focusmedia Search This Blog

Thursday, March 30, 2017

MIEZI MINNE BAADA YA UZINDUZI WA NDEGE MBILI ZA ATCL(BOMBARDIER),WAKUSANYA BILIONI TISA


Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la ATCL anasema wamefanikiwa kukusanya Shilingi Bilioni 9 kwa Miezi minne tu kwa kutumia Ndege hizo mbili zilizonunuliwa na Rais Magufuli, nakuleta utata mkubwa na wapinzani wa siasa nchini waliodai kuwa hazikuwa na tija kwa Taifa.

Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) ilianzishwa mwezi Novemba 2002 baada ya Serikali kubinafsisha lililokuwa Shirika la Ndege la Tanzania (Air Tanzania Corporation, ATC); katika Shirika hilo, Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) lilinunua hisa asilimia 49 ndani ya ATC. Hata hivyo ubia kati ya ATCL na SAA ulikabiliwa na matatizo ya kiuendeshaji na kulazimika kusitishwa mwezi Agosti 2006 na ATCL kurejeshwa tena Serikalini kwa asilimia 100.


Monday, March 27, 2017

RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI APOKEA RIPOTI YA MDHIBITI NA MKAGUZI WA MKUU WA HESABU ZA SERIKALI (CAG), IKULU JIJINI DAR ES SALAAM MARCH 27,2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Nakala ya Vitabu vya Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es Salaam March 27,2017

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa anapiga makofi pamoja na Katibu Mkuu Ikulu, Alphayo Kidata mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kupokea Ripoti hiyo kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad mara baada ya kupokea ripoti hiyo Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahi pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad mara baada ya kupokea ripoti hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa na Katibu Mkuu wa Ikulu Alphayo Kidata pamoja na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Ripoti hiyo kutoka kwa CAG Ikulu jijini Dar es Salaam.

Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad akizungumza kabla ya kuwasilisha Ripoti hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kupokea Ripoti hiyo ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es Salaam.

Maafisa kutoka katika Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wakifatilia kwa makini wakati wa uwasilishwaji wa Ripoti hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam.

MH. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA JUMUIYA YA WANAWAKE WALIOJIAJIRI (SEWA) KUTOKA INDIA

SEWA – “Self Employed Women Association” ni Jumuiya ya Wanawake Waliojiajiri ambayo miongoni mwa viongozi wake wakuu ni Bi. Renana Jhabvala (Chair Women in Informal Employment WIEGO).  

Aidha, Bi Renana na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais JMT ni miongoni mwa viongozi wakuu wa  Jopo la Juu Duniani katika Kuwezesha Wanawake Kiuchumi chini ya Umoja wa Mataifa.

Ushirikiano wa viongozi hawa unandelea kuleta mafanikio makubwa kwa Wanawake hasa wa ngazi ya chini hapa Tanzania.

Baada ya ujumbe huo kutua Tanzania tangu tarehe 21 – 26 Machi, 2017, wanawake wa Zanzibar na Tanzania Bara wamepata mafunzo mbalimbali kupitia vikundi vyao vya ujasiriamali. Taasisi zilizoshiriki ni TEWO SACCOS, JUWABIKA, UWAKE, BACCA, BAMITA na MKUDUWODEA.

Mhe. Makamu wa Rais baada ya kukutana na ujumbe huo tarehe 27/3/2017 ukioongozwa na “Deputy High Commissioner” India Bw. Robert Shetkintong, akiongozana na Shree Kumar anayemuwakilisha Renana Jhabvala, Pushpa Rathod , Sophia Kinega kiongozi wa wanawake waliojiajiri  na Mhe. Siriel Mchembe msaidizi wa Mama Samia kwenye jopo la juu la dunia katika kuwezesha wanawake kiuchumi amekubali kuanzisha Jumuiya hiyo hapa Tanzania.

Mchakato wa kuanzisha Jumuiya  ya wanawake waliojiajiri India na Tanzania (SEWA) unaanza mara moja chini ya ulezi wake.Wanawake waliojiajiri Tanzania hongereni kwa kupata sauti Duniani.


Mh Makamu wa Rais akipokea taarifa ya ziara kutoka kwa Shree Kumar anayemuwakilisha Renana Jhabvala pamoja na Pushpa Rathod - SEWA


Makamu wa Rais baada ya kuvishwa alama ya heshima kwa mila za Kihindi kutoka kwa Pushpa Rathod 


“Deputy High Commissioner” India Bw. Robert Shetkintong,wa pili kutoka kulia mwenye suti katika picha ya pamoja na  Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassa, Shree Kumar anayemuwakilisha Renana Jhabvala, Pushpa Rathod , Sophia Kinega kiongozi wa wanawake waliojiajiri  na Mhe. Siriel Mchembe msaidizi wa Mama Samia kwenye jopo la juu la dunia katika kuwezesha wanawake kiuchumi amekubali kuanzisha Jumuiya hiyo hapa Tanzania.



