MKUU WA WILAYA YA GAIRO MHE. SIRIEL SHAIDI MCHEMBE TAREHE 22/8/2017 AMEFANYA ZIARA YA KUKAGUA BAADHI YA WANUFAIKA WA PESA ZA TASAF
Kupitia pesa za TASAF, wamefanya yafuatayo:-
Wameweza kutoka kwenye nyumba za tembe (full suite) na kujenga nyumba zilizoezekwa na mabati.
Wameweza kujenga vyoo hivyo kuacha kujisaidia porini.
Wameweza kufuga mifugo na mifugo inazaliana.
Kuna wanawake waliokuwa na vigenge vya mbogamboga na sasa wameweza kuanzisha viduka vya wastani.
Wameweza kulima hata kama ni kwa kukodisha nusu eka na hivyo kupata mazao kama mtama, mahindi na alizeti.Wameweza kununulia watoto nguo za shule na madaftari.
Asilimia 80 ya Kaya masikini zaidi ya 1,000/- alizotembelea Mkuu wa Wilaya wamekata Bima ya Afya ya Jamii (Community Health Fund). Hivyo basi badala ya kuuza kuku au mbuzi anapougua sasa wanatibiwa moja kwa moja. Pia wamama wajawazito na watoto wanapata huduma bila shida.
No comments:
Post a Comment