Maandamano ya kumpiga rais mteule wa marekani Donald Trump yanafanyika katika karibu miji saba ya Marekani siku moja tu baada ya ushindi wake kwenye uchaguzi ulokua na ushindani mkubwa katika historia ya karibuni ya taifa hili.
Maelfu ya watu wanaandamana New York, Chicago, Washington na miji mingine mitano Jumatano usiku ili kupinga kauli za kudhalilisha za rais mteule Trump aliyokua anatoa wakati wa kipndi cha kampeni za uchaguzi mkuu.
Huko Austin Texas wanafunzi wa chuo kikuu cha Austin waliandamana hadi bunge la jimbo wakibeba mabango yanayosema "yeye si rais wangu."
Mjini Nashville wanafunzi wengine wengi weusi wamekua wakisema wamechoshwa na ubaguzi na wanastahiki kupata maisha bora zaidi.
Maandamano mjini New York na Washington na Chcago yanafanyika mbele ya majengo ya Trump, yakifanyika kwa amani huku polisi wakihakikisha usalama usalama unadumishwa.
Waandamanaji wakiwa katika mtaa wa Fifth Avenue nje ya jengo la Trump Tower, New York.
Waandamanaji wakipita katika mtaa wa 57th Street mjini New York wakilekea hadi jengo la Trump Tower, Nov. 9, 2016.
Maandamano ya kumpinga
Donald Trump mjini Los Angeles.
Waandamanaji
wakifurika mtaa wa Fifth Avenue wakipinga ushindi wa Donald Trump nje ya jengo
lake laTrump Tower in New York City, Nov. 9, 2016
Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) imefanikiwa kushinda kesi 9 kati ya 10 zilizokuwa zikiendelea katika mahakama mbalimbali nchini dhidi ya walipa kodi wake na kufanikiwa kupata kiasi cha takribani Bilioni 16.9.Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi Richard Kayombo amewapongeza Mawakili na wanasheria wa ndani kwa kuonyesha uzalendo wa dhati kwa Taifa “Tumeshinda kwa juhudi za kizalendo za Timu nzima ya Wanasheria na watumishi wa TRA”
Miaka hamsini iliyopita, kulikuwa na Tembo 300,000 nchini Tanzania. Mwaka 2009, kulikuwa na Tembo 109,000. Leo, inakadiriwa kuna Tembo 43,000 tu waliobaki – upungufu wa asilimia 60 ndani ya miaka mitano tu
Utafiti mkubwa kuwahi kufanywa unaonyesha kuwa Idadi ya tembo barani Afrika inazidi kupungua kutokana na kuongezeka kwa vitendo vya ujangili ambavyoo vimewaangamiza tembo zaidi ya 140,000 kati ya mwaka 2007 na 2014
Kupatikana kwa miili ya tembo waliokufa ni ishara ya kupungua kwa idadi ya tembo huku ripoti hiyo ikizitaja nchi zinazoongoza kuwa vifo vya wanyama hao ni pamoja na Cameroon, Msumbiji, Angola na Tanzania. wakati nchi ambazo zinaongoza kwa pembe za ndovu ni Msumbiji, Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameongoza mamia ya wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam katika matembezi ya hisani ya kilomita 4.2 ya kuchangia fedha kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya mafunzo ya wauguzi, wakunga 400 katika ngazi mbalimbali kupitia mafunzo ya kimtandao yaani e-learning nchini.
Akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza katika matembezi hayo katika viwanja vya Green Ground, Oysterbay Jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wananchi kuwa Serikali ya awamu ya Tano imeweka mikakati madhubuti ya kukabiliana na changamoto mbalimbali katika sekta ya Afya ikiwemo kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto kwa kuongeza idadi ya wataalamu wa Afya na kuimarisha miundombinu pamoja na upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kote nchini.
Amesisitiza kuwa ili kuhakikisha huduma za Afya zinazotolewa kwa wananchi zinakuwa na ubora unaotakiwa Serikali itaendelea kusimamia uwajibikaji kwa watumishi na watoa huduma za Afya mpango utaenda pamoja na kuongeza vitanda kwenye wodi za wazazi na utoaji wa huduma ya Afya bure kwa makundi maalum.
