focusmedia Search This Blog

Monday, January 30, 2017

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AHUTUBIA KATIKA KUTANGAZA JINA RASMI LA KITUO CHA AMANI NA USALAMA KILICHOPEWA JINA LA MWALIMU JULIUS NYERERE KATIKA MAKAO MAKUU YA UMOJA WA AFRICA (AU) ADDIS ABABA NCHINI ETHIOPIA JANUARI 29,2017

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia Viongozi Wakuu wa Mataifa mbalimbali hawapo (pichani) katika Jengo jipya la Kituo cha Amani na Usalama kilichopewa jina Rasmi la Mwalimu Julius Nyerere, Addis Ababa nchini Ethiopia
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Rais wa Kenya Mh. Uhuru Kenyatta mara baada ya kutangazwa rasmi kwa Jina la Mwalimu Julius Nyerere katika kituo hicho cha Amani na Usalama   
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Rais wa Rwanda Paul Kagame wakati wakielekea katika Kituo cha Amani na Usalama cha Makao Makuu ya Umoja wa Afrika kilichopewa jina la Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere, Addis Abba nchini Ethiopia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na viongozi wa mataifa mabalimbali wakiwa katika picha ya pamoja katika jengo jipya la kituo cha Amani na Usalama (JULIUS NYERERE) lililopo katika Makao makuu ya Umoja wa Afrika Addis Ababa nchini Ethiopia. Januari 29,2019

Sunday, January 29, 2017

TRENI YA ABIRIA (DELUXE) YAPATA AJALI IKITOKEA KIGOMA KUELEKEA DAR ES SALAAM

  • Kwenye ajali iliyotokea kuna Mabehewa ambayo yametoka nje ya reli na kuanguka lakini bahati nzuri kichwa cha Treni hakikuanguka
  • Abiria walihamishiwa kwenye Mabehewa ambayo hayakuanguka na wakaondoka na Treni hiyohiyo kuelekea Dar es salaam na  wamefika kwenye mida ya saa mbili usiku, 
  • katika eneo la tukio kuna Mabehewa ambayo yalitoka nje ya reli. Kilometa 73 kutoka Dar es salaam na ni maeneo ya Ngeta Ruvu na ajali hii ilitokea kwenye saa kumi kasoro jioni, kuhusu chanzo cha ajali….uchunguzi  unafanywa na  Wataalamu ndani ya kampuni ya TRL watatoa taarifa baada ya uchunguzi wao.
  • Njia ya Treni imeharibika sana na kuna Treni nyingine ya abiria itasafiri kutoka Dar es salaam kwenda bara kwahiyo  ndani ya saa 24 TRL wanafanya juhudi kurudisha njia ya Reli  ili abiria na Treni nyingine za mizigo ziweze kupita TRL inasema  mpaka saa tisa alasiri siku ya Jumatatu January 30 2017 Treni zipite kama kawaida
  • Maswali magumu tunapaswa kujiuliza Je hakuna ukaguzi wa njia zetu za Reli kabla na baada ya kupita treni
  • Ni hasara kiasi gani inalikabili shirika letu ukizingatia mabehewa haya ni mapya kabisaa









SERIKALI NCHINI TANZANIA IMEPONGEZA UPENDO,JITIHADA,USHIRIKIANO NA UMOJA ULIOFANYWA NA WATANZANIA MKOANI GEITA KATIKA KUWAOKOA WACHIMBAJI WADOGO WALIFUKIWA KWA MASAA 77 KATIKA MACHIMBO YA DHAHABU YA RZU KIJIJI CHA NYARUGUSU WILAYANI GEITA


Mawasiliano ya wachimbaji na waokoaji yalivyokuwa yakifanyika







           

Saturday, January 28, 2017

VYAMA VYA SIASA KAMA HAVITA BADILI MITAZAMO NA HALI YA SASA VIKO HATALINI KUFA,SHIBUDA

Mwenyekiti wa vyama vya Siasa Nchini John Shibuda amesema kutokana na utendaji wa Dr.John Pombe Magufuli na uelewa wa wananchi juu ya utenda wake kunahaja ya kubadilimifumo ya mtazamo na utendaji wa vyama ili kuendana na kile anachokifanya Rais Magufuli

