focusmedia Search This Blog

Monday, July 25, 2022

WIZARA YASAINI MAKUBALIANO NA KAMPUNI YA EXTENSIA YA UINGEREZA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi (Kulia) na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Extensia Limited, Bw. Tariq Malik wakitia saini Mkataba wa Makubaliano wa kuandaa Kongamano litakalowakutanisha wadau wa sekta ya mawasiliano wa ndani na nje ya nchi linalojulikana kama Connect To Connect, tukio lililofanyika  Julai 25, 2022 jijini Dodoma.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi (katikati) na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Extensia Limited, Bw. Tariq Malik wakitia saini Mkataba wa Makubaliano wa kuandaa Kongamano litakalowakutanisha wadau wa sekta ya mawasiliano wa ndani na nje ya nchi linalojulikana kama Connect To Connect. Anayeshuhudia kulia ni Mkurugenzi wa Sheria wa Wizara hiyo, Bi. Lugano Rwetaka. 


Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi akibadilishana nyaraka na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Extensia Limited, Bw. Tariq Malik wakati wa tukio la utiaji saini wa Mkataba wa Makubaliano wa kuandaa Kongamano litakalowakutanisha wadau wa sekta ya mawasiliano wa ndani na nje ya nchi linalojulikana kama Connect To Connect  Julai 25, 2022 jijini Dodoma.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi (Kulia) na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Extensia Limited, Bw. Tariq Malik wakionesha nyaraka zilizosainiwa za Makubaliano baina ya Wizara na Kampuni hiyo ya kuandaa Kongamano litakalowakutanisha wadau wa sekta ya mawasiliano wa ndani na nje ya nchi linalojulikana kama Connect To Connect  Julai 25, 2022 jijini Dodoma.

 


Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi akizungumza baada ya kusaini Mkataba wa Makubaliano na  Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Extensia Limited ya Uingereza, Bw. Tariq Malik (kushoto) wenye lengo la kuandaa Kongamano litakalowakutanisha wadau wa sekta ya mawasiliano wa ndani na nje ya nchi linalojulikana kama Connect To Connect   Julai 25, 2022 jijini Dodoma.


Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Extensia Limited ya Uingereza, Bw. Tariq Malik akizungumza wakati wa hafla fupi ya utiaji saini wa mkataba wa makubaliano baina ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Tewknolojia ya Habari na Kampuni ya Extensia Limited ya Uingereza  Julai 25, 2022 jijini Dodoma 


Picha ya pamoja ya baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara Dkt. Jim Yonazi (wa nne kushoto mstari wa mbele) na watendaji kutoka Kampuni ya Extensia Limited ya Uingereza wakiongozwa na Mtendaji Mkuu wa Kampunihiyo, Bw. Tariq Malik (wanne kulia mstari wa mbele kabla ya kusaini mkataba wa makubaliano baina ya Wizara na Kampuni hiyo wa kuandaa Kongamano litakalowakutanisha wadau wa sekta ya mawasiliano wa ndani na nje ya nchi linalojulikana kama Connect To Connect   Julai 25, 2022 jijini Dodoma.


 Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imesaini mkataba wa makubaliano na kampuni ya Extensia Limited ya Uingereza, lengo likiwa ni kuandaa Kongamano litakalowakutanisha wadau wa sekta ya mawasiliano wa ndani na nje ya nchi linalojulikana kama Connect To Connect.

 

Kongamano hilo pia linalenga kuzidi kukuza matumizi ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na kufungua wigo wa mifumo, ubunifu na uwekezaji katika TEHAMA.

 

Akizungumza wakati wa utiaji saini wa makubaliano hayo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonazi amesema  Kongamano la Connect To Connect (C2C) litafanyika kwa siku mbili tarehe 7 na 8 Septemba, 2022 ambapo nchi nyingi zinatarajiwa kushiriki ikiwa ni pamoja na nchi za ukanda wa Afrika ya Mashariki.

 

Amesema kuwa Tanzania inaunganisha nchi saba za jirani ambazo ni Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi, Zambia na Msumbiji  kupitia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano hivyo kuwa na fursa kubwa ya kupeleka huduma na kuchichimua uchumi kupitia TEHAMA.

 

Dkt. Yonazi ameeleza kuwa Kongamano litatoa pia fursa kwa nchi zitakazoshiriki kufanya majadiliano, kujifunza na kuweka mikakati ya teknolojia ya habari na mawasiliano katika kuchangia uchumi , kuongeza fursa za uwekezaji, ajira na elimu.

 

Naye Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Extensia Limited, Bw. Tariq Malik amesema kuwa 

Kongamano hilo lilifanyika Tanzania kwa miaka mitatu mfululizo kuanzia mwaka 2013 hadi 2015 na kuleta mafanikio makubwa. Aidha, Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Kongamano kwa mara nyingine ambapo itapaisha zaidi Tanzania kama kitovu cha mawasiliano. 

 

Kwa upande wa Mkurugenzi wa TEHAMA wa Wizara hiyo, Bw. Mulembwa Munaku amesema kuwa utiaji saini wa makubaliano hayo ni hatua ya awali ya kuanza maandalizi ya Kongamano kubwa litakalowakutanisha wadau wa sekta ya mawasiliano zaidi ya 300 kutoka ndani na nje ya nchi.

