Generali Fransis Njie kutoka Jeshi la Senegal ndie ataongoza kikosi cha wanajeshi 860 kutoka jeshi la Nigeria,Wanajeshi 500 kutoka jeshi la Senegal na Makomandoo 60 ambao wanaunda kikosi cha Jumuia ya Afrika Magharibi ECOWAS katika kile kinachooneka kumwondoa kwa nguvu mamlakani Bwana Yahya Jammeh amabae amekataa kuachia madaraka baada ya kushindwa katika uchaguzi Nchini Gambia na Rais mteule Bwana Adama Barrow
Gambia inawanajeshi 2,500 tu na tayari Mkuu wa Majeshi Nchini humo Generali Ousman Badjie amenukuliwa na AFP akionya hata ruhusu wanajeshi wake kuuingia kupambana na majeshi ya ECOWAS akisema Ni mzozo wa kisiasa na hata ruhusu wanajeshi wake kupigana,"Ninawapenda na sitaruhusu wapigane na majeshi ya Ecowas kama yataingia Gambia"alinukuliwa akisema
|
Bwana Yahya Jammeh |
No comments:
Post a Comment