focusmedia Search This Blog

Saturday, July 2, 2016

RAIS WANGU MAGUFULI UMEMSIKIA HUYU?




















Maxcom Africa ltd inauwezo wa kuhakikisha kwamba mapato
yanakusaywa moja kwa moja kwenda TRA bila TRA kuendelea kusubiri wakusanyaji
wapeleke mapato TRA, kwani mara nyingine yanacheleweshwa kufika serekalini kwa
sababu za kibinadamu. Amesema inawezekana kwamba mapato yanayotakiwa kulipwa
serekalini yanalipwa  mojakwamoja kutoka
kwa Mnunuzi yanafika TRA kwa wakati kwa njia ya mtandao popote nchini.

Ukweli kuhusu Maxcom na TRA - Part 2


Ukweli kuhusu Maxcom
na TRA

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Maxcom Africa Ndugu Juma
Rajabu amefafanua mkataba  wake na
Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)  [CONTRACT AGREEMENT FOR THE PROVISION OF
CHARGES AND TAX PAYMENT SYSTEM SERVICE AND SMS INFORMATION SERVICES. NO.
AE/023/2013-14/HQ/G/001 wa Oktoba 2013.]

Akizungumza na Focus Media amesema kwamba haoni kosa lake na
wala hajasikia ametajwa popote kwamba ameshindwa kutekeleza matakwa ya mkataba
wake na mteja wake (TRA). Kwani anatekeleza jukumu lake na amefanikiwa kwa
kiasi kikubwa kuondoa kero zilizokuwa zinawasibu walipa kodi nchi hasa kodi za
magari. Ameongeza ukusanyaji wa mapato kwa kiasi kikubwa na inalipwa  kwa wakati muafaka.

“Mambo yanayoendelea kuandikwa yenye nia ya kuichafua
kampuni ya Maxcom ni chuki ya ushindani wa kibiashara kwani hata viambatanisho
vilivyowekwa kwamba kuna wakubwa wanailinda kampuni sio vya kweli kwani
Ukiangalia barua inayotoka kwa OS kuja kwetu iliandikwa May 19, 2014 tukiwa na
miezi 6 tu kazini. Je inahusikaje kuwekwa hapa kama kielelezo kwamba “wakubwa”
wanatutetea kuongezewa muda wa kufanya kazi kinyume cha sharia?” Anahoji

Mambo yanayosemwa na kuandikwa yanatakiwa yakosoe utendaji
kazi wa Maxmalipo na sio kuingilia mkataba wake na mteja wake kwa kuhoji ninani
amewapa kazi na wamefikaje hapo. “Wahusika (TRA) wanaweza kujibu baadhi ya
maswali yanayoulizwa kwani wanafahamu utekelezaji wetu. Ninaomba jamii IPUUZE
UWONGO HUU WENYE LENGO LA KUTUKATISHA TAMAA katika juhudi za kuwabana wakwepa
kodi na kukusanya kodi” amasema Ndgu Rajabu.

Maxcom imesaidia sana TRA kugundua wamiliki wa Kadi bandia
za kumiliki magari ambao walikuwa wakizitumia katika malipo bandia kwa kukwepa kodi.

Vilevile Maxcom ndio waliobuni mfumo wa kutoza faini za papokwahapo
kwa kutumia mashine maalum barabarani. Mifumo ambayo imelisaidia sana jeshi la
polisi kuongeza mapato yake ambayo wanayaona. Vilevile mfumo huu unawaondoa watumiaji
wa leseni bandia za Udereva waliokuwa wanaikosesha serekali mapato.

Mafanikio mengine ni kuwezesha ukusanyaji wa mapato na
ulipaji wa kodi kupiti a mabasi yaendeyo kasi (UDART), vivuko mbalimbali nchini
kama Magogoni na Busisi Mkoani Mwanza mabako mapato yameongezeka kwa kiasi kikubwa,
na tumerahisisha manunuzi ya umeme (LUKU) maji na huduma nyingine nyingi
kwakutumia simu ya mkononi au Mawakala wa Maxmalipo nchi nzima.

Hata hivyo amepongeza jitihada za Rais wa jamhuri ya
muungano ya Tanzania Dr. Magufuli za kukusanya kodi na jinsi anavyoamini kwamba
nchi hii haitakiwi kuwa tegemezi bali inatakiwa kuwa nchi ya kutoa misaada.

Amefafanua kwamba Maxcom Africa ltd inauwezo wa kuhakikisha
kwamba mapato yanakusaywa moja kwa moja kwenda TRA bila TRA kuendelea kusubiri
wakusanyaji wapeleke mapato TRA, kwani mara nyingine yanacheleweshwa kufika
serekalini kwa sababu za kibinadamu. Amesema inawezekana kwamba mapato
yanayotakiwa kulipwa serekalini yanalipwa 
mojakwamoja kutoka kwa Mnunuzi yanafika TRA kwa wakati kwa njia ya
mtandao popote nchini.

Hivyo amemuomba Mheshimiwa Rais azidi kuwapa Fursa zaidi
wazawa washirikiane na Serekali ili kukusanya mapato ya ndani kwa lengo la
kufika kule tunapotarajia.

Kampuni ya maxcom Africa Ltd kwa sasa imetoa ajira rasmi
zaidi ya mia tano (500) na ajira zisizo rasmi zaidi ya elfu ishirini (20,000)
kote nchini, zikiwa ni ajira kwa wakala, wafanyakazi katika vituo mbalimbali
vya usafiri na usafirishaji kama ferry, DART na sehemu mbalimbali za malipo.



































































Hivi sasa maxcom Afica ltd inafanya kazi katika nchi
nyingine kama Uganda, na Rwanda (MaxPay)