focusmedia Search This Blog

Sunday, March 5, 2017

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI ATEMBELEA KIWANDA CHA SARUJI CHA DANGOTE PIA AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA KUSAMBAZA UMEME KATIKA MIKOA YA MTWARA NA LINDI MARCH 5,2017

Rais Dkt. Magufuli  akiwa na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote wakipeperusha bendera kuashiria uzinduzi rasmi wa Magari  580.

Rais Dkt. Magufuli akizungumza jambo na mmiliki  wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote.

Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote akimuonesha Rais Dkt. Magufuli sehemu ya Kiwanda hicho pamoja na vifaa vyake mkoani Mtwara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote mara baada ya kuwasili kiwandani hapo kwa ajili ya kuzindua magari 580 ya kusafirisha saruji nchini.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote mara baada ya kumkabidhi barua ya malalamiko kutoka kwa madereva wanaolalamikia utoaji wa ajira hizo kiwandani hapo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika viwanja hivyo vya kiwanda cha Dangote kabla kuzindua magari 580 ya kiwanda hicho yatakayosafirisha saruji nchini.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote mara baada ya kukagua kiwanda chake cha Saruji mkoani Mtwara.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Magari makubwa ya kusafirishia Saruji kiwanda hapo. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego March 5, 2017

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiweka jiwe la msingi Mradi wa Kituo cha kupooza umeme kwa ajili ya kuusambaza katika mikoa ya Lindi na Mtwara. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo March 5, 2017

No comments:

Post a Comment