focusmedia Search This Blog

Saturday, October 1, 2022

KILIMO KIDIGITALI, WAKULIMA MILIONI 1.3 TANZANIA WAMEHUISHA TAARIFA ZAO

 Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema Wizara hiyo imeanza usajili wa Wakulima kwa mwezi mmoja sasa na wamefikia takribani Wakulima Milioni 1.3 kwenye mfumo na 50% wamepata namba zao za siri na namba maalumu (unique identity number).


Wakulima wengi wenye umri mdogo ni wanawake, na sasa tunaona ongezeko la wakulima wenye mashamba yenye ukubwa wa hekari 5 hadi 50. Ukodishaji wa mashamba umeanza kuonekana umeongezeka kwenye mashamba makubwa kuanzia hekari 10-300.


wakulima wengi waliosajiliwa wana utambulisho (NIDA), taswira inaonyesha zaidi ya asilimia 70 wana umri wa kati 18-50yrs ,kwamba ile dhana kuwa kilimo kimetawaliwa na mababu inaonekana kuwa sio sahihi.




No comments:

Post a Comment