Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amehudhuria mkutano wa Jopo la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa la Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi kama mmoja wa wajumbe wa jopo hilo.
Tanzania kama nchi mwanachama ilipata fursa ya kutoa uzoefu wake jinsi Serikali imeweka mikakati mbalimbali ya kuwawezesha wanawake hususani wale walio katika sekta isiyo rasmi; hasa wakulima na wafanyabiashara wadogo wadogo wanawake ili kuhakikisha wanafaidika na mifumo ya kifedha na kijiditali kama vile kupata mikopo ya gharama nafuu; kuingizwa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii na huduma zingine.
Makamu wa Rais alisema pamoja na kila bara kuwa na changamoto zake, bado kuna umuhimu wa dunia kuhakikisha inaweka misingi madhubuti ya kuinua wanawake kiuchumi hasa kwa wanawake wa ngazi za chini ambao wengi wao wanaishii vijijini.
Alitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni pamoja na mifumo ya sheria na sera zilizopo kuwa bado zinawanyima wanawake haki ya kurithi na kumiliki ardhi hata kama haki hizo zimewekwa kisheria.
Mkutano huo ulileta washiriki takriban 45 kutoka sekta mbalimbali ikiwemo serikali, Taasisi binafsi, wachambuzi mbalimbali wa masuala ya kumwezesha mwanamke kiuchumi kutoka Jumuiya ya Kimataifa.
|
No comments:
Post a Comment