focusmedia Search This Blog

Monday, January 23, 2023

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI KILICHOFANYIKA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.





 

SIASA ZA KIISTARABU ZA RAISI SAMIA NA KUMBUKUMBU YA TUKIO LA " DINNER TABLE BARGAIN 1790 " NCHINI MAREKANI

Ilikuwa Usiku Wa June 20, 1790 Wakati Mikutano Ya " Congress " Inafanyika Jijini Newyork .Thomas Jefferson Wakati Huo Akiwa Secretary Of The State( Baadae Raisi Wa Tatu Wa Marekani) Alipoamua Kuwaalika Chakula Cha Usiku Watu Wawili Alexander Hamilton Wakati Huo Akiwa Secretary Of Treasure  Na James Madison Mwakilishi Wa Jimbo La Virginia( Baadae Raisi Wa Nne Wa Marekani).

Ni Majadiliani Katika Kikao Hiki "Dinner Table Bargain Of 1790" Kilichoitishwa Na Jafferson Ndicho Kilicholeta Suluhu Hasa Baada Ya Madison Kukubali Hoja Ya Hamilton Na Kushawishi Majimbo Ya Kusini Kuunga Mkono Hoja Na Kwa Pamoja Kulijenga Taifa Lao Ambalo Leo Ni Moja Ya Mataifa Makubwa Na Yenye Nguvu Duniani.


Na Kassim Mpingi  Rufiji-Pwani 

Bila Shaka Taifa Linaunganishwa Na Siasa Za Umoja,Mshikamano,Kusameheana Na Kujenga Nchi Kwa Pamoja(4R).

Vyama Pinzani Baada Miaka Saba Vinaingia Tena Mtaani Kufanya Mikutano Na Kufurahi Matunda Ya Siasa  Safi Na Za Kiistarabu Za Raisi Samia .

Aina Hii Ya Siasa  Anayofanya Raisi Samia Imenifanya Nikumbuke Tukio Muhimu Katika Historia Ya Siasa Za Kiistarabu Duniani Lililotokea Nchini Marekani Mwaka 1790  Lijulikanalo Kama " Dinner Table Bargain " Au " Great Compromise Of 1790 "

Ilikuwa Usiku Wa June 20, 1790 Wakati Mikutano Ya " Congress " Inafanyika Jijini Newyork .Thomas Jefferson Wakati Huo Akiwa Secretary Of The State( Baadae Raisi Wa Tatu Wa Marekani) Alipoamua Kuwaalika Chakula Cha Usiku Watu Wawili Alexander Hamilton Wakati Huo Akiwa Secretary Of Treasure  Na James Madison Mwakilishi Wa Jimbo La Virginia( Baadae Raisi Wa Nne Wa Marekani).

Mualiko Huu Ulisukumwa Na Tofauti Kubwa Na Uhasama Uliokuwa Wakati Huo Katika Ujenzi Wa Taifa  La Marekani .

Tofauti Kubwa Iliyopelekea Kugawanyika Kwa Taifa Lao Ni Hoja Ya Hamilton Na Wenzake Kuwa Serikali Ya Shirikisho (F.G) Ibebe Madeni Ya Majimbo Yatokanayo Na Vita Vya Mapinduzi .Hoja Hii Ililigawa "Congress"  Majimbo Ya Kaskani Yaliunga Mkono Hoja Hii Kwa Vile Madeni Yao Yalikuwa Ni Makubwa Na Wasingeweza Kuyalipa  Huku Majimbo Ya Kusini Akiwemo Madison Wakipinga Kwa Kuwa Wao Walishalipa Madeni Yao.

Na Hoja Ya Pili Ilikuwa Wapi Yawe Makao Makuu Ya Taifa Lao La Marekani .

Ni Majadiliani Katika Kikao Hiki "Dinner Table Bargain Of 1790" Kilichoitishwa Na Jafferson Ndicho Kilicholeta Suluhu Hasa Baada Ya Madison Kukubali Hoja Ya Hamilton Na Kushawishi Majimbo Ya Kusini Kuunga Mkono Hoja Na Kwa Pamoja Kulijenga Taifa Lao Ambalo Leo Ni Moja Ya Mataifa Makubwa Na Yenye Nguvu Duniani.

