focusmedia Search This Blog

Tuesday, March 1, 2016

UJENZI BOMBA LA MAJI KUTOKA RUVU CHINI MPAKA DAR


 
mkandarasi ya kulaza bomba hilo
inaridhisha licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali zinazochelewesha
kazi hiyo zikiwemo za ufinyu wa eneo linapojengwa bomba hilo kuwezesha
mitambo kufanya kazi vizuri katika eneo la mbezi Beach, mvua
zinazoendelea kunyesha ,changamoto ya makazi ya watu kuwa ndani ya mradi
ambapo kulikuwa na kesi 17 Mahakamani zikihusisha madai mbalimbali ya
wananchi katika maeneo hayo. 

“Ni kweli zipo changamoto
zilizosababisha mradi kukawia kumalizika zikiwemo za wananchi kufungua
kesi 17  Mahakama ya Ardhi, hadi sasa DAWASA tumeshinda kesi 14  ndiyo
maana tumepata haki ya kutumia njia hii kukamilisha upanuzi wa mradi”
Amesema Mwang’ingo.



Ameongeza kuwa lengo la mradi huu
nikuongeza uzalishaji wa maji na kuboresha huduma kwa wakazi wa maeneo
ya uwekezaji (EPZ) Bagamoyo, Chasimba, Buma, Zinga, Kerege na Mpiji mkoa
wa Pwani.





Maeneo mengine yatakayonufaika na mradi
huo kwa Mkoa wa Dar es Salaam ni Bunju, Wazo, Salasala, Madale na
Kinzudi Mbezi Juu, Goba, Kawe, Makongo, Mwenge, Msasani, Mikocheni,
Mlalakua, Masaki, Sinza, Kijitonyama, Manzese, Konondoni, Magomeni,
Kigogo na Vingunguti.



Kwa upande wake Meneja Mradi wa Kampuni
inajenga bomba hilo nchini Muhandisi Eric Omuruli akizungumzia mradi huo
amesema kuwa yeye kama Meneja mradi atahakikisha anashughulikia
changamoto zilizopo ili kukamilisha kwa wakati.

No comments:

Post a Comment