Mkoa wa Arusha
Mkoa wa Arusha | |
Mlima Ol Doinyo Lengai karibu na kijiji cha Ngare Sero, Mkoa wa Arusha. |
|
Mahali pa Mkoa wa Arusha katika Tanzania |
|
Anwani ya kijiografia: 3°0′S 36°0′E | |
6
|
|
- Mkuu wa Mkoa
|
Isidori Shirima
|
- Mkoa
|
86,100 km²
|
- Maji
|
2,460 km²
|
Idadi ya wakazi (2002)
|
|
-
|
1,288,088
|
Tovuti: http://www.arusha.go.tz/ |
Wilaya zake ni Monduli, Longido, Meru, Arusha Vijijini, Arusha Mjini,Ngorongoro na Karatu. Makao makuu yapo Arusha mjini.
Eneo lake ni km za mraba 86,100 zikiwemo km² 2,460 za maji. Kati ya milima yake Oldoinyo Lengai (2,878 m) bado ni volkeno
hai, na mlima Meru ni volkeno ya kulala tangu mw. 1910. Mvua hunyesha
kati ya millimita 1,800 mm kwa mwaka mlimani Arusha hadi 508 mm kwa
mwaka katika maeneo makavu.
Mkoa wa Arusha ndio kitovu cha utalii Tanzania Bara. Barabara ya lami Dar Es Salaam-Nairobi inavuka eneo lake. Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kilimanjaro wahudumia miji ya Arusha na Moshi. Kuna mbuga za taifa na hifadhi za wanyamapori Ngorongoro, Serengeti, Olduvai, Arusha, Tarangire na Ziwa Manyara. Hifadhi ya Mlima Kilimajaro iko karibu.
Arusha hulimwa kahawa, nafaka, pareto, katani, pamba, alizeti.
Fosfati inachimbuliwa Minjingu Mkoani Arusha, na takribani tani 48,000
kwa mwaka hutumiwa katika uzalishaji wa mbolea.
Majimbo ya Bunge
Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:
- Arumeru Magharibi : mbunge ni Gibson Ole Mesiyeki (Chadema)
- Arumeru Mashariki : mbunge ni Joshua Nassari (Chadema)
- Arusha Mjini :mbunge ni Godbless Lema (Chadema)
- Karatu : mbunge ni Wille Qulwi Qambalo (Chadema)
- Longido : mbunge ni Onesmo Ole Nangole (Chadema)
- Monduli : mbunge ni Kalanga Julius Laizer (Chadema)
- Ngorongoro : mbunge ni William Tate ole Nasha (CCM)
No comments:
Post a Comment