Ambapo baada ya kukutana na Mtawala wa Oman Mh. Sultan Haitham bin Tariq kwa mazungumzo yaliyofanyika katika Kasri la Sultani la Al Barakah alielekea kutembelea Msikiti Mkubwa unaojulikana kama Grand Mosque ambapo alitembezwa na kushuhudia maajabu ya ukubwa wa Msikiti huo unaovutia.
Ziara yake ya leo iliyojaa harakati nyingi ilimchukua hadi katika majengo yanayohifadhi nyaraka mbalimbali za kale zikiwemo za Zanzibar eneo limaloitwa GHALA.
Baada ya hapo akaelekea katika jengo kubwa la Kifalme linalotumika kwa ajili ya maonesho ya muziki na sanaa. Ni jengo la kisasa kwa wale wanaovutiwa na sanaa za maonesho.
Baadae alitembelea Jumba la Makumbusho ya Taifa liitwalo Oman National Museum.
No comments:
Post a Comment