focusmedia Search This Blog

Friday, October 14, 2022

RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. HUSSEIN ALI MWINYI, AKIWA KATIKA SIKU YA TATU YA ZIARA YAKE NCHINI OMAN

Alishuhudia utiaji saini wa hati za ushirikiano baina ya Zanzibar na Oman. 

Hati hizo zinahusu masuala ya Miundo Mbinu ya TEHAMA, ambapo  Dk. Khalid  Salum Mohamed,  Waziri Wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi ametia saini kwa niaba ya Serikali ya Zanzibar. 

Hati nyingine ilikuwa inahusu Elimu ya Juu, ambapo Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Saada Mkuya Salum ametia saini kwa niaba ya Serikali ya Zanzibar,  ambapo hati zinazohusu mpango wa utekelezaji wa hati za ushirikiano kuhusu utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka ambao umesainiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Utalii, Fatma Mbarouk Khamis. 

Hati nyingine za ushirikiano zilihusu Urithi na Mambo ya Kale ambapo Dk. Saada Mkuya Salum ametia saini na kumalizia na  hati ya  Ushirikiano inayohusu uwekaji Mifumo ya Mapato ya Kidijitali. 

📆 13 Oktoba, 2022 

📍Muscat, Oman.















No comments:

Post a Comment