JAJI PROF. IBRAHIM KITAALUMA ANA
1.Bachelor of Laws,UDSM
2.LLM,UDSM
3.Specialist,Law of Sea,LLM Ghent University,Belgium
4.Master of Laws(international Human Rights Law) Raoul Wallenberg University,Lund,Sweden wanaojua hiki ni moja ya vyuo bora zaidi vya Haki za Binadamu Ulaya
5.PhD,Law of sea,Ghent University,Belgium
Jaji Prof Ibrahimu ni mwanazuoni mbobevu katika sheria za Bahari,ni kati ya wasomi wachache walioko Tanzania wenye utaalamu huo wa Sheria za Bahari akiwemo Prof Mahalu na Prof. Nasila Rembe kwa wale waliopitia vyuoni hasa upande wa sheria za Bahari,Haki za Binadamu,Sheria za Wakimbizi na Sheria za Mazingira wanamtambua Prof Ibrahimu kwa Machapisho na maandiko yake ambayo yanatumika na kila mwanafunzi.
Weledi wake katika Sheria utaleta mwanga mpya katika muhimili huu wa Mahakama ameapishwa kukaimu nafasi ya ujaji Mkuu wakati Taifa likikabiliana na vita dhidi ya Ubadhirifu,uhujumu uchumi vikiwemo ujangili,Rushwa na ukiukwaji wa Maadili kwa baadhi ya watendaji wa Umma kwa Kifupi Mtihani alionao ni kurejesha imani kwa wananchi juu ya watendaji wa Mahakama kuzingatia Sheria,Haki na Wajibu,Pongezi Jaji Prof Ibrahim Juma
No comments:
Post a Comment