focusmedia Search This Blog
Thursday, June 8, 2017
Tuesday, June 6, 2017
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan Ziarani mkoani Mara
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia
Suluhu Hassan ameuagiza uongozi wa wilaya ya Serengeti na wa mkoa Mara
kukamilisha haraka awamu ya kwanza ya ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo ili
kuondoa adha ya wananchi kusafiri kwenda mikoa ya jirani ya Arusha na Mwanza
kwenda kupata huduma afya.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa agizo 6-June-2017 kwenye mkutano wa hadhara mjini
Mugumu wilayani Serengeti mkoani Mara mara baada ya kutembelea ujenzi wa
hospitali hiyo ya wilaya na kuweka jiwe
la msingi.
Makamu wa Rais amesema kutokana na wilaya ya Serengeti
kupata wegeni wengi kutoka nje ya nchi ambao wanaenda kutembelea Hifadhi ya
Taifa ya Serengeti hivyo ni muhimu kwa
viongozi wa wilaya na mkoa kwa ushirikiano na wadau wa maendeleo kukamilisha
ujenzi huo haraka ili wananchi waweze kupata huduma za afya za uhakika katika
wilaya yao.
Makamu wa Rais amesema kukamilika kwa ujenzi huo wa awamu ya
kwanza kutaondoa taabu kubwa wanayopata wananchi wa wilaya ya Serengeti katika
kupata huduma ya afya karibu na maeneo yao.
Katika kuunga mkono jitihada hizo za ujenzi wa hospitali ya
wilaya ya Serengeti, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ameahidi kuchangia
kiasi cha shilingi milioni Tano na amewaahidi wananchi wa wilaya ya Serengeti
kuwa atakikisha fedha kutoka Serikalini ambazo zinatakiwa kupelekwa wilayani
humo zinapelekwa haraka ili kukamilisha ujenzi huo.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan pia amewataka
wananchi kote nchini kuunga mkono jitihada za Serikali za kupambana na rushwa
na ufisadi ili kuhakikisha miradi inayotekelezwa inakuwa na manufaa kwa
wananchi wote.
Amewaomba wananchi nchini wasirudi nyuma katika mapambano
dhidi ya rushwa bali waendelee kubaini watu wanaofanya vitendo hivyo ili
Serikali iweze kuwachukulia hatua kali za kisheria .
Kuhusu tatizo la mimba mkoani Mara, Makamu wa Rais
ameonyesha kuchukizwa na vitendo hivyo na kuomba vyombo vya dola na wananchi
kwa ujumla kushirikiana katika kukomesha mimba za utotoni mkoani Mara.
Kwa upande wake, Mkuu wa mkoa wa Mara Dkt Charles Mlingwa
amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa maelekezo yote anayoyatoa katika ziara yake
yatafanyiwa kazi ipasavyo ili kuondoa kero na changamoto zinazowakabili
wananchi.
Mkuu huyo wa mkoa wa Mara ameomba wananchi wa Mkoa wa Mara
kuwepa pembeni tofauti zao za kisiasa bali washirikiane na Serikali katika
utekelezaji wa miradi yao ya maendeleo.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan bado anaendelea na
ziara yake ya kikazi mkoani Mara ambapo hapo kesho atafanya ziara katika wilaya
za Butiama na Musoma mkoani Mara.
