focusmedia Search This Blog

Wednesday, June 21, 2017

MAGUFULI IS A REAL DEAL 04

UMOJA NI USHINDI KWA WATANZANIA WOTE

MAGUFULI IS A REAL DEAL

MAGARI MABOVU YA POLISI DAR KUTENGENEZWA

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM PAUL MAKONDA AWEZESHA UJENZI WA WADI ZA WA...

NCHI YANGU TANZANIA MENGI TUNAYO YA KUJIVUNIA

RC MAKONDA AWAAGIZA WAKURUGENZI WA MANISPAA KUTUMIA MFUMO WA KIELEKTONIKI (e-RCS) KUKUSANYA MAPATO

MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda akizingumza na Wakurugenzi wa Manispaa za Jiji la Dar es salaam alipotembelea Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Kumbukumbu (National Internet Data Center) kilichopo Kijitonyama. Picha Zote na Mathias Canal
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Kushoto) akimsikiliza kwa makini MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda alipotembelea Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Kumbukumbu (National Internet Data Center) kilichopo Kijitonyama. Mwingine ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Bi Theresia Mmbando (Kulia)
Wakurugenzi, Na Maofisa Biashara wa Manispaa za Jiji la Dar es salaam wakimsikiliza kwa makini MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda wakati wa kikao Cha pamoja katika Ukumbi wa Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Kumbukumbu (National Internet Data Center) kilichopo Kijitonyama.
MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda akizingumza na Wakurugenzi wa Manispaa za Jiji la Dar es salaam alipotembelea Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Kumbukumbu (National Internet Data Center) kilichopo Kijitonyama.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Kulia) akimsikiliza kwa makini MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda alipotembelea Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Kumbukumbu (National Internet Data Center) kilichopo Kijitonyama. Mwingine ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Ndg Aron Kagoromjuli
Na Mathias Canal, Dar es salaam
MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda amewaagiza Wakurugenzi wa Manispaa Jijini Dar es salaam kujiunga katika mfumo mpya wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wa ukusanyaji mapato kwa njia ya kielektroniki (e-RCS) ili serikali iweze kupata kodi stahiki kwa mujibu wa sheria.
Rc Makonda ametoa agizo hilo leo June 20, 2017 Jijini Dar es Salaam alipotembelea Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Kumbukumbu (National Internet Data Center) kilichopo Kijitonyama,  dhifa iliyohudhuriwa pia na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam, Wakurugenzi wa Manispaa sambamba na Maofisa Biashara wa Manispaa zote za Jiji la Dar es salaam.
Mhe Makonda alisema kuwa kujiunga katika mfumo huo Manispaa zote zitapata urahisi katika kuwahudumia wananchi sawia na kurahisisha kuboresha vyanzo vya mapato.
Alisema kuwa mfumo huo utaongeza Mapato katika Manispaa, Kuondoa usumbufu kwa wananchi ikiwemo kuepuka Rushwa, sambamba na Kuimarisha huduma kwa wananchi.
"Najua Kuna watu Jambo hili litawakwaza Sana hususani wale wapiga dili lakini niwahakikishie kuwa kuna umuhimu mkubwa Sana kujiunga na Mfumo huu wa kisasa wa kuhifadhi kumbukumbu kwani ni njia rahisi ya kutoa taarifa pia ni Mfumo mzuri kwa usalama wa Taifa" Alisisitiza Mhe Makonda
Wakurugenzi hao wameagizwa kutumia wiki moja kujadili namna gani ya kujiunga na Mfumo huo huku akielekeza Hadi kufikia Agosti Mosi mwaka huu Manispaa zote ziwe zimejiunga na Mfumo huo.
Aidha, Alisema kuwa Kujiunga na Mfumo huo wa serikali wa ukusanyaji Mapato kwa njia ya Kielektroniki itarahisisha umakini wa huduma hivyo kuachana na Mfumo wa zamani wa kutuma watu kutambua watu ambao leseni zao zimemaliza muda wa matumizi.
Alisema kuwa Jiji la Dar es salaam Lina vituo vya Daladala zaidi ya 800 hivyo endapo kama ukiwekwa mfumo mzuri wa ukusanyaji wa Mapato katika vituo hivyo itakuwa ni chanzo Cha upatikanaji wa mapato ya serikali.
Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa Njia ya kielektroniki ulizinduliwa June Mosi Mwaka huu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John pombe Magufuli ambaye aliambatana na Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine

ZIARA YA RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI MKOANI PWANI AZINDUA RASMI MRADI WA MAJI WA RUVU JUU MLANDIZI MKOANI PWANI PIA AZINDUA VIWANDA VINGINE MKOANI HUMO JUNI 21,2017







Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia kabla ya kuzindua Mradi wa maji wa Ruvu juu Mlandizi mkoani Pwani




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia hatua za usafishaji wa maji katika kituo cha kusafisha maji ya Ruvu juu Mlandizi Mkoani Pwani, kushoto ni Mtendaji mkuu wa DAWASCO Eng. Cyprian Luhemeja akitoa maelezo






Wananchi wakifuatilia Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wakati akiwahutubia mamia ya wananchi wa Mji wa Kibaha Mkoani Pwani June 20,2017. Rais Magufuli yupo Mkoani Pwani kwa Ziara ya siku tatu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza mwananchi Azilongwa Buhali alipokuwa akimuelezea shida yake mara baada ya kuhutubia wananchi wa Kibaha Mkoani Pwani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma pamoja na Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya mara baada uzinduzi wa mradi huo mkubwa wa kusafisha na kuzalisha Maji kwa miji ya Pwani na Dar es Salaam.


