focusmedia Search This Blog

Friday, September 22, 2017

JWTZ LAANZA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS DKT MAGUFULI LA UJENZI WA UKUTA MERERANI-SIMANJIRO MKOANI MANYARA


Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania JWTZ laanza kutekeleza agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli. Meja Jenerali Michael Isamuyo atua Mererani, Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara kwa helkopta na kukagua maeneo ambayo ukuta utaanza kujengwa mara moja. Wachimba na wananchi wa Manyara wafurahi na waahidi ushirikiano.
Helikopta iliyombeba Meja Jenerali Michael Isamuyo akitua Mererani, Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara kwa helkopta na kukagua maeneo ambayo ukuta utaanza kujengwa mara moja. Wachimba na wananchi wa Manyara wafurahi na waahidi ushirikiano. Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania JWTZ limenanza kutekeleza agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
 Helkopta iliyombeba Meja Jenerali Michael Isamuhyo ikitua katika uwanja wa wazi wa Mererani, Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara tayari kwa kukagua eneo litakalojengwa uzio kuzunguka kitalu A hadi D katika eneo la Madini la Tanzanite Mererani ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli
 Meja Jenerali Michael Isamuhyo akisalimiana na viongozi wa Wilaya ya Simanjiro na wananchi mara baada ya kutua katika uwanja wa wazi wa Mererani, Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara tayari kwa kukagua eneo litakalojengwa uzio kuzunguka kitalu A hadi D katika eneo la Madini la Tanzanite Mererani ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
  Meja Jenerali Michael Isamuhyo akisalimiana na baadhi ya wakazi wa eneo la Mererani,mara baada ya kutua katika uwanja wa wazi wa Mererani, Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara
 Meja Jenerali Michael Isamuhyo akipenya kwenye vichaka wakati wa kukagua eneo litakalojengwa ukuta.
  Meja Jenerali Michael Isamuhyo akitembelea na kuoneshwa eneo la vitalu A mpaka D katika eneo la machimbo ya Tanzanite Mererani wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara leo Septemba 21, 2017, tayari kwa kuanza kazi ya kujenga uzio kuzunguka eneo hilo kufuatia amri ya Rais Dkt John Pombe Magufuli aliyotoa jana ili kudhibiti biashara ya madini hayo yanayopatikana Tanzania pekee. 
 Meja Jenerali Michael Isamuhyo akioneshwa ramani ya vitalu A hadi D katika eneo la madini ya Tanzanite huko Mererani.
Meja Jenerali Michael Isamuhyo akitembelea na kuoneshwa eneo la vitalu A mpaka D katika eneo la machimbo ya Tanzanite Mererani wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara leo Septemba 21, 2017, tayari kwa kuanza kazi ya kujenga uzio kuzunguka eneo hilo kufuatia amri ya Rais Dkt John Pombe Magufuli aliyotoa jana ili kudhibiti biashara ya madini hayo yanayopatikana Tanzania pekee.

Wednesday, September 20, 2017

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AZINDUA BARABARA YA KILOMITA 26 YA KIA-MERERANI MKOA WA MANYARA SEPTEMBA 20,2017


