focusmedia Search This Blog

Monday, June 5, 2017

WANAHISA WA NMB WAPITISHA GAWIO LA SHILINGI BILIONI 52

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (kulia) akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kumalizika kwa Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa NMB wa Mwaka 2017.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (kushoto) akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa NMB kwa Mwaka 2017 ulifanyika juzi katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mmoja ya wanahisa wa Benki ya NMB akiuliza swali kwenye Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa NMB kwa Mwaka 2017 ulifanyika juzi katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

BENKI ya NMB (National Microfinance Bank Plc) imetangaza gawio la shilingi 104 kwa kila hisa. Wanahisa wa NMB walipitisha kiasi kilichokuwa kimependekezwa katika mkutano mkuu wa Mwaka uliofanyika jana jijini Dar es Salaam. Jumla ya gawio lote litakalolipwa kwa wana hisa ni shilingi Bilioni 52 kiwango ambacho kinaendana na sera ya benki ya kutoa moja ya tatu (33.3%) ya faida baada ya kodi. Benki ilipata faida ya shilingi Bilioni 153.8 kwa mwaka ulioishia disemba 31, 2016; ikiwa ni ongezeko la 2.3% kutoka shilingi Bilioni 150.3 iliyopatikana mwaka uliotangulia.

Ukitoa faida iliyopatikana, NMB iliandikisha mafanikio mbalimbali kwa mwaka 2016. Uzinduzi wa akaunti ya Pamoja ya Wajibu, kuongezeka kwa mawakala zaidi ya 1000 wa NMB Wakala na kuunganishwa kwa halmashauri zaidi ya 150 katika mfumo wa malipo kwa njia za kielektroniki viliongeza upatikanaji wa huduma za kibenki kwa watanzania wengi zaidi ambao awali hawakuwa na huduma hizo, hususani kupitia njia za kielektroniki na hivyo kuongeza hazina ya fedha kwenye benki.
Kutambuliwa kwa NMB na mashirika ya kimataifa kama Moody kuwa na Kiwango cha juu cha ufanisi yaani Stable B1 credit rating inadhihirisha imani waliyonayo wawekezaji wa kimataifa kwa NMB. Wawekezaji wa ndani pia walionyesha Imani yao kubwa kwa NMB kwa kupita Kiwango kilichowekwa na NMB katika uuzwaji wa hati fungani za benki (NMB Retail Bond).
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya NMB – Prof Joseph Semboja, alisema kuwa bodi ya wakurugenzi imeazimia kuweka ulingano kwa kuhakikisha wanahisa wanapata gawio zuri huku benki ikiendelea kuongeza uwekezaji kwenye biashara yake ili kusaidia mipango ya ukuaji wa benki.
“NMB kwa miaka mingi imekuwa ikihakikisha ina mtaji wa kutosha na tunaazimia kuendeleza kasumba hii. Kufikia malengo haya, ni muhimu kufanya maamuzi sahihi hususani tukilenga kuendana na matakwa ya mabadiriko ya kisera hasa matakwa ya mitaji.” Alisema Prof Semboja
Uwiano wa Mitaji wa mabenki nchini unategemewa kubadirika karibuni na hii ni kutokana na matakwa ya benki kuu yanayoyataka mabenki yote ya kibiashara kukubali kuendana na matakwa ya Basel II na matakwa ya kimataifa ya kimahesabu kwa hasara za mikopo za mabenki. Katika muda mfupi, hili litaleta msukumo kwa viwango vya faida ambazo mabenki nchini yatapata.

“NMB imedhamiria kuendelea kuchangia katika maendeleo ya kiuchumi, pia hivi sasa ambapo mambo mbalimbali yanabadirika. Tunapenda kuwahakikishia ukuaji wa faida utakaotuwezesha kuendeleza ukuaji wa mtaji na kuendelea kuwa benki namba moja nchini,” alisema Mkurugenzi wa NMB – Ineke Bussemaker.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (kushoto) akitoa ufafanuzi baadhi ya mambo kwa wanahisa kwenye Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa NMB kwa Mwaka 2017 ulifanyika juzi katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Kulia ni mmoja wa wajumbe wa Bodi ya NMB, Mike Laiser.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Phillip Mpango akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa NMB kwa Mwaka 2017 ulifanyika juzi katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (kulia) akizungumza jambo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Phillip Mpango kwenye Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa NMB kwa Mwaka 2017 ulifanyika juzi katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo ukiendelea.

