focusmedia Search This Blog

Thursday, August 10, 2017

JUNE 1,2017 RAIS JOHN MAGUFULI ALIFANYA UZINDUZI WA MFUMO WA KIELEKTRONIKI WA UKUSANYAJI KODI,UTEKELEZAJI WA AGIZO LA KUJIUNGA NA MFUMO HUO LIKOJE BAADA YA MIEZI MIWILI


#Nayaomba Makampuni binafsi kujiunga kwa hiari na mfumo huo wa kielektroniki wa ulipaji kodi -Rais Dkt.Magufuli.

#Wizara zote ni lazima zijiunge na mfumo mpya wa kielektroniki wa ulipaji kodi - Rais Dkt.Magufuli.

#Serikali ya Tanzania ninayoiongoza inataka kufanya kazi na Serikali zilizo makini- Rais Dkt.Magufuli.

#Rais Dkt.Magufuli amezitaka Wizara na Taasisi mbali mbali za Serikali zisiendelee kujenga vituo vya kutunzia taarifa na badala yake taarifa zao ziingizwe katika vituo vilivyopo.

#Rais Dkt. Magufuli amezitaka Kampuni za simu kuwa wa kwanza kuingia katika mfumo mpya wa kielektroniki wa ulipaji kodi. JUNE 1 2017




 NUKUU MUHIMU SIKU YA UZINDUZI WA MFUMO HUO JUNE 1 2017

#Mfumo wa kielektroniki wa ukusanyaji kodi unalenga kupata taarifa sahihi za watoa huduma na walipa kodi-Kamishna Mkuu TRA,Charles Kichere .

#Mfumo  hautasababisha ongezeko lolote la kodi kwa watoa huduma na walipa kodi-Kamishna Mkuu TRA, Charles Kichere.

#Utekelezaji wa mfumo wa kielekroniki wa ukusanyaji kodi utafanyika kielektroniki bila kuhusisha mtu yeyote - Kamishna Mkuu TRA,Charles Kichere.

#Mfumo wa kielektroniki wa ukusanyaji kodi utahakikisha unakusanya mapato ya Serikali kwa mujibu wa sheria-Kamishna Mkuu TRA,Charles Kichere.

#Mfumo wa kielektroniki  wa ukusanyaji kodi umetengenezwa na jopo la wataalam wa kitanzania -Kamishna Mkuu TRA,Charles Kichere.

#Jopo la wataalamu wa kitanzania waliotengeneza mfumo huo wamefanya bila kulipwa chochote -Kamishna Mkuu TRA,Charles Kichere.

#Mfumo mpya wa kielektroniki wa ulipaji kodi utasaidia kupunguza mianya ya kuvujisha mapato yanayopotea kwa njia ya mitandao- Prof.Mpango.

#Mfumo mpya wa kielektroniki wa ukusanyaji kodi utaondoa tatizo la kutoaminiana katika ukokotoaji na ulipaji wa kodi - Prof.Mpango.

#Serikali zilizo makini haziwezi kuendelea bila kukusanya mapato- Rais wa Zanzibar, Dkt. Shein.

#Wananchi tujitahidi kulipa kodi ili tuweze kujenga uchumi wa nchi -Rais wa Zanzibar,Dkt. Shein.

#Nimeridhika na ujenzi wa kituo kipya cha elektroniki cha ulipaji kodi -Rais Dkt.Magufuli.

#Serikali iliamua kujenga kituo kipya cha elektroniki cha ulipaji kodi ili kulinda usalama wa Taifa,Taasisi na Sekta Binafsi-Rais Dkt.Magufuli.

#Mfumo mpya wa ulipaji kodi kwa njia ya kielektroniki utalinda taarifa za mteja hata kama kutatokea uharibifu wowote -Rais Dkt.Magufuli.

#Rais Dkt.Magufuli,Makamu wa Rais,Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar Dkt.Shein walikabidhiwa ipad kwa ajili ya kuangalia mapato na kodi zote zinazokusanywa kupitia mfumo mpya wa kielektroniki wa ukusanyaji kodi.




























                  BADO UITIKIO WA UTEKELEZAJI WA AGIZO LA RAIS NIWA KUSUA SUA.

No comments:

Post a Comment