Makamu wa Rais pia amehimiza wadau wa sekta binafsi waendelee kushirikiana na Serikali katika utoaji wa huduma za Afya kwa wananchi nchini ili kufikia malengo ya kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametumia sehemu ya hotuba yake kwa kulipongeza Shirika la AMREF Health Africa Tanzania kwa mipango yake ya kusaidia jamii ya Kitanzania kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa na shirika hilo ukiwemo mpango wa kugharamia masomo kwa njia ya ufadhili kwa wanafunzi wanaotoka kwenye familia duni kwa lengo la kuwawezesha kusomea cheti ya uuguzi ukunga.
Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa mipango na mikakati ya Serikali ya awamu ya Tano ni kuhakikisha vifo vya wanawake wajawazito na watoto nchini vinapunguzwa kwa kiwango kikubwa kutokana na Serikali kuendelea kutenga bajeti ya kutosha kwa Wizara ya Afya kwa ajili ya kununua vifaa tiba na kuongeza idadi ya wataalamu.
Katika harambee hiyo, Jumla ya shilingi milioni 290 zimechangwa na wadau wa maendeleo na lengo ni kukusanya shilingi milioni 500 fedha ambazo zitatumika kusomesha wauguzi 400 wakiwemo 50 kwa ngazi ya cheti na 350 kwa ngazi ya diploma kupitia mafunzo ya kimtandao yaani e-learning.
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amesema kuwa Kenya ndio mshirika nambari moja wa Tanzania katika uwekezaji na biashara barani Afrika.
Akizungumza katika ikulu ya rais jijini Nairobi mda mfupi baada ya kuwasili nchini Kenya,Rais Magufuli amesisitiza kuwa hakuna taifa jingine ambalo limewekeza nchini mwake kama Kenya.
Amesema kuwa kulingana na rekodi za uwekezaji nchini Tanzania kuna takriban kampuni 529 nchini humo kutoka Kenya ambazo zinaingiza takriban dola bilioni 1.7 kila mwaka huku takriban Watanzania 57,260 wakiwa wameajiriwa.
Rais huyo vilevile ametoa wito kwa Wakenya wanaotaka kuwekeza nchini Tanzania kuharakisha hatua hiyo.
Aidha ameongezea kuwa amekuwa akiwasiliana na rais Uhuru Kenyatta mara kwa mara na kiwakosoa wale wanaodhani kwamba uhusiano wake na rais wa Kenya una utata.
RAIS wa Tanzania John Pombe Magufuli amesema kuwa Kenya ndio mshirika nambari moja wa Tanzania katika uwekezaji na biashara barani Afrika. Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amesema kuwa Kenya ndio mshirika nambari moja wa Tanzania katika uwekezaji na biashara barani Afrika.
Akizungumza katika ikulu ya rais jijini Nairobi mda mfupi baada ya kuwasili nchini Kenya,Rais Magufuli amesisitiza kuwa hakuna taifa jingine ambalo limewekeza nchini mwake kama Kenya.
Amesema kuwa kulingana na rekodi za uwekezaji nchini Tanzania kuna takriban kampuni 529 nchini humo kutoka Kenya ambazo zinaingiza takriban dola bilioni 1.7 kila mwaka huku takriban Watanzania 57,260 wakiwa wameajiriwa.
Rais huyo vilevile ametoa wito kwa Wakenya wanaotaka kuwekeza nchini Tanzania kuharakisha hatua hiyo.
Aidha ameongezea kuwa amekuwa akiwasiliana na rais Uhuru Kenyatta mara kwa mara na kiwakosoa wale wanaodhani kwamba uhusiano wake na rais wa Kenya una utata.Ikulu Nchini Tanzania Imetoa Taarifa kwa vyombo vya habari nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewakaribisha wawekezaji kutoka nchi ya Finland kuja kuwekeza katika sekta mbalimbali nchini ikiwemo ya nishati katika kipindi hiki wakati ambapo taifa la Tanzania linaelekea katika uchumi wa viwanda.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Finland Vesa Viitaniem
Makamu wa Rais amesema kuwa mkakati wa sasa wa Serikali ni kuhakikisha taifa linajitosheleza ipasavyo katika nishati ya umeme hatua ambayo itasaidia wawekezaji wengi kutoka mataifa mbalimbali Duniani kuja kuwekeza nchini kutokana na nchi kuwa na umeme wa kutosha na wa uhakika utakaotumika katika viwanda vitakavyojengwa katika maeneo mbalimbali Nchini.
