Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mhe Hashim Mgandilwa aamuru akamatwe mara moja
Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mhe Hashim Mgandilwa, tarehe 22/11/2016 akiwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ametembelea shule ya Sekondari Kibada kujionea uharibifu wa kuvunjwa nyumba mbili za Walimu.
Uvunjaji wa nyumba hizo za Walimu Unadaiwa kufanywa na tajiri mmoja ambaye inasemekana amemilikishwa eneo hilo na anataka kuliendeleza.
DC Mgandilwa ameagiza waliohusika na uharibifu huo kukamatwa mara moja na kumtaka Mkurugenzi wa manispaa ya Kigamboni kufanya tathimini ya gharama za uharibifu huo ili zilipwe haraka na ujenzi mpya kuanza kwenye eneo ambalo halina mgogoro.
".....hata kama angelikuwa amemilikishwa eneo hilo kihalali, kitendo cha kujichukulia Sheria mkononi na kuvunja bila Utaratibu hakikubaliki.... ", alisema Mgandilwa.
Pia amesisitiza kuwa yeyote atakaye vamia eneo la shule au taasisi nyingine za kijamii serikali haitamfumbia macho.
No comments:
Post a Comment