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AMUAPISHA ANNA ELISHA MGWIRA, MKUU MPYA WA MKOA WA KILIMANJARO JUNE 6, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Anna Elisha Mgwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Ikulu jijini Dar es salaam June 6, 2017
Mkuu wa mkoa kilimanjaro Anna Elisha Mgwira akisoma hati ya kiapo cha maadili ya utumishi wa umma mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam June 6, 2017
Mkuu wa mkoa kilimanjaro Anna Elisha Mgwira akisaini hati ya kiapo cha maadili ya utumishi wa umma mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam June 6, 2017
Mkuu wa mkoa kilimanjaro Anna Elisha Mgwira akiongea jambo la shukrani mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam June 6, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea jambo mara baada ya kumuapisha Anna Elisha Mgwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Ikulu jijini Dar es salaam June 6, 2017
Baadhi ya viongozi mabilimbali waliohudhuria kwenye uapisho Mkuu wa Mkoa wa kilimanjaro Anna Elisha Mgwira alipoapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam June 6, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Anna Elisha Mgwira Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro mara baada ya kumuapisha Ikulu jijini Dar es salaam June 6, 2017
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa akimpongeza Anna Elisha Mgwira Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro mara baada ya kuapisha Ikulu jijini Dar es salaam June 6, 2017
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akimpongeza Anna Elisha Mgwira Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro mara baaya ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam June 6, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa, na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mgwira Mkuu mara baada ya kumuapisha Ikulu jijini Dar es salaam June 6, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa, na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mgwira na viongozi mbalimbali ya serikali mara baada ya kumuapisha Ikulu jijini Dar es salaam June 6, 2017
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Rodrick Mpogoro akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mgwira Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa ajili ya Mkuu wa Mkoa huyo kwenda kuitekeleza ilani hiyo katika kazi yake ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro mara baada ya kuapisha Ikulu jijini Dar es salaam June 6, 2017Monday, June 5, 2017
RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AFUNGUA KIKAO CHA MAAFISA WAANDAMIZI, MAKAMANDA WA MIKOA NA VIKOSI WA JESHI LA POLISI JIJINI DAR ES SALAAM JUNE 2, 2017
RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AFUNGUA KIKAO CHA MAAFISA WAANDAMIZI, MAKAMANDA WA MIKOA NA VIKOSI WA JESHI LA POLISI JIJINI DAR ES SALAAM JUNE 2, 201
Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Simon Sirro akitoa muhtasari wakati wa ufunguzi wa kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam Juni 2, 2017
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kufungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam Juni 2, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam Juni 2, 2017
Ukumbi wote ukimsikiliza kwa makini wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam Juni 2, 2017
Meza kuu ikimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kufungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam Juni 2, 2017
Kamishna wa Jeshi la Polisi Visiwani Zanzibar Afande Hamdan Omar makame akitoa shukurani kwa niaba ya wote kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli baada ya kufungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam Juni 2, 2017.
Kamishna wa Jeshi la Polisi Visiwani Zanzibar Afande Hamdan Omar makame akipeana mikono na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli baada ya kumshukuru kwa niaba ya wote kwa kufungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam Juni 2, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na meza kuu akipata picha ya pamoja na Makamishna wa Jeshi la Polisi baada ya kufungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam Juni 2, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na meza kuu akipata picha ya pamoja na Makamishna, makamanda wa Wakuu wa Vikosi wa Jeshi la Polisi baada ya kufungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam Juni 2, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na meza kuu akipata picha ya pamoja na Makamanda wa Vikosi vya Polisi baada ya kufungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam Juni 2, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na meza kuu akipata picha ya pamoja na Makamanda wa Vikosi vya Polisi baada ya kufungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam Juni 2, 2017RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKUTANA NA MJUMBE WA RAIS KABILA WA KONGO, MJUMBE WA RAIS NYUSI WA MSUMBIJI NA BALOZI WA KUWAIT IKULU DAR ES SALAAM JUNE 5,2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsalimu Mjumbe Maalumu wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Leonard She Okitunda alipofika Ikulu jijini Dar es salaam kuwasilisha ujumbe huo Juni 5, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea ujumbe kutoka kwa Mjumbe Maalumu wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Leonard She Okitunda alipofika Ikulu jijini Dar es salaam kuwasilisha ujumbe huo Juni 5, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mjumbe Maalumu wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Leonard She Okitunda na ujumbe wake na wa Tanzania alipofika Ikulu jijini Dar es salaam kuwasilisha ujumbe huo Juni 5, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia malori mawili Mpya ya kuzolea taka baada ya kumaliza mazungumzo na Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Ibrahim Al Najem alipofika kumtembelea na kukabidjhi msaada wa magari hayo Ikulu jijini Dar es salaam Juni 5, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimlaki Mjumbe Maalumu wa Rais wa Msumbiji na Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo Jenerali Atanasio Salvador Ntumuke alipofika Ikulu jijini Dar es salaam kuwasilisha ujumbe huo Juni 5, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mjumbe Maalumu wa Rais wa Msumbiji na Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo Jenerali Atanasio Salvador Ntumuke alipofika Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi ujumbe maalumu Juni 5, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana baada ya mazungumzo na Mjumbe Maalumu wa Rais wa Msumbiji na Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo Jenerali Atanasio Salvador Ntumuke alipofika Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi ujumbe maalumu Juni 5, 2017
Subscribe to:
Posts (Atom)





























