focusmedia Search This Blog

Wednesday, March 9, 2016

Rais Magufuli alipomtembelea Maalim Seif kumjulia hali720P






Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
amemtembelea na kumjulia hali Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Mheshimiwa Maalim Seif Shariff Hamad, katika Hoteli ya Serena Jijini
Dar es salaam, ambako anapata mapumziko baada ya kuruhusiwa kutoka
hospitali ya Hindu Mandal alikokuwa amelzwa kwa matibabu.


Pamojana kumpa mkono wa pole, Rais Magufuli amemuombea Maalim Seif Shariff
Hamad kupona haraka ili aweze kuendelea na shughuli zake kama
kawaida
.

"Nilishtushwasana na taarifa za kuugua kwako, lakini sasa nafurahi kukuona ukiwa
mwenye afya nzuri ikilinganishwa na taarifa nilizozipata hapo awali,
nakupa pole sana" amesema
Rais Magufuli wakati akimjulia hali hotelini hapo.


Kwaupande wake Maalim Seif Shariff Hamad amemshukuru Rais Magufuli kwa
ukarimu na upendo aliouonesha kwa kumtembelea hotelini hapo, na
amewahakikishia watanzania kuwa hali yake sasa inakwenda vizuri na
inazidi kuimarika kila kukicha.


"Sasahivi ninaweza kutembea vizuri, kufanya shughuli zote mwenyewe bila ya
msaada wa mtu yeyote yule, na ni matumaini yangu kwamba baada ya muda
mfupi, hali yangu itarudi kama kawaida, nije nishirikiane na
watanzania wenzangu katika kutekeleza majukumu ya nchi yetu"
Maalim Seif alimweleza Rais Magufuli.




Tuesday, March 1, 2016

UJENZI WA BOMBA LA MAJI KUTOKA RUVU CHINI


UJENZI BOMBA LA MAJI KUTOKA RUVU CHINI MPAKA DAR


 
mkandarasi ya kulaza bomba hilo
inaridhisha licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali zinazochelewesha
kazi hiyo zikiwemo za ufinyu wa eneo linapojengwa bomba hilo kuwezesha
mitambo kufanya kazi vizuri katika eneo la mbezi Beach, mvua
zinazoendelea kunyesha ,changamoto ya makazi ya watu kuwa ndani ya mradi
ambapo kulikuwa na kesi 17 Mahakamani zikihusisha madai mbalimbali ya
wananchi katika maeneo hayo. 

“Ni kweli zipo changamoto
zilizosababisha mradi kukawia kumalizika zikiwemo za wananchi kufungua
kesi 17  Mahakama ya Ardhi, hadi sasa DAWASA tumeshinda kesi 14  ndiyo
maana tumepata haki ya kutumia njia hii kukamilisha upanuzi wa mradi”
Amesema Mwang’ingo.



Ameongeza kuwa lengo la mradi huu
nikuongeza uzalishaji wa maji na kuboresha huduma kwa wakazi wa maeneo
ya uwekezaji (EPZ) Bagamoyo, Chasimba, Buma, Zinga, Kerege na Mpiji mkoa
wa Pwani.





Maeneo mengine yatakayonufaika na mradi
huo kwa Mkoa wa Dar es Salaam ni Bunju, Wazo, Salasala, Madale na
Kinzudi Mbezi Juu, Goba, Kawe, Makongo, Mwenge, Msasani, Mikocheni,
Mlalakua, Masaki, Sinza, Kijitonyama, Manzese, Konondoni, Magomeni,
Kigogo na Vingunguti.



Kwa upande wake Meneja Mradi wa Kampuni
inajenga bomba hilo nchini Muhandisi Eric Omuruli akizungumzia mradi huo
amesema kuwa yeye kama Meneja mradi atahakikisha anashughulikia
changamoto zilizopo ili kukamilisha kwa wakati.