 

Naye Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Habari- MAELEZO,Bw. Gerson Msigwa ameipongeza Wizara kwa juhudi za kuweka mifumo imara ambayo itasaidia kutimiza malengo ya Serikali ya kuinua uchumi wa nchi kupitia matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

WAZIRI NDALICHAKO AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA USWISI NCHINI TANZANIA


Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot akieleza jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (hayupo pichani). 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akimkaribisha Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot   tarehe 25 Julai, 2022 katika ofisi ndogo za Ofisi hiyo Jijini Dar es salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akiwa na   Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot pamoja na ujumbe wake  leo tarehe 25 Julai, 2022, mara baada ya kukutana naye katika ofisi ndogo za Ofisi hiyo Jijini Dar es salaam.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akifafanua jambo kwa  Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot  tarehe 25 Jula, 2022, alipomtembelea katika ofisi ndogo za Ofisi hiyo Jijini Dar es salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akiwa na   Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot  tarehe 25 Julai, 2022, mara baada ya kukutana naye katika ofisi ndogo za ofisi hiyo Jijini Dar es salaam.

 

RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AHUTUBIA KWENYE SIKU YA MASHUJAA JIJINI DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye Viwanja vya Mashujaa Jijini Dodoma kwa ajili ya kushiriki katika Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa tarehe 25 Julai, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama kwa ajili ya Heshima ya Wimbo wa Taifa wakati ukipigwa kwenye Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa Jijini Dodoma tarehe 25 Julai, 2022.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka silaha za jadi (Ngao na Mkuki) kwenye mnara wa Mashujaa kuadhimisha Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mashujaa Jijini Dodoma tarehe 25 Julai, 2022.








Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi kwenye Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mashujaa Jijini Dodoma tarehe 25 Julai, 2022.

 





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka wakati akiondoka katika viwanja vya Mashujaa Jijini Dodoma tarehe 25 Julai, 2022.






 

Thursday, July 21, 2022

WAKUU WA NCHI ZA EAC WASISITIZA UMUHIMU WA SOKO LA PAMOJA KATIKA KUKUZA UCHUMI WA KIKANDA

 

Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wamesisitiza umuhimu wa soko la pamoja katika kukuza uchumi wakati waliposhiriki Mkutano Maalum wa Ngazi ya Juu wa Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mkutano huo maalum wa ngazi ya Wakuu wa Nchi uliofanyika tarehe 21 Julai 2022 na mkutano maalum wa ngazi ya Mawaziri uliofanyika tarehe 20 Julai 2022 jijini Arusha ni sehemu ya mikutano ya awali kuelekea Mkutano wa 22 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika tarehe 22 Julai 2022.

Katika mkutano huo Wakuu wa Nchi walijadili na kuyawekea msisitizo masuala mbalimbali ya hali ya halisi ya utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki sambamba na kuainisha changamoto zinazohitaji ufumbuzi wa pamoja katika kuyafikia malengo ya jumuiya hiyo.

Akichangia mada wakati wa mkutano huo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni mwenyeji wa mkutano huo, amesisitiza juu ya kukuza uzalishaji pamoja na  kuongeza thamani ya mazao na bidhaa  zinazozalishwa ndani ya jumuiya ili kuweza kuingia katika ushindani wa kibiashara kimataifa.

Aidha, aliongeza kufafanua kuwa katika kuyafikia malengo ya pamoja ni muhimu kwa nchi wanachama kuwekeza katika amani na utawala bora ili nchi ziweze kuongeza nguvu katika usimamizi wa rasilimali na uzalishaji badala ya kuwekeza katika migogoro.

Naye Mwenyekiti wa mkutano huo na Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Uhuru Kenyatta amesisitiza umuhimu wa kuwa na mawasiliano kupitia ujenzi wa miundombinu ambao ndio msingi mkuu wa kuyafikia malengo ya soko la pamoja.

Vilevile akaeleza kwa sasa nchi wanachama zimeunganishwa kupitia ujenzi wa miundombinu ya kisasa na akatolea mfano ujenzi wa reli ya kisasa unaofanywa na Tanzania ambao utaziunganisha nchi wanachama na kwamba kwa upande mwingine Tanzania na Kenya zinaunganishwa kupitia ujenzi wa miundombinu uliofanywa mipakani katika eneo la Namanga na Taveta.

Maeneo mengine yaliyojadiliwa ni pamoja na fursa za kiuchumi zilizoongezeka kufuatia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kujiunga na jumuiya hiyo, umuhimu wa usimamizi wa rasilimali kama vile madini na umuhimu wa ushiriki wa sekta binafsi katika kuyafikia malengo yaliyowekwa.

Kadhalika, mkutano huo ulijadili mafanikio yaliyofikiwa na jumuiya hiyo ikiwemo, uhuru wa kufanya biashara, mtangamano wa kijamii na fursa za kuvuka mipaka kupitia Hati ya kusafiria ya kielektroni ya Afrika Mashariki na kuondoleana visa miongozi mwa nchi wanachama.

