Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo March 18,2017 amehudhuria mkutano wa dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya maendeleo ya kusini mwa Afrika SADC akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, mkutano huo umefunguliwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mfalme Mswati wa III wa Swaziland mjini Mbabane Swaziland ambapo amezitaka Nchi wanachama wa SADC kuimarisha ushirikiano katika utekelezaji wa maendeleo ya Jumuiya hiyo kama hatua ya kuwakwamua wananchi na umasikini.
focusmedia Search This Blog
Saturday, March 18, 2017
Wednesday, March 8, 2017
WILL SMITH NA FAMILIA YAKE WAMEITENDEA HAKI TANZANIA
Tanzania
ni urithi wa ulimwengu kimazingira. Hifadhi za Taifa Kumi na sita zenye uasili
wa kimazingira tangu karne na karne Zinawaleta watu maarufu Duniani. Kuna mengi zaidi ya kusema kuhusu
uzuri wa Tanzania kuliko eneo lolote ulimwenguni. Kuna maeneo machache sana Duniani
ambayo yanatoa taswila bora ya ikolojia kwa zaidi ya matarajio yako eneo
hili ni Tanzania,hapa ndio utaona wazi Jamii ya Paka wakubwa ulimwenguni,utaona
uhamiaji wa wanyama wakisafiri kila msimu wa maisha yao,Utaona sakafu ya
Ngorongoro kama urithi wa Kihistoria wa maisha ya viumbe wote sehemu moja, maelfu ya
flamingo,Sokwe wa Mahale au fukwe Mwanana za maziwa na Bahari ya Hindi ziiubeba ukanda wa pwani,
maziwa ya Victoria, Tanganyika na Nyasa,Will Smith anaamini yeyote ajae
Tanzania atabaki na alama ya kumbukumbu ya urithi wa ulimwengu wa
mazingira na viumbe wake,eneo lenye maumbile ya amani na utulivu kila
kona,Utafika kileleni mwa Afrika Kilimanjaro,visiwa mwanana vya Zanzibar,eneo
lenyeshamba kubwa la mauwa kiasili linaitwa bustani ya mungu Kitulo, Hii ni
Tanzania
![]() |
| Fresh Prince a.k.a will smith baba yake Jada smith na Willo smith na wengine wakiwa katika Moja ya mbuga zetu Tanzania |
![]() |
| Rubani Abed na mzee wa Men In Black Will Smith |
![]() |
| Mwanamitindo maarufu wa marekani aitwaye #chaneliman ameitembelea serengeti . |
![]() |
| Mwanamitindo maarufu wa marekani aitwaye #chaneliman picha ya pamoja na Will Smith wakiwa Serengeti . |
![]() |
| Mwanamitindo maarufu wa marekani aitwaye #chaneliman |
Sunday, March 5, 2017
RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI ATEMBELEA KIWANDA CHA SARUJI CHA DANGOTE PIA AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA KUSAMBAZA UMEME KATIKA MIKOA YA MTWARA NA LINDI MARCH 5,2017
![]() |
| Rais Dkt. Magufuli akiwa na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote wakipeperusha bendera kuashiria uzinduzi rasmi wa Magari 580. |
![]() |
| Rais Dkt. Magufuli akizungumza jambo na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote. |
![]() |
| Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote akimuonesha Rais Dkt. Magufuli sehemu ya Kiwanda hicho pamoja na vifaa vyake mkoani Mtwara. |
![]() |
| Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika viwanja hivyo vya kiwanda cha Dangote kabla kuzindua magari 580 ya kiwanda hicho yatakayosafirisha saruji nchini. |
Sunday, February 19, 2017
WAZIRI MKUU AKERWA MBOLEA YA MINJINGU KUPEWA LEBO YA KENYA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema haridhiki na hali aliyoikuta kwenye kiwanda cha kutengeneza mbolea cha Minjingu baada ya kubaini kuwa wanatumia mifuko yenye lebo ya Kenya wakati mbolea hiyo inazalishwa hapa nchini.
Kutokana na hilo, Waziri Mkuu amewataka wamiliki wa kiwanda hicho waandike barua kwa Mheshimiwa Rais Dk. John Pombe Magufuli kabla hajamaliza ziara yake Jumatano, Februari 22, 2017 apate nakala ya barua hiyo.
Ametoa agizo hilo (Jumapili, Februari 19, 2017) baada ya kutembelea kiwanda hicho kilichopo wilaya Babati akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake mkoani Manyara. Waziri Mkuu amerejea Babati leo akitokea Dar es Salaam ambako alikuwa na ratiba za kitaifa.
