwa vifo vya wanyama hao ni pamoja na Cameroon, Msumbiji, Angola na Tanzania. wakati nchi ambazo zinaongoza kwa pembe za ndovu ni Msumbiji, Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Saturday, November 5, 2016

MATEMBEZI YA HISANI KUSOMESHA WAUGUZI YAFANA JIJINI DAR,YAONGOZWA NA MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameongoza mamia ya wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam katika matembezi ya hisani ya kilomita 4.2 ya kuchangia fedha kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya mafunzo ya wauguzi, wakunga 400 katika ngazi mbalimbali kupitia mafunzo ya kimtandao yaani e-learning nchini.

Akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza katika matembezi hayo katika viwanja vya Green Ground, Oysterbay Jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wananchi kuwa Serikali ya awamu ya Tano imeweka mikakati madhubuti ya kukabiliana na changamoto mbalimbali katika sekta ya Afya ikiwemo kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto kwa kuongeza idadi ya wataalamu wa Afya na kuimarisha miundombinu pamoja na upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kote nchini.

Amesisitiza kuwa ili kuhakikisha huduma za Afya zinazotolewa kwa wananchi zinakuwa na ubora unaotakiwa Serikali itaendelea kusimamia uwajibikaji kwa watumishi na watoa huduma za Afya mpango utaenda pamoja na kuongeza vitanda kwenye wodi za wazazi na utoaji wa huduma ya Afya bure kwa makundi maalum.

Makamu wa Rais pia amehimiza wadau wa sekta binafsi waendelee kushirikiana na Serikali katika utoaji wa huduma za Afya kwa wananchi nchini ili kufikia malengo ya kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametumia sehemu ya hotuba yake kwa kulipongeza Shirika la AMREF Health Africa Tanzania kwa mipango yake ya kusaidia jamii ya Kitanzania kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa na shirika hilo ukiwemo mpango wa kugharamia masomo kwa njia ya ufadhili kwa wanafunzi wanaotoka kwenye familia duni kwa lengo la kuwawezesha kusomea cheti ya uuguzi ukunga.

Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa mipango na mikakati ya Serikali ya awamu ya Tano ni kuhakikisha vifo vya wanawake wajawazito na watoto nchini vinapunguzwa kwa kiwango kikubwa kutokana na Serikali kuendelea kutenga bajeti ya kutosha kwa Wizara ya Afya kwa ajili ya kununua vifaa tiba na kuongeza idadi ya wataalamu.

Katika harambee hiyo, Jumla ya shilingi milioni 290 zimechangwa na wadau wa maendeleo na lengo ni kukusanya shilingi milioni 500 fedha ambazo zitatumika kusomesha wauguzi 400 wakiwemo 50 kwa ngazi ya cheti na 350 kwa ngazi ya diploma kupitia mafunzo ya kimtandao yaani e-learning.