Makamu wa Rais pia ameishukuru Serikali ya Finland kwa kuendelea kuisaidia Tanzania katika Nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na kuwezesha makundi mbalimbali ya kijamii hapa nchini ikiwemo ya wanawake,yatima na vijana.
Makamu wa Rais amemweleza Balozi huyo kuwa kwa sasa jitihada kubwa za Serikali ya awamu ya Tano zimeelekezwa katika uimarishaji wa miundombinu ikiwemo reli, bandari na barabara ili kurahisisha usafiri na usafirishaji wa bidhaa mbalimbali kote Nchini.
Kwa upande wake, Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Finland Vesa Viitaniem amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa nchi ya Finland itaendelea kushirikiana na Serikali katika kusaidia uimarishaji wa huduma bora kwa wananchi ikiwemo kuwezesha wajasiriamali ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Mahusiano mazuri kati ya Tanzania na Finland yamewezesha Watanzania zaidi ya 500 kuishi nchini humo kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo za kimasomo.
Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Finland Vesa Viitaniem aliongozana na Mke wa Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mama Anna Mkapa.
Katika kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli alilolitoa Machi 16,2016 wakati anawaapisha wakuu wa mikoa kuhusu utekelezaji wa elimu bila malipo,Rais aliwataka wakuu hao wa mikoa kuhakikisha wanasimamia upatikanaji wa madawati ifikapo Juni mwaka huu. Mkoa wa Mtwara chini ya uongozi wa mkuu wa mkoa huo Mheshimiwa Halima Dendego umedhamiria kukamilisha suala la madawati ifikapo Mei 2016 kwa Halmashauri zote tisa zinazounda mkoa huo Masasi mji ikiwemo kutumia njia mbalimbali ili wanafunzi wote wakae kwenye madawati. Katika kikao kilichoitishwa Februari, mwaka huu na mkuu wa mkoa wa Mtwara baada ya kubaini changamoto hizo, wakurugenzi wa halmashauri na wakuu wa wilaya waliagizwa kuhakikisha wanashughulikia changamoto hizo hasa uhaba wa madawati ambapo kwa ujumla mkoa wa Mtwara una upungufu wa madawati 35,406. Kwa upande wa Halmashauri ya mji wa Masasi tayari mchakato wa upatikanaji wa madawati hayo umeanza kwa kutumia rasilimali zilizopo pamoja na mapato ya ndani sambamba na kushirikisha wadau mbalimbali wa maendeleo zikiwemo taasisi za serikali,taasisi binafsi za kifedha,wafanyabiashara pamoja na wananchi wote kwa ujumla kwa lengo la kuhakikisha kuwa ifikapo Mei 2016 watoto wote wanaokaa chini wa madawati.
Mkoa wa Arusha ni moja kati ya mikoa 30 ya Tanzania. Imepakana na Kenya upande wa kaskazini. Mikoa ya jirani ni kufuatana na mwendo wa saa: Kilimanjaro, Manyara, Shinyanga na Mara. Mkoa wa Arusha ni Mkoa wa pili kwa Utajiri nchini Tanzania.
Maxcom Africa ltd inauwezo wa kuhakikisha kwamba mapato
yanakusaywa moja kwa moja kwenda TRA bila TRA kuendelea kusubiri wakusanyaji
wapeleke mapato TRA, kwani mara nyingine yanacheleweshwa kufika serekalini kwa
sababu za kibinadamu. Amesema inawezekana kwamba mapato yanayotakiwa kulipwa
serekalini yanalipwamojakwamoja kutoka
kwa Mnunuzi yanafika TRA kwa wakati kwa njia ya mtandao popote nchini.
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Maxcom Africa Ndugu Juma
Rajabu amefafanua mkatabawake na
Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) [CONTRACT AGREEMENT FOR THE PROVISION OF
CHARGES AND TAX PAYMENT SYSTEM SERVICE AND SMS INFORMATION SERVICES. NO.
AE/023/2013-14/HQ/G/001 wa Oktoba 2013.]