Monday, May 29, 2017

AMIR JESHI MKUU RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AMUAPISHA KAMISHNA WA POLISI SIMON SIRRO KUWA KAMISHNA GENERALI WA JESHI LA POLISI NCHINI MEI 29,2017 IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Amir jeshi mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimvua cheo cha Kamishna wa Polisi Simon Sirro na kumvalisha cheo cha Kamishna Generali wa Jeshi la polisi nchini Mei 29,2017 Ikulu jijini Dar es salaam




Kamshina Jenerali wa Polisi nchini Simon Sirro akila kiapo cha maadili ya utumishi wa Umma mara baada ya kumuapisha  na Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  kuwa Kamshina Jenerali wa Polisi nchini Mei 29,2017 Ikulu jijini Dar es salaam

Amir jeshi mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mkuu wa Jeshi la Polisi Mteule, Kamishna wa Polisi Simon Sirro kuwa Kamishna Generali wa Jeshi la Polisi Nchini Mei 29,2017 Ikulu jijini Dar es salaam

Amir jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Kamshina Jenerali wa Polisi nchini Simon Sirro mara baada ya kumuapisha Mei 29,2017 Ikulu jijini Dar es salaam

Kamshina Jenerali wa Polisi nchini Simon Sirro  akisaini hati ya kiapo cha maadili ya utumishi wa Umma mara baada ya kuapishwa

Kamshina Jenerali wa Polisi nchini Simon Sirro  mara baada ya kupandishwa cheo

Amir jeshi mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Hassani Suluhu, Waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchema,Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Jaji Prof. Ibrahim Hamis Juma, Mkuu wa Jeshi la Polisi Mteule Simon Sirro, aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Erenest Mango, katibu Mkuu kiongozi Balozi John Kijazi, pamoja na Makamishna mbalimbali wa Wizara ya mambo ya ndani katika picha ya pamoja



Amir jeshi mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akisalimia na makamanda mbalimbali wa polisi na Jeshi la wananchi wa tanzania mara baada ya kumuapisha  Mkuu wa Jeshi la Polisi Mteule Simon Sirro Ikulu jijini Dar es salaam



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Hassan Suluhu akimpongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi Mteule, Kamishna Jenerali wa Jeshi la polisi nchini Simon Sirro mara baada ya kuapishwa Mei 29,2017 Ikulu jijini Dar es salaam

Wednesday, May 24, 2017

MUHTASARI WA KAMATI YA UCHUNGUZI WA MCHANGA WA MADINI

Muhtasari wa kamati ya uchunguzi wa mchanga wa madini kama ulivyowasilishwa na mwenyekiti wake Prof Abdulkarim Hamis Mruma  Ikulu!.



HADIDU ZA REJEA!.

1.Kamati ilikuwa na kazi ya kuchunguza aina na kiwango cha madini yaliyopo ndani ya mchanga wa madini unaosafirishwa nje!.

2.Chimbuko la utafiti huo ni kutojulikana kwa kiwango cha makinikia na mikataba yake!.

3. Hadidu za rejea zilikuwa ,Kufanya uchunguzi wa makinikia kwenye bandari ya dsm na migodini,Kufanya uchunguzi wa kimaabara ili kujua thamani na aina ya madini yaliyopo kwenye makilikia,kuchuza uwezo wa scanner zilizopo bandarini,kuchunguza uwezo wa TMAA katika kusimamia makinikia,

4.Kamati ilitembelea bandari ya Dsm,bandari kavu na kwenye migodi ya Bulyanhuru na Buswagi,yapo makontena ambayo kamati ilichukua sampuli ya juu na chini,sampuli nyingine ilikuwa zigzaga!.

5.Kamati ilichunguza uwezo wa scanner kupima makinikia!.

6.Kamati ilikokotoa thamani ya madini yaliyopatikana kwenye makinikia!.

MATOKEO YA UCHUNGUZI

1.Kamati imebaini uwepo wa dhahabu kiasi Kikubwa cha dhahabu kwenye makinikia,katika makontena 277 yaliyozuiliwa kulikuwa na tani saba za dhahabu!.
2.Makontena 277 yaliyozuliwa yalikuwa na dhahabu yenye thamani zaidi ya shilingi Trilioni moja nukta moja nne saba!.

3.Kamati ilibaini uwepo wa madini ya shaba,Silver,surpher,chuma.

4.Copper pekee ilikuwa ya thamani ya shilingi Bilioni 23.3,hapa kulikuwa na tofauti kubwa na ripotibya serikali ambayo ilionesha kuwa na thamaninya Bilioni 13.

4.Upande wa silver kamati ilibaini uwepo wa silver ya thamani ya bilioni 2.1.tofauti na ripoti ya Serikali ilionesha thamani ya Bilioni 1.

5.Upande wa surpher kamati ilibaini uwepo wa surpher ya thamani ya shilingi bilioni 1.9,kamati ilibaini madini madini haya hayapo katika mrabaha

6.Kamati ilibaini uwepo wa madini ya chuma yenye thamani ya shilingi Bilioni 2.3,

7.Kamati ilibaini uwepo wa madini mkakati ambayo kwa sasa yanahitajika sana duniani yenye thamani kati ya bilioni 129.5 mpaka  bilioni 261.5

Thamani ya madini yote katika makinikia kwenye makontena 277 yaliyochunguzwa kamati imebaini yana thamani ya triloni 1.339,ambazo serikali haipati hasa senti moja na hayapo kwenye mrabaha!.

