Air Tanzania ( ATCL) kuanza safari mpya ya
ndege kutoka Dar es salaam kwenda Dodoma
kupitia Kigoma mara tano kwa wiki. Njia hiyo inatajwa kwenda kufungua fursa
mbali mbali za kiuchumi kuanzia katikati ya Januari mwaka huu, imefahamika.
Akizungumza na Focus Media Pro LTD, kwenye mahojiano
maalum jana katika makao makuu ya ofisi
za ATCL Jijini Dar es salaam, Afisa Masoko
wa ATCL , Lily FungaMtama amesema
Safari ya Dodoma inaenda kuwa mkombozi wa usafiri kwa wafanyabiashara, wakulima
wanafunzi na wabunge.
‘’Tumejipanga
kwa mwaka huu kuwaunganisha na fursa zilizopo Dodoma kwa kusafiri kwa nafuu
bilakuchoka; kwa wakulima, wafanyabiashara, wabunge, wanafunzi watatumia ndege
ya ATLC kwenda na kutoka Dodoma mara tano kwa wiki karibuni na bei ni nafuu sana
ya Tsh 180,000’’. Alisema Lily na kuongeza kuwa abiria anaruhusiwa kubeba
kilo20 ya mzigo mkononi ni kilo saba na unaweza kununua tiketi kupitia bank na
mitandao ya simu
No comments:
Post a Comment