“Nilikuja kukagua kiwanda baada ya kupokea malalamiko kuwa mbolea hii haikubaliki huko vijijini. Watafiti wameonyesha kuwa ikitumika inasaidia kutoa mazao mengi. Lakini wakati niko kiwandani nimekerwa kukuta mifuko ya kupakia mbolea hii ina anuani ya Nairobi, Kenya wakati mali ghafi inatoka Tanzania,” amesema.
“Ni kwa nini mifuko hii ina anuani ya Kenya? Hapa tulipaswa tuone anuani ya Babati! Je mlipata kibali kutoka serikalini? Tena kuna lebo ya TBS. Kwa nini Tanzania haionekani? Kwani malighafi iko Kenya? Haiwezekani, ni lazima uandike barua na uombe radhi kwa Mheshimiwa Rais Magufuli. Yeye anahimiza ujenzi wa viwanda ndani ya nchi, halafu ninyi mnafanya hivyo?”
Akiwa ndani ya kiwanda hicho, Waziri Mkuu alikuta baadhi ya mifuko ya mbolea ikiwa imeandikwa: ‘County Government of Bungoma’, ina nembo ya Serikali ya Kenya, na anuani ikionesha kuwa mbolea hiyo imetengenezwa na kiwanda cha mbolea cha Minjingu lakini anuani inasomeka P. O Box 2941 – 00200 Nairobi, Kenbro Industrial Park, Mombasa Road; namba ya simu +254-20-6000-970 lakini mifuko hiyo pia ina muhuri wa TBS.
Baadhi ya mifuko ilikuwa ikipakiwa ndani ya lori tayari kwa kusafirishwa kwenda kwa wateja. Pia amesema atamwagiza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage aje hapa na wanasheria wake na wataalamu kutoka Tume ya Ushindani wa Kibiashara (FCC) ili waje kuangalia hatua gani zinapaswa kuchukuliwa. “Kwa staili hii hii tumeona watu wakinunua kahawa yetu na kwenda kuipakia upya huku wakiweka lebo za kwao. Leo hii hata Tanzanite pia inasemwa imetengenzwa India. Hatuwezi kukubali hali hii iendelee,” amesisitiza.
“Tukiruhusu hali hii, watu watajuaje kuwa mbolea hii ambayo ni first class duniani kuwa inapatikana Tanzania? Kiwanda chetu, ardhi yetu, suala la kutangaza nchi yetu kwa kutumia bidhaa zetu litafanikiwa kwa njia hii kweli?”
“Nataka wakati namaliza ziara nipate taarifa ya hili jambo pamoja na nakala ya barua ambayo imetumwa kwa Mheshimiwa Rais,” amesisitiza.
Akitoa maelezo kuhusu hali hiyo, Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Bw. Tosky Hans alimweleza Waziri Mkuu kwamba wametumia lebo hiyo kutokana na makubaliano na wanunuzi jibu ambalo Waziri Mkuu hakulikubali na kusisitiza kuwa anapaswa aombe radhi. Waziri Mkuu kesho anaendelea na ziara yake wilayani Mbulu ambako atatembelea hospitali ya Haydom, kuzungumza na watumishi wa wilaya hiyo na kuzindua shule ya sekondari Singland.
![]() |
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mgodi wa kiwanda cha mbolea cha Minjingu wakati alipotembelea kiwanda hicho mkoani Manyara, Februari 19, 2017. |
![]() |
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha mbolea cha Minjingu mkoani Manyara, Februari 19, 2017 |
![]() |
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha mbolea cha Minjingu mkoani Manyara, Februari 19, 2017
|
Saturday, February 18, 2017
TANZANIA INA WATUMIAJI WA INTANETI TAKRIBANI MILIONI 20
TCRA inatueleza kuwa hadi Disemba 2016 tulikuwa na watumiaji wa mtandao wa Intaneti takribani milioni 20.Taifa limejipanga vipi kukabiliana na Vita ya kimtandao na taarifa sahihi kwa manufaa ya kizazi kijacho?
Friday, February 17, 2017
WABUNGE NA WAWAKILISHI WAONYESHA USHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA MAENDELEO YA JAMII NCHINI TANZANIA, MATOKEO CHANYA+ IMEIBUKA NA NEEMA MGAYA MBUNGE WA VITI MAALUMU CCM
MBUNGE VITI MAALUM NEEMA MGAYA ameaazisha kampeni ya kugawa vitabu katika Shule zote za Sekondari mkoani Njombe zaidi ya 80.Hadi sasa amekwisha kugawa Vitabu vya "Kiada na Ziada”katika shule za Sekondari 37 Mkoani humo
Saturday, February 11, 2017
Monday, February 6, 2017
MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA WA KUWAWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI MJINI DUBAI
![]() |
Subscribe to:
Posts (Atom)










