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bi.Anna Mgwila mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro KIA na kuelekea Mererani wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara kwaajili ya ufunguzi wa barabara ya KIA – MERERANI yenye urefu wa km26. Septemba,20 ,2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mkuu wa mkoa wa Arusha Bw.Mrisho Gambio mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro KIAna kuelekea Mererani wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara kwaajili ya ufunguzi wa barabara ya KIA – MERERANI yenye urefu wa km26. Septemba,20 ,2017.
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembea pamoja  na wakuu wa mikoa ya Kilimanjaro na Arusha mata baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuelekea katika uzinduzi wa barabara ya lami ya kilomita 26 kutoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa kilimanjaro (KIA) katika mkoa wa Kilimanjaro hadi Mererani mkoani Manyara Septemba 20,2017
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa kwa furaha na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joel Bendera alipowasili kuzindua barabara ya lami ya kilomita 26 kutoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa kilimanjaro (KIA) katika mkoa wa Kilimanjaro hadi Mererani mkoani Manyara lSeptemba 20, 2017
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipungia maelfu ya wananchi alipowasili Mererani kuzindua barabara ya lami ya kilomita 26 kutoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa kilimanjaro (KIA) katika mkoa wa Kilimanjaro hadi Mererani mkoani Manyara Septemba 20,2017
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipungia maelfu ya wananchi alipowasili Mererani kuzindua barabara ya lami ya kilomita 26 kutoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa kilimanjaro (KIA) katika mkoa wa Kilimanjaro hadi Mererani mkoani Manyara Septemba 20,2017
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisoma moja ya mabango ya wananchi waliojitokeza  katika uzinduzi wa barabara ya lami ya kilomita 26 kutoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa kilimanjaro (KIA) katika mkoa wa Kilimanjaro hadi Mererani mkoani Manyara Septemba 20,2017
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiteta jambo na wakuu wa mikoa ya Manyara na Arusha katika uzinduzi wa barabara ya lami ya kilomita 26 kutoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa kilimanjaro (KIA) katika mkoa wa Kilimanjaro hadi Mererani mkoani Manyara Septemba 20,2017
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mbunge wa Simanjiro Mhe. James Ole Milya kwenye sherehe ya kuzindua barabara ya lami ya kilomita 26 kutoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa kilimanjaro (KIA) katika mkoa wa Kilimanjaro hadi Mererani mkoani Manyara Septemba 20, 2017.
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi wa Mererani wakati wa kuzindua barabara ya lami ya kilomita 26 kutoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa kilimanjaro (KIA) katika mkoa wa Kilimanjaro hadi Mererani mkoani Manyara Septemba 20, 2017.
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishangiliwa na wananchi wakati wa hotuba yake ya  kuzindua barabara ya lami ya kilomita 26 kutoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa kilimanjaro (KIA) katika mkoa wa Kilimanjaro hadi Mererani mkoani Manyara Septemba 20, 2017.
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizinfdua rasmi barabara ya lami ya kilomita 26 kutoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa kilimanjaro (KIA) katika mkoa wa Kilimanjaro hadi Mererani mkoani Manyara Septemba 20, 2017
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Ua Mbunge wa Simanjiro Mhe. James Ole Milya mara baada ya kuzindua barabara ya lami ya kilomita 26 kutoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa kilimanjaro (KIA) katika mkoa wa Kilimanjaro hadi Mererani mkoani Manyara Septemba 20, 2017.
PICHA NA IKULU


Friday, September 15, 2017

UKARABATI WA MAGARI CHAKAVU YA JESHI LA POLISI UNALETA... MATOKEO CHANYA+

UKARABATI WA MAGARI CHAKAVU YA JESHI LA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAAM, UNALETA... MATOKEO CHANYA+

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda amefanya Ziara ya Ukaguzi wa UKARABATI wa Magari mabovu 26 ya Jeshi la POLISI ambayo Hapo AWALI yalikuwa yamekaa kwa Muda Usiopungua miaka 5 Bila kufanya kazi, magari ambayo yalikuwa yakitumiwa na jeshi la Polisi katika Mkoa wa Dar Es salaam.

Magari hayo 26 sasa yamekamilika na yanatembea ambapo Muda ujao wa wiki mbili yatakabidhiwa Rasmi kwa ajili ya kuongeza na KUBORESHA ulinzi katika Mkoa wa Dar es salaam kutokana na Magari hayo kukarabatiwa kwa mfumo KISASA tofauti na ule wa AWALI.

Mhe Makonda amefurahishwa na hali ya magari hayo yalivyo kwa SASA kwani yanarejea baranarani uku akiwa amefanikiwa KUOKOA kiasi kikubwa cha Fedha ambacho kingelazimika kununua magari mengine.

"Wako baadhi ya wananchi WALIBEZA hili wazo langu la kuyakarabati magari haya kwa kiwango cha Kimataifa, lakini sasa nafurahi kuona ndoto yangu imekuwa kweli, hili ni jambo jema kwa mkoa wetu," amesema Makonda akiwa Kwenye Karakana inayokarabati Magari hayo, Mkoani Kilimanjaro.