Mkurugenzi Mtendaji wa wakala wa usajili wa matukio kijamii Dkt. Hussein Khamis Shaban,amesema kuwa wameamua kuboresha vitambulisho na mfumo mzima wa uhifadhi taarifa zote za kijamii.
“Tunaboresha mfumo wa uhifadhi wa taarifa za ndoa,talaka,vifo,vizazi na utambulisho ili kuziweka katika mfumo wa kieletroniki ambao utasaidia kuboresha huduma za kijamii”.amesema Dkt. Shabani
Mfumo huh mpya utasaidia katika kutoa huduma kwa haraka Kwani taarifa zitakazoifadhiwa katika mfumo huo zitatumika na mamlaka nyingine kama Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA),Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZRB), Idara ya Uhamiaji,National Internet Data Center(NIDC), Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Msajili wa Makampuni, mfumo wa hosptali (e-health) na mfumo wa utalii.
Aidha Tayari kila wilaya kumejengwa kituo cha kidigitali ambapo vituo vyote katika wilaya 11 Unguja na Pemba vinaunganishwa na mkongo wa Taifa na Wananchi watajisajili huko huko wilayani na kuboresha Taarifa zao, kwa sasa utaratibu wa kuchakata data za kale tangu Daftari la mwanzo la mwaka 1909 zina hitahifadhiwa Kidigitali katka kanzi data ya Taifa.
Baadhi ya Vituo vya Usajili vinavyokamilishwa kila kila wilaya ya Unguja na Pemba |
Baadhi ya Vifaa vilivyoko ndani ya vituo vipya |
Baadhi ya Vifaa vilivyoko ndani ya vituo vipya |
Mambo Msiige jengo la mwanzo lililotunza kumbukumbu za Wazanzibar za maswala ya matukio ya kijamii |
Jengo jipya ambapo Ofisi kuu ya Wakala wa usajili wa matukio ya Kijamii Zanzibar |
Mambo Msiige jengo la mwanzo lililotunza kumbukumbu za Wazanzibar za maswala ya matukio ya kijamii |
Zaharan Nassor Mhifadhi Mkuu wa Nyaraka wa wakala wa usajili wa matukio ya kijamii Zanzibar akionyesha Nyaraka Kongwe zaidi yenye majina ya Uzazi kuanzia mwaka 1909 hadi 1911 |
Mhifadhi akichambua Taarifa katika Ghala la Nyaraka Ofisi kuu ya Mamlaka ya Usajili matukio ya kijamii Zanzibar |
Dr Hussein Khamis Shaaban, Mkurugenzi mtendandaji wa wakala wa usajili wa matukio ya kijamii akikagua Nyaraka za Kale za vizazi na vifo ambazo zinachakatwa kuwekwa katika mfumo wa Kidigitali |
Nyaraka zenye kumbu kumbu za wazanzibari za Uzazi,Vifo,Talaka,Ndoa na na utambulisho tangu 1909 |
Bi Mwanajuma Mwinyi Mohamedy Msajili wa vizazi na vifo Wilaya ya Kati Mkoa wa kusini Unguja akichambua Taarifa za mwananchi ili kujaza vyeti mbali mbali vya Wazanzibar |
Dr Hussein Khamis Shaaban, Mkurugenzi mtendandaji wa wakala wa usajili wa matukio ya kijamii akikagua Nyaraka za Kale za vizazi na vifo ambazo zinachakatwa kuwekwa katika mfumo wa Kidigitali |
Zanzibar sasa Kisasa Zaidi Mifumo yote na taarifa zote zinahifadhiwa kisasa na teknolojia Mpya |
Msajili wa vizazi na vifo Wilaya ya Kati Mkoa wa kusini Unguja akichambua Taarifa za mwananchi kisasa zaidi ili kujaza vyeti mbali mbali vya Wazanzibar |
Msajili wa vizazi na vifo Wilaya ya Kati Mkoa wa kusini Unguja akichambua Taarifa za mwananchi ili kujaza vyeti mbali mbali vya Wazanzibar |
Sehemu ya Mabuku ya kale yenye kumbu kumbu za Vizazi,Vifo,Talaka,Ndoa na Utambulisho ambapo zitahifadhiwa katika kanzi data ya Wakala wa Usajili wa matukio ya kijamii Zanzibar |
Jamani tunaomba iwekwe baada wiki mtu apate kitambulisho chake Mana inafika miaka mitatu mpaka mitano hujapata kitambulisho ukifatilia u apewa reason hazieleweki ati barua hatuioni jamani tunapoteza muda kufatilia alafu mnatuumiza
ReplyDelete