Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi tarehe 12 Oktoba, 2022 amehudhuria mkutano mkubwa wa jukwaa la Biashara lililowaleta pamoja wafanyabiashara na wawekezaji mbalimbali
Katika mkutano huo Rais Dk Mwinyi, aliwahakikishia usalama wafanyabishara wa vitega uchumi vyao kwani kwa sasa Zanzibar kisiasa imeimarika kisiasa baada ya mivutano ya muda mrefu hali iliyosababisha kuundwa kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa
Mh. Rais Dk pia alitumia jukwaa hilo la wafanyabiashara kuutangaza uchumi wa buluu kwa kuwaalika katika Utalii ukiwemo ule wa fukwe utalii wa kujionea urithi wa kuvutia wa Zanzibar ikiwemo utamaduni wake, na utalii wa michezo na mikutano mikubwa.
No comments:
Post a Comment