8.Kamati imegundua uwepo wa madini mengine mengii ambayo hayarekodiwi kwenye nyaraka za serikali!.

9.Kamati imebaini wakala wa madini Tanzania hawafungi utepe kwenye makontena kuonesha viwango vya madini,kamati imebaini ufungwaji huu kufanyika wakati wa kusafirisha makontena.

10.Kamati imebaini scanner za bandarini kutokuwa na uwepo wa kubaini utotoshwaji wa mali!.

MAPENDEKEZO YA KAMATI

1.Serikali isitishe usafirishaji wa mchanga nje ya nchi

2.Serikali ihakikishe mitambo ya kusafisha makinikia unafanyika nchini

3.TMAA ifunge utepe mara baada ya mchanga kupakiwa kwenye makontena!.

4.TMAA ipime metal zote kwenye makininia

5.TMAA ipime viwango vyote vya makinikia na madini kwenye mbar bila kujali ripoti ya msafirishaji hii itasaidia Serikali kupata mrabaha!.

6.Serikali iwachukulie hatua watendaji wa TMAA na wizara husika.

7.Serikali iweke mfumo kushtukiza kwenye udhibiti wa madini!.

8.Serikali itumie wataalam wa mionzi kwenye scanner za bandarini!.



Thursday, May 11, 2017

MVUA NCHINI TANZANIA ZALETA MAAFA,MAPOROMOKO YAFUNGA BARABARA

Maporomoko ya mawe Lushoto eneo la Vuga






RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AMPOKEA RAIS WA JAMHURI YA AFRIKA KUSINI MHE. JACOB ZUMA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM MEI 11,2017



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli     na Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Jacob Zuma wakiwa wamesimama huku Nyimbo za Mataifa mawili zikiimbwa Ikulu jijini Dar es salaam mei 11,2017

Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Jacob Zuma akikagua gwaride lililoandaliwa kwa heshima yake na kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es salaam mei 11,2017



Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Jacob Zuma akiteta jambo na mwenyeji wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es salaam mei 11,2017


Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Jacob Zuma zawadi mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es salaam mei 11,2017

PICHA NA IKULU

Wednesday, April 26, 2017

Miaka 53 ya Muungano; Tuulinde na Kuuimarisha, Tupige Vita Dawa za Kulevya na Kufanya Kazi kwa Bidii








Miaka 53 ya Muungano; Tuulinde na Kuuimarisha, Tupige Vita Dawa za Kulevya na Kufanya Kazi kwa Bidii,”

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliundwa mnamo tarehe 26 Aprili, 1964 kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (inayojumuisha Visiwa vya Pemba na Unguja). Tanganyika ilikuwa ni mwendelezo wakoloni la Ujerumani, utawala wa Waingereza kwa Mamlaka ya Umoja wa Mataifa, Himaya ya Umoja wa Mataifa chini ya utawala wa Uingereza na mwisho Taifa huru kuanzia mwaka 1961 ndani ya nchi za Jumuiya ya Madola.
Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ziliingia mkataba wa Muungano mnamo mwaka 1964 na kuanzishwa Dola ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mkataba huu wa Muungano ulitiwa saini na aliyekuwa Rais wa Tanganyika, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume tarehe 22 Aprili 1964 huko Zanzibar. Mkataba huo ulithibitishwa na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi hapo tarehe 26 Aprili, 1964 na mnamo tarehe 27 Aprili, 1964, viongozi wa nchi zote mbili walikutana katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam na kubadilishana Hati za Muungano. Sheria za Muungano zilitoa tamko la Jamhuri ya Muungano katika Ibara ya 4 kwamba:
“Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zitalazimika, baada ya kuungana na siku zote baada ya kuungana, kuunganishwa kuwa Dola ya Jamhuri kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar’ (Ibara ya 4 Sheria za Muungano)”
Jina hili la “Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar” lilibadilishwa baadae mnamo tarehe 28 Oktoba, 1964 na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia Sheria ya Jamhuri ya Muungano, Sheria namba 61 ya mwaka 1964.
Kauri Mbiu ya sherehe za kutimiza miaka 53 ya Muungano huu wa Tanganyika na zanzibar ni Watanzania Tuulinde na kuuimarisha,Tupige vita dawa za Kulevya na kufanya kazi kwa Bidii
TUKIUTAFAKARI MUUNGANO WETU TUWAENZI WAASISI WETU KWA JUHUDI NA MISIMAMO DHIDI YA MASHIRIKA YETU YA UMMA TUAANZA NA TTCL TUNARUDI NYUMBANI KUUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS MAGUFULI KUFUFUA MASHIRIKA YA UMMA.