SEWA – “Self Employed Women
Association” ni Jumuiya ya Wanawake Waliojiajiri ambayo miongoni mwa viongozi
wake wakuu ni Bi. Renana Jhabvala (Chair Women in Informal Employment WIEGO).
Aidha, Bi Renana na Mhe. Samia
Suluhu Hassan, Makamu wa Rais JMT ni miongoni mwa viongozi wakuu wa Jopo la Juu Duniani katika Kuwezesha Wanawake
Kiuchumi chini ya Umoja wa Mataifa.
Ushirikiano wa viongozi hawa
unandelea kuleta mafanikio makubwa kwa Wanawake hasa wa ngazi ya chini hapa Tanzania.
Baada ya ujumbe huo kutua
Tanzania tangu tarehe 21 – 26 Machi, 2017, wanawake wa Zanzibar na Tanzania
Bara wamepata mafunzo mbalimbali kupitia vikundi vyao vya ujasiriamali. Taasisi
zilizoshiriki ni TEWO SACCOS, JUWABIKA, UWAKE, BACCA, BAMITA na MKUDUWODEA.
Mhe. Makamu wa Rais baada ya
kukutana na ujumbe huo tarehe 27/3/2017 ukioongozwa na “Deputy High
Commissioner” India Bw. Robert Shetkintong, akiongozana na Shree Kumar anayemuwakilisha
Renana Jhabvala, Pushpa Rathod , Sophia Kinega kiongozi wa wanawake
waliojiajiri na Mhe. Siriel Mchembe
msaidizi wa Mama Samia kwenye jopo la juu la dunia katika kuwezesha wanawake
kiuchumi amekubali kuanzisha Jumuiya hiyo hapa Tanzania.
Mchakato wa kuanzisha Jumuiya
ya wanawake waliojiajiri India na
Tanzania (SEWA) unaanza mara moja chini ya ulezi wake. Wanawake waliojiajiri Tanzania hongereni kwa kupata sauti Duniani.
Mh Makamu wa Rais akipokea taarifa ya ziara kutoka kwa Shree Kumar anayemuwakilisha Renana Jhabvala pamoja na Pushpa Rathod - SEWA |
Makamu wa Rais baada ya kuvishwa alama ya heshima kwa mila za Kihindi kutoka kwa Pushpa Rathod |
No comments:
Post a Comment