Waumini wa Kiislamu mkoa wa Pwani wakiswali swala ya Magharibi kabla ya kupata futari iliyoandaliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli katika Ikulu ndogo mjini Kibaha akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya siku tatu mkoani Pwani







Wednesday, June 14, 2017

RAIS MAGUFULI AMTOLEA UVIVU MZUNGU WA BARRICK

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AMEKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MWENYEKITI WA KAMPUNI YA BARRICK GOLD CORPORATION IKULU JIJINI DAR ES SALAAM JUNE 14,2017


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Ikulu Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mining Limited Prof. John L. Thorntonalipofika Ikulu kwa Mazungumzo, kulia ni Balozi wa Canada nchini Mhe. Ian Myles June 14, 2017


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na waandishi wa habari baada ya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation Prof. John L. Thornton alipofika Ikulu kwa Mazungumzo June 14, 2017 

Balozi wa Canada nchini Mhe. Ian Myles na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mining Limited Prof. John L. Thornton wakiongea na waandishi wa habari mara baada ya Mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu June 14, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na  Mwenyekiti wa Barrick  Gold Corporation  Profesa John L. Thornton baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es salaam  Juni 14, 2017. wakiwa na  Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi na Balozi wa Canada nchini Mhe. Ian Myles 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na  Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mining Limited Prof. John L. Thornton pamoja na Balozi wa Canada hapa nchini Mhe. Ian Myles na Waziri wa Sheria na Katiba Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiagana Mhe. Ian Myles balozi wa Canada Nchini pamoja na  Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mining Limited Prof. John L. Thornton alipofoika ikulu kwa mazungumzo juni 14,2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe akiwa na Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba kabudi  baada ya mazungumzo na Mwenyekiti wa  Barrick Gold Corporation ya Canada Profesa John L. Thornton  Ikulu jijini Dar es salaam  Juni 14, 2017. 

Tuesday, June 6, 2017

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan Ziarani mkoani Mara


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameuagiza uongozi wa wilaya ya Serengeti na wa mkoa Mara kukamilisha haraka awamu ya kwanza ya ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo ili kuondoa adha ya wananchi kusafiri kwenda mikoa ya jirani ya Arusha na Mwanza kwenda kupata huduma afya.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa agizo  6-June-2017 kwenye mkutano wa hadhara mjini Mugumu wilayani Serengeti mkoani Mara mara baada ya kutembelea ujenzi wa hospitali hiyo ya wilaya  na kuweka jiwe la msingi.

Makamu wa Rais amesema kutokana na wilaya ya Serengeti kupata wegeni wengi kutoka nje ya nchi ambao wanaenda kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti  hivyo ni muhimu kwa viongozi wa wilaya na mkoa kwa ushirikiano na wadau wa maendeleo kukamilisha ujenzi huo haraka ili wananchi waweze kupata huduma za afya za uhakika katika wilaya yao.

Makamu wa Rais amesema kukamilika kwa ujenzi huo wa awamu ya kwanza kutaondoa taabu kubwa wanayopata wananchi wa wilaya ya Serengeti katika kupata huduma ya afya karibu na maeneo yao.

Katika kuunga mkono jitihada hizo za ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Serengeti, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ameahidi kuchangia kiasi cha shilingi milioni Tano na amewaahidi wananchi wa wilaya ya Serengeti kuwa atakikisha fedha kutoka Serikalini ambazo zinatakiwa kupelekwa wilayani humo zinapelekwa haraka ili kukamilisha ujenzi huo.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan pia amewataka wananchi kote nchini kuunga mkono jitihada za Serikali za kupambana na rushwa na ufisadi ili kuhakikisha miradi inayotekelezwa inakuwa na manufaa kwa wananchi wote.

Amewaomba wananchi nchini wasirudi nyuma katika mapambano dhidi ya rushwa bali waendelee kubaini watu wanaofanya vitendo hivyo ili Serikali iweze kuwachukulia hatua kali za kisheria .

Kuhusu tatizo la mimba mkoani Mara, Makamu wa Rais ameonyesha kuchukizwa na vitendo hivyo na kuomba vyombo vya dola na wananchi kwa ujumla kushirikiana katika kukomesha mimba za utotoni mkoani Mara.

Kwa upande wake, Mkuu wa mkoa wa Mara Dkt Charles Mlingwa amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa maelekezo yote anayoyatoa katika ziara yake yatafanyiwa kazi ipasavyo ili kuondoa kero na changamoto zinazowakabili wananchi.

Mkuu huyo wa mkoa wa Mara ameomba wananchi wa Mkoa wa Mara kuwepa pembeni tofauti zao za kisiasa bali washirikiane na Serikali katika utekelezaji wa miradi yao ya maendeleo.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan bado anaendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Mara ambapo hapo kesho atafanya ziara katika wilaya za Butiama na Musoma mkoani Mara.