Na Ni Katika Kikao Hii Ndio Maamuzi Ya Kuwa Makao Makuu Ya Taifa Lao Kuwa Newyork Yalifikiwa

Ndio Maana Tunasema Wakati Huu Nchi Inaunganishwa Na Siasa Za Kiistarabu Za Samia Kupitia Sera Yake Ya "4R" Ni Vyema Kukumbuka Moja Ya Tukio Muhimu Katika Historia Ya Siasa Za Kiistarabu Ulimwenguni.

" The Great Compromise of 1790 

Thursday, January 12, 2023

HISTORIA PANA YA ZANZIBAR NA TAWALA MBALI MBALI ZA KIFALME - SAYYID KHALIFA BIN HARUBU


Jina lake hasa ni Sayyid Khalifa bin Harub bin Thuwein bin Said bin Sultan bin Imam Ahmed bin Said bin Mohammed bin Ahmed bin Khelef bin Said Al Azdy.
alizaliwa Oman tarehe 26 mwezi wa Agosti mwaka 1879, mama yake alifariki mudamchache baada ya kujifungua,lipelekwa kulelewa kwenye kasri ya Sultan Sayyid Feisal bin Turki, ambae ndie mjomba wake na ndie alikuwa Sultan wa Muskat. 



Alipotimiza miaka 13 alilazimika kuja Unguja kwa babu yake Syd Hemed bin Thuwein, aliyekuwa mfalme wa Zanzibar wakati huo, aliyetawala mwaka 1893 mpaka mwaka 1896
Kwa hivyo yeye ni mjukuu khalisi wa Syd Thuwein, aliyetawala Oman, ambae Mwenyezi Mungu Alimtunukia watoto wengi , akiwemo Syd Harub na Syd
Hemed. Na Syd Harub alikufa akiwa kijana sana. 
Mama yake aliitwa Turkiya binti Syd Turky bin Said Sultan, Syd Turky ni mtoto wa 5 wa Syd Sutan, ambae aliwahi kutawala Oman mwaka 1871 akafa 1888, ambae ndie baba wa mama yake Syd Khalifa, na akaolewa na Syd Harub na akazaliwa yeye syd Khalifa.
Baada ya kufa baba yake Syd Khalifa alilelewa na babu yake Syd Turky na alilelewa pamoja na mjukuu mwengine wa Syd Turky yaani Syd Taimur na walilelewa kishujaa na mafunzo kede kede mpaka akapikika na alipokuja huku Zanzibar akazidi kuwa mahiri na mtaalam wa mengi, hasa  farasi.Siku aliyokuja hakuna
mtu yoyote aliyejuwa aliingia ghafla katika mwaka 1903, na meli aliokuja nayo ikiitwa Aboukir, kabla ya kuja Zanzibar alipitia Makka kwa ajili ya ibada ya Umra, mara ya pili alikwenda na shemeji yake Syd  Ali , na huko ndiko alipokutana na mkewe bi Matuka na wakapendana, ambae naye yeye alifuatana na harimu yake, kaka Ali bin Humud ambae nae pia aliwahi kuwa Sultan wa Zanzibar 
 


Syd Khalifa alifanya mambo mengi ikiwemo  michezo kama ya sailing, polo, tennis na mambo ya kidunia na ya kiakhera [Dini] alimradi  aliishi. Alihudhuria mabaraza mengi sana akiwa 
bado mtoto, kitu kilompelekea kuwa kiongozi mzuri baadae, na kumudu kukaa kwenye kiti cha usultani kwa muda mrefu zaidi. 
Aliowa alipotawala Syd Humud Baada ya kufa Syd Hemed, alimuowa yule yule mpenzi wake Sayyidah Matuka binti Humud, mtoto wa Syd Humud aliyezaa na mkewe Seyyidah Khoufara binti Majid bin Sutan.

Syd Khalifa alipata watoto wawili, baada ya kufa mmoja alizaliwa Syd Prince Sir Abdalla 12 feb 1910. 
na alipokufa Bi Matuka Ndipo alipomuowa Bi Nunuu binti Ahmed. 


Alitawala Zanzibar kuanzia tarehe 9 Disemba mwaka 1911 ,akiwa na miaka 32, ingawa kiti hicho ilikuwa atawale Syd Khalid bin Muhammed, 
lakini Bwana huyu alikataa kata kata kutawala na akajitia maradhi.