Mkutano huo umehudhuriwa na Nchi zote saba wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao ni pamoja mwenyekiti wa mkutano huo Jamhuri ya Kenya; Mwenyeji wa mkutano huo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Jamhuri ya Uganda; Jamhuri ya Burundi, Jamhuri ya Rwanda, Jamhuri ya Sudan Kusini, na Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo. Pia ulihudhuriwa na Jamhuri ya Shirikisho la Somalia ambaye alikuwa mgeni mwalikwa katika mkutano huo.

==========================================================



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwatambulisha viongozi mbalimbali wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Uhuru Kenyatta baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Arusha tarehe 21 Julai 2022.
Mhe. Kenyatta yupo nchini kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 22 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika tarehe 22 Julai 2022.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine aliposhiriki Mkutano Maalum wa Ngazi ya Juu wa Soko la Pamoja la Afrika Mashariki uliofanyika tarehe 21 Julai 2022 jijini Arusha.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Peter Mathuki akimkaribisha Waziri anayeshughulikia masuala ya Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini, Mhe. Barnaba Marial Benjamin mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha kushiriki Mkutano Maalum wa Ngazi ya Juu wa Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika tarehe 21 Julai 2022 jijini Arusha.
Mhe. Benjamin anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini, Mhe. Salva Kiir katika mkutano huo pamoja na Mkutano wa 22 wa Wakuu wa Nchi wa EAC .



Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mwigulu Nchemba akifafanua kwa wananchi juu ya umuhimu wa soko la pamoja na fursa zake kwa taifa na wanachi wa Tanzania kwa ujumla kupitia kituo cha Luninga cha TBC1 .

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akifafanua juu ya fursa za biashara na uwekezaji zinazopatikana katika Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa wananchi kupitia kituo cha Luninga cha TBC1.

Sehemu ya wajumbe wa mkutano huo wakifatilia majadiliano ya Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika.
Wapili kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi akifuatilia Mkutano Maalum wa Ngazi ya Juu wa Soko la Pamoja la Afrika Mashariki uliofanyika tarehe 21 Julai 2022 jijini Arusha.

MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ASHIRIKI MKUTANO WA 22 WA WAKUU WA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (EAC) JIJINI ARUSHA TAREHE 21 JULAI, 2022

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika Mkutano wa 22 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ulionza tarehe 21 Julai, 2022 Jijini Arusha
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha AICC kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 22 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ulionza tarehe 21 Julai, 2022 Jijini Arusha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza  na Rais wa Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha AICC kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 22 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ulionza tarehe 21 Julai, 2022 Jijini Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na baadhi ya Viongozi Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na Wawakilishi wakati wa Wimbo wa Taifa wa Afrika Mashariki ukipigwa kwenye ukumbi wa Mikutano wa AICC Jijini Arusha kabla ya kuanza kwa Kikao cha Wakuu hao wa Nchi tarehe 21 Julai, 2022.

MAKAMU WA RAIS AKIWASILI KATAVI KWA ZIARA YA KIKAZI

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango leo tarahe 21 Julai 2022 akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mpanda mkoani Katavi kwaajili ya ziara ya kikazi ya siku nne mkoani humo.



















Wednesday, July 20, 2022

MAADHIMISHO YA SIKU YA IDADI YA WATU DUNIANI KITAIFA YAFANA MANYARA

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa pili kushoto), akiwasili katika viwanja vya shule ya Msingi Katesh B Wilayani Hanang’, mkoani Manyara, katika kilele cha siku ya maadhimisho ya Idadi ya Watu Duniani, wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa huo, Bw. Makongoro Nyerere.


Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiwataka wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la Sensa ya watu na Makazi itakayfanyika tarehe 23 Agostu, 2022 ili kupata takwimu sahihi za idadi ya watu ili kurahisisha mipango ya maendeleo, wakati wa kilele cha siku ya maadhimisho ya Idadi ya Watu Duniani, Wilayani Hanang’, mkoani Manyara.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akiteta jambo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA), Bw. Mark Bryan Schreiner, wakati wa kilele cha siku ya maadhimisho ya Idadi ya Watu Duniani, ikliyofanyika kitaifa Wilayani Hanang’, mkoani Manyara.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Frederick Sumaye, wakiangalia alizeti iliyozalishwa kwa kutumia mbegu ya kisasa, wakati wa kilele cha siku ya maadhimisho ya Idadi ya Watu Duniani, iliyofanyika kitaifa Wilayani Hanang’, mkoani Manyara.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akicheza ngoma ya kikundi cha utamaduni cha kabila la Kiiraq cha Gehandu kutoka Wilaya ya Hanang mkoani Manyara, wakati wa maadhimishi ya kilele cha siku ya Watu Duniani, iliyofanyika kitaifa Wilayani Hanang mkoani Manyara.


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Lawrence Mafuru, wakifurahia jambo na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Mipango ya Kitaifa wa Wizara hiyo, Bw. Royal Lyanga, wakati wa kilele cha siku ya maadhimisho ya Idadi ya Watu Duniani,iliyofanyika Wilayani Hanang’, mkoani Manyara.