Akizungumza na Focus Media amesema kwamba haoni kosa lake na
wala hajasikia ametajwa popote kwamba ameshindwa kutekeleza matakwa ya mkataba
wake na mteja wake (TRA). Kwani anatekeleza jukumu lake na amefanikiwa kwa
kiasi kikubwa kuondoa kero zilizokuwa zinawasibu walipa kodi nchi hasa kodi za
magari. Ameongeza ukusanyaji wa mapato kwa kiasi kikubwa na inalipwa kwa wakati muafaka.
“Mambo yanayoendelea kuandikwa yenye nia ya kuichafua
kampuni ya Maxcom ni chuki ya ushindani wa kibiashara kwani hata viambatanisho
vilivyowekwa kwamba kuna wakubwa wanailinda kampuni sio vya kweli kwani
Ukiangalia barua inayotoka kwa OS kuja kwetu iliandikwa May 19, 2014 tukiwa na
miezi 6 tu kazini. Je inahusikaje kuwekwa hapa kama kielelezo kwamba “wakubwa”
wanatutetea kuongezewa muda wa kufanya kazi kinyume cha sharia?” Anahoji
Mambo yanayosemwa na kuandikwa yanatakiwa yakosoe utendaji
kazi wa Maxmalipo na sio kuingilia mkataba wake na mteja wake kwa kuhoji ninani
amewapa kazi na wamefikaje hapo. “Wahusika (TRA) wanaweza kujibu baadhi ya
maswali yanayoulizwa kwani wanafahamu utekelezaji wetu. Ninaomba jamii IPUUZE
UWONGO HUU WENYE LENGO LA KUTUKATISHA TAMAA katika juhudi za kuwabana wakwepa
kodi na kukusanya kodi” amasema Ndgu Rajabu.
Maxcom imesaidia sana TRA kugundua wamiliki wa Kadi bandia
za kumiliki magari ambao walikuwa wakizitumia katika malipo bandia kwa kukwepa kodi.
Vilevile Maxcom ndio waliobuni mfumo wa kutoza faini za papokwahapo
kwa kutumia mashine maalum barabarani. Mifumo ambayo imelisaidia sana jeshi la
polisi kuongeza mapato yake ambayo wanayaona. Vilevile mfumo huu unawaondoa watumiaji
wa leseni bandia za Udereva waliokuwa wanaikosesha serekali mapato.
Mafanikio mengine ni kuwezesha ukusanyaji wa mapato na
ulipaji wa kodi kupiti a mabasi yaendeyo kasi (UDART), vivuko mbalimbali nchini
kama Magogoni na Busisi Mkoani Mwanza mabako mapato yameongezeka kwa kiasi kikubwa,
na tumerahisisha manunuzi ya umeme (LUKU) maji na huduma nyingine nyingi
kwakutumia simu ya mkononi au Mawakala wa Maxmalipo nchi nzima.
Hata hivyo amepongeza jitihada za Rais wa jamhuri ya
muungano ya Tanzania Dr. Magufuli za kukusanya kodi na jinsi anavyoamini kwamba
nchi hii haitakiwi kuwa tegemezi bali inatakiwa kuwa nchi ya kutoa misaada.
Amefafanua kwamba Maxcom Africa ltd inauwezo wa kuhakikisha
kwamba mapato yanakusaywa moja kwa moja kwenda TRA bila TRA kuendelea kusubiri
wakusanyaji wapeleke mapato TRA, kwani mara nyingine yanacheleweshwa kufika
serekalini kwa sababu za kibinadamu. Amesema inawezekana kwamba mapato
yanayotakiwa kulipwa serekalini yanalipwa mojakwamoja kutoka kwa Mnunuzi yanafika TRA kwa wakati kwa njia ya
mtandao popote nchini.
Hivyo amemuomba Mheshimiwa Rais azidi kuwapa Fursa zaidi
wazawa washirikiane na Serekali ili kukusanya mapato ya ndani kwa lengo la
kufika kule tunapotarajia.
Kampuni ya maxcom Africa Ltd kwa sasa imetoa ajira rasmi
zaidi ya mia tano (500) na ajira zisizo rasmi zaidi ya elfu ishirini (20,000)
kote nchini, zikiwa ni ajira kwa wakala, wafanyakazi katika vituo mbalimbali
vya usafiri na usafirishaji kama ferry, DART na sehemu mbalimbali za malipo.
Hivi sasa maxcom Afica ltd inafanya kazi katika nchi
nyingine kama Uganda, na Rwanda (MaxPay)