Alitawala kwa miaka 49  ni miaka mingi kuliko Sultani yoyote wazanzibar aliepeta kutawala, alifariki Dunia saa 9 alfajiri ya Jumapili ya tarehe 9 Oktober mwaka 1960, sawa sawa na Mwezi 17 Rabil Thani 1380 Hijra. Bwana huyu alikuwa akipendwa mno, kifochake ni moja ya vifo mashuhuri Duniani si Ulaya, si Bara hindi si Afrika wala Uarabuni kila alomfahamu alijuwa kuwa Zanzibar imeondokewa, kwani alikuwa ni mtu wa watu sana.

Wingereza inamtambua kama kiongo mshirika wa vita zoto miili za Dunia dhidi ya Wajerumani,Wamarekani wanamjua alipowaruhusu kujenga kituo kikubwa cha kuongozea safari za Anga pale Tunguu





 

Saturday, January 7, 2023

HOSPITALI YA KISASA KITOGANI,WILAYA YA KUSINI UNGUJA YAFUNGULIWA NA RAIS MWINYI













 Na Mwandishi wetu Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi afungua Hospitali ya  Kisasa ya Kitogani Wilaya ya Kusini  ,Mkoa wa Kusini Unguja.

Kufunguliwa kwa Hospitali hii  pia imeambatana na kufungwa kwa  Vifaa tiba vipya,Gari la kubebea wagonjwa,hospitali ipo tayari kutoa huduma tofauti,ikiwemo huduma za wagonjwa wa nje(OPD),Mama na Mtoto ,huduma za kliniki mbalimbali zikiwemo za Pua,Koo,Masikio ,Macho,Magonjwa yasio ya kuambukiza kama Sukari,shinikizo la damu ,huduma za madawa(pharmacy),huduma za Wagonjwa wanaolazwa ikiwemo ,Wodi za Watoto,Mama Wajawazito kabla na baada ya kujifungua,Watu wazima Wanawake na Wanaume,huduma za wagonjwa wa dharura na ajali,Wagonjwa mahututi(ICU),huduma za watoto njiti ,Wodi tatu za wagonjwa wenye mahitaji maalum ya  kujitenga(isolation) pia Kuna Theatres mbili (2)za kisasa, huduma za ushauri nasaha na kupiga vita vitendo vya udhalilishaji na huduma za uchunguzi ikiwemo Maabara ,Ultrasound,ECG na XRAYS.Kuna huduma za kisasa za Mfumo wa Tehama zikiwemo huduma za data,sauti na picha zitakazotumika katika kutoa elimu ya afya kwa wagonjwa na wananchi wanaofika katika hospitali hii,usajili wa mahudhurio ya wafanyakazi ,mifumo ya tahadhari ya moto ,Mfumo wa Nursing  call System na Mfumo wa kutunza taarifa za wagonjwa kieletroniki(EMR).

Hospitali itawahudumia Wananchi zaidi ya 52,850 wakaazi wa Wilaya ya Kusini na maeneo jirani,

Tuesday, January 3, 2023

RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN ATANGAZA KURUHUSU KUFANYIKA KWA MIKUTANO YA HADHARA KWA VYAMA VYA SIASA NCHINI, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi wa Vyama Vya Siasa kuhusiana na maamuzi ya Serikali ya kuruhusu kufanyika kwa Mikutano ya Hadhara kwa Vyama hivyo wakati wa Kikao kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 03 Januari, 2023.

 





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi wa Vyama Vya Siasa kuhusiana na maamuzi ya Serikali ya kuruhusu kufanyika kwa Mikutano ya Hadhara kwa Vyama hivyo wakati wa Kikao kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 03 Januari, 2023.

 


Sehemu ya Viongozi mbalimbali wa Vyama Vya Siasa 19 waliohudhuria Kikao kilichoitishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ikulu Jijini Dar es Salaam Dar es Salaam tarehe 03 Januari, 2023.

 






Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa mara baada ya Kikao na Viongozi wa Vyama vya Siasa Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 03 Januari, 2023.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. George Simbachawene, Msajili wa Vyama vya Siasa Mhe. Jaji Francis Mutungi, Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Mohammed Ally Ahmed pamoja na viongozi wa Vyama Vya Siasa mara baada ya Kikao Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 03 Januari, 2023.