Ni lazima tuwe na mapinduzi ya fikra amefafanua Shibuda,siasa si uadui ni kama wacheza mpira tu hukumbatiana na kupeana mikono pale mpira unapomalizika, Tarehe 29/1/2017 pale ukumbi wa Bunge nitatoa Dira ya sisa za kistaarabu,utendaji wa Rais Magufuli ni lazima tuwe na dira ya maono mapya ya utumishi wa baraza la vyama vya siasa Tanzania

 Mapinduzi ya Dola yanayofanywa na Rais Magufuli ni lazima vyama vya siasa kwenda sambamba na mageuzi hayo la si hivyo vitanyauka tu, Tarehe 29/1/2017 ndio kutajulikana kuishi hai kwa vyama vya Siasa Tanzania alimesisitiza alipokuwa akiongea na Focus Media

Saturday, January 21, 2017

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Tanzania itaendelea kudumisha,kuimarisha na kuendeleza mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na China kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa pande hizo mbili.


Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam katika sherehe ya maadhimisho ya mwaka mpya wa Kichina hapa nchini sherehe ambazo zimehudhuriwa na mamia ya raia wa China na Tanzania.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa China imekuwa mshirika na mdau mkubwa wa maendeleo hapa nchini na hali hiyo inatokana na mahusiano mema na mazuri yaliyopo kati ya nchi hizi Mbili.

Makamu wa Rais amemhakikishia Balozi wa China hapa nchini Dkt Lu Youging kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli itakuwa bega kwa bega na serikali ya China hasa katika uimarishaji wa sekta za biashara, utamaduni, elimu, afya  na masuala ya kijeshi kwa ajili ya maslahi na ustawi wa wananchi wa Tanzania na China.

Makamu wa Rais amesisitiza kuwa Tanzania itaendelea kujifunza mambo mengi kutoka China ili kuharakisha shughuli za maendeleo za wananchi kutokana na Taifa la China kupiga hatua kubwa ya kimaendeleo.

Amehimiza ubadilishanaji wa wataalamu kati ya Tanzania na China katika sekta mbalimbali kama hatua ya kuongeza kasi ya maendeleo kwa wananchi nchini.

Kwa Upande wake, Balozi wa China hapa nchini Dkt Lu Youging amepongeza hatua zinachukuliwa na serikali ya Tanzania katika kupambana na rushwa na ufisadi.

Dkt  Lu Youging amesema serikali ya China na raia wake wanafurahishwa na hatua hizo kwa sababu zinalenga kuondoa na kukomesha rushwa na ufisadi kwani tabia hizo zikiachwa ziendelee zinachangia kwa kiasi kikubwa kuzorotesha utoaji wa huduma bora na za msingi kwa wananchi.

Akizungumzia mwaka mpya wa Kichina hapa nchini Balozi huyo amesema maadhimisho hayo ni muhimu kwa sababu raia Wachina na Tanzania wanajumuika pamoja katika kubadilisha mawazo na kutakiana heri na mafanikio kwa mwaka 2017.

Balozi huyo wa Tanzania hapa nchini Dkt  Lu Youging pia amewashukuru wananchi wa Tanzania kwa kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Mnazi Moja katika kusheherekea sikukuu ya Mwaka mpya wa Kichina sherehe ambazo inapambwa na michezo mbalimbali ikiwemo sarakasi na vikundi vya ngoma asili kutoka China na maonyesho.

Katika Maadhimisho hayo, Balozi wa China nchini Tanzania Dkt  Lu Youging amemkabidhi Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mfano wa hundi ya shilingi milioni 70 fedha ambazo zitatumika katika ujenzi kwenye shule ya msingi Chato iliyopo mkoani Geita.
PICHA NA OFISI YA MAKAMO WA RAIS