Thursday, March 23, 2017

RAIS MHE. DKT.JOHN POMBE MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA BANDARINI NA KUZUIA MAKONTENA 20 YENYE MCHANGA WA MADINI ULIOKUWA USAFIRISHWE NJE YA NCHI MARCH 23,201


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Dar es Salaam kufatilia maagizo yake ya kudhibiti vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na wafanyabiashara wanaogiza na kusafirisha vitu mbalimbali nje ya nchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akihesabu makontena 20 yenye mchanga wa madini ambapo ameamuru kontena hizo zisisafirishwe mahali popot

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Dar es Salaam kufatilia maagizo yake ya kudhibiti vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na wafanyabiashara wanaogiza na kusafirisha vitu mbalimbali nje ya nchi.



Makontena 20 yenye mchanga wa madini yakiwa yamezuiwa kusafirishwa nje ya nchi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mara alipofanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Dar es Salaam.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akikagua nyaraka mbalimbali zenye kuhusu makontena ambayo husafirishwa nje ya nchi katika Bandari ya Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia baadhi ya magari yalivyoingizwa nchini kwa njia isiyo halali ya kudai kuwa ni makontena ya mitumba wakati ndani yake wanaficha magari yakifahari pamoja na vitu vilivyochakaa March 23,2017

Moja ya kontena likiwa lina gari ndani yake aina ya Range Rover ambapo muagizaji alidai kuwa anaagiza mitumba lakini kumbe ndani yake wanakuwa wameficha magari ya kifahari.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na IGP Ernest Mangu mara baada ya kufanya ukaguzi Bandarini hapo.

Picha na lkulu

Monday, March 20, 2017

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA BARABARA ZA JUU (INTERCHANGE) KWENYE MAKUTANO YA UBUNGO MARCH 20,2017





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim wakiwa wamepanda basi la mwendokasi huku wakibadilishana mawazo wakielekea Ubungo kuweka jiwe la Msing la ujenzi wa barabara za juu (Interchange) kwenye makutano ya Ubungo March 20,2017

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim baada ya kuweka jiwe la Msingi ujenzi wa barabara za juu (Interchange) kwenye Makutano ya Ubungo March 20,2017


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kabla ya kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa barabara za juu (Interchange) kwenye makutano ya Ubungo March 20,2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilia Prof. Makame Mbarawa kwa Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim walipokwenda kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa barabara za juu (Interchange) kwenye makutano ya Ubungo March 20,2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kabla ya kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa barabara za juu (Interchange) kwenye makutano ya Ubungo March 20,2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim wakipata maelezo jinsi barabara za juu (Interchange) kwenye makutano ya Ubungo zitakavyokuwa baada ya kujengwa March 20,2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali baada ya kuweka jiwe la Msingi ujenzi wa barabara za juu (Interchange) kwenye Makutano ya Ubungo March 20,2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim wakifungua kitambaa ikiwa ni ishara ya kuweka jiwe la Msing la ujenzi wa barabara za juu (Interchange) kwenye makutano ya Ubungo March 20,2017

PICHA NA IKULU

Saturday, March 18, 2017

RAIS DKT. MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA AFYA WA KENYA KUHUSU TANZANIA KUPELEKA MADAKTARI 500(WASIO NA AJIRA SERIKALINI) KWENDA KUFANYA KAZI NCHINI KENYA



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu aliyefika Ikulu pamoja na ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu kuhusu Tanzania kupeleka madaktari 500 nchini Kenya, Ajira za Madaktari hao zitatangazwa mara moja na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu na zitawahusu Madaktari ambao hawajaajiriwa Serikalini(hawapo katika utumishi wa umma au taasisi za serikali) waliomaliza mafunzo kwa vitendo na ambao wamesajiliwa na Baraza la Madaktari la Tanganyika.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na ujumbe kutoka nchini Kenya uliongozwa na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Gavana wa Kisumu County Jack Rangumba ambaye aliambatana na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu Ikulu jijini Dar es Salaam.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu aliyeambatana pamoja na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu akizungumza na Wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akizungumza kuhusu Kutangaza ajira za Madaktari wapatao 500 ambao watakwenda kufanya kazi nchini Kenya. Ajira hizo zitawahusu Madaktari ambao hawajaajiriwa Serikalini(hawapo katika utumishi wa umma au taasisi za serikali. PICHA NA IKULU.