"Kuanzia siku ya leo na kuendelea itakuwa Marekani kwanza," rais huyo kutoka chama cha Republican aliwaambia maelfu ya watu waliokusanyika katika uwanja wa taifa kumshuhudia akichukua madaraka kutoka kwa Barack Obama wa chama cha Democratic.
Pamoja na Obama na marais wengine wa zamani watatu wakiwa wameketi karibu, Trump aliushutumu uongozi wa zamani wa Marekani wa kuwatajirisha maafisa mjini Washington kwa mgongo wa familia zenye matatizo nchini Marekani.
Rais Trump aliongezea kwa kusema kuwa hafla ya kuapishwa kwake si ya kuhamisha uongozi kutoka kwa chama kimoja kwenda kingine ila tu ni kuhamisha madaraka kutoka Marekani kwenda kwa wamarekani.
Marekani ya sasa itaendeshwa kwa msemo wa Trump ''Buy American Hire American'' akimaanisha kuwa bidhaa nyingi zitakuwa zikitengenezwa Marekani hivyo basi kuongeza ajira kwa raia wengi wa Marekani.
Kuanzia sasa itakuwa Marekani kwanza Marekani kwanza.
Trump ameaongeza,''Tutaungaunisha ulimwengu dhidi ya ugaidi,amabao tutauangamiza kabisa duniani.
Maandamano dhidi ya Trump yalifikia hali ya purukushani kubwa mjini Washington. Wanaharakati waliovalia mavazi meusi walivunja madirisha ya vioo ya maduka , walizuwia magari kupita na kupambana na polisi wa kuzuwia ghasia ambao walijibu kwa kurusha mabomu ya kutoa machozi na mabomu ya kushitua. Polisi walisema zaidi ya watu 200 walikamatwa.
Wakati Trump akiapishwa maandamano yalikuwa yakiendelea mjini Washington waandamanaji wakipinga kuchaguliwa kwake.Picha zinajieleza hali halisi ya viongozi hao wawili katika taifa lenye nguvu kubwa Duniani
No comments:
Post a Comment