focusmedia Search This Blog

Wednesday, July 3, 2019

RAIS KENYATTA AMTUMIA UJUMBE RAIS DKT. MAGUFULI


 
PMO_4211
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Kenya nchini, Dany Kazungu, ofisini kwa Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar es salaam, Julai 2, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_4222

PMO_4223
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Kenya nchini, Mhe. Dany Kazungu, ofisini kwa Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam, Julai 2, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_4232%2B2

PMO_4242
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea ujumbe maalum wa Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya  kwa naiba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kutoka kwa Balozi wa Kenya nchini, Mhe. Dany Kazungu, ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Julai 2, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NAIBU WAZIRI MHE.KANYASU ATOA NAFASI KWA WADAU WA UTALII WA UTALII NCHINI

1m
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akimkabidhi cheti Mratibu wa safari ya Utalii wa ndani, Dayna Saimoni ikiwa ni ishara ya shukrani kwa kuunga mkono jitihada za Wizara ya Maliasili na Utalii katika kuchochea na kuinua idadi ya watalii wa ndani katika Msitu Asilia wa Magoroto katika wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
2m
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akimkabidhi cheti Mratibu wa safari ya Utalii wa ndani, Esta Satta ikiwa ni ishara ya shukrani kwa kuunga mkono jitihada za Wizara ya Maliasili na Utalii katika kuchochea na kuinua idadi ya watalii wa ndani katika Msitu Asilia wa Magoroto katika wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
3m
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Nhe, Constantine Kanyasu akizungumza na watalii wa ndani walitembelea Msitu asilia wa Magoroto ambao ni kivutio kikubwa cha Utalii wakati walipokusanyika usiku kufurahia ngoma za kabila la wadigo.
4
 Kundi la watalii wa ndani kutoka jijini Dar es Salaam walioungana kwa pamoja na kwenda kutembelea msitu Asilia wa Magoroto katika wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
5
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akiwa kwenye picha ya pamoja na watalii wa nje mara baada ya kuwasili katika msitu Asilia wa Magoroto katika wilaya ya Handeni mkoani Tanga
6
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akiwa kwenye picha ya pamoja na watalii wa ndani mara baada ya chakula cha jioni katika msitu Asilia wa Magoroto katika wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
7
Baadhi ya watalii wa ndani na wa nje nyakati za usiku wakifurahia ngoma ya kabila wasambaa iliyokuwa ikitumbuizwa kwa watalii hao. (Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii)

BILIONI 114.1 KUWAPA NEEMA YA MAJISAFI WAKAZI WA DAR NA PWANI


 Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya utiaji saini wa DAWASA na wakandarasi juu ya ujenzi na uendeshaji wa miradi sita mikubwa ya usambazaji wa maji yenye thamani ya Bilion 114.5 iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/Michuzi TV. 
Wageni waalikwa na wafanyakazi wa DAWASA wakifuatilia hotuba ya Mhe. Waziri Prof Mbarawa. 
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akiwasilisha taarifa fupi ya miradi sita mikubwa yenye thamani ya Bilion 114.5 kwa Waziri wa Maji Prof Makame Mbarawa wakati wa halfa iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Miradi hiyo itahudumia maeneo ambayo hayana kabisa mtandao wa DAWASA pamoja na Mkoa wa Pwani. 
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja (kulia) akibadilishana mkataba wa utekelezaji wa miradi ya majisafi toka kwa wawakilishi wa makampuni ya ukandarasi ya Watanzania na Wachina yatakayotekeleza ujenzi wa miradi itakayojengwa Dar es Salaam na Pwani. Wengine wanaoshuhudia ni Mawaziri, Naibu Waziri, Mwakilishi wa benki ya Dunia na viongozi wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/Michuzi TV. 
Wageni waalikwa na wafanyakazi wa DAWASA waliohudhuria hafla hiyo.  
Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jaffo akitoa machache. Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akifafanua jambo.  
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akielezea furaha yake juu ya DAWASA kupeleka wa maji katika jimbo lake la Mkuranga na vitongoji vyake kupitia miradi hiyo.  
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi DAWASA Jenarali Mstaafu Davis Mwamunyange akielezea chagamoto zinazoikabili mamlaka hiyo. 

Wageni waalikwa na wafanyakazi wa DAWASA waliohudhuria hafla hiyo. 
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Assumpta Mshama ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kibaha akitoa salamu. 
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sophia Mjema ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Ilala akitoa salamu. 
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Kate Kamba akielezea furaha yake jinsi DAWASA inavyotekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi kumtua mama ndoo kichwani.  
Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jaffo (kushoto) akiteta jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja (kulia). 

WIZARA YA VIWANDA YAJIPANGA KUKUZA MASOKO NDANI NA NJE YA NCHI


TANTRADE wapongezwa kwa kuyatendea haki maonesho hayo kila mwaka

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
 
Maonesho ya 43 ya biashara maarufu kama sabasaba yenye  kauli mbiu ya usindikaji wa mazao ya kilimo kwa maendeleo ya viwanda yamezinduliwa rasmi leo jijini Dar es Salaam huku masuala ya utafutaji wa masoko pamoja na kuelimimisha wafanyabiashara kuhusiana na kliniki ya biashara yakitiliwa mkazo.

Akizungumza katika ufunguzi huo makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa maonesho hayo ni kwa kutoa kipaumbele kwa bidhaa zinazozalishwa nchini Kama Rais anavyosisitiza.

Suluhu amesema kuwa maonesho ya sabasaba ni makubwa katika ukanda wa Afrika na katika maonesho hayo zaidi ya nchi 35 zimeshiriki katika hali inayoashiria ubora na utulivu unaovutia uwekezaji katika nchi yetu.

Amesema kuwa serikali itaviwezesha viwanda vidogo na Kati katika masoko pamoja na kuendelea kushiriki katika maonesho hayo ili waweze kutangaza bidhaa zao zaidi.

Pia amesema kuwa kukua kwa uchumi kwa asilimia 7 kunachagizwa na maendeleo ya viwanda na kasi zaidi pamoja na wasimamizi wa sekta hiyo utapelekea wananchi kufanana na kasi ya ukuaji wa uchumi.

Aidha amezitaka mamlaka za TFDA, TBS, mamlaka za uvuvi na kilimo kufanya kazi kwa uadilifu na utii na wao kama Serikali watasimamia na kuhakikisha hakuna urasimu katika hilo, na amewahimiza tantrade ambao ndio wasimamizi na waandaaji wa maonesho hayo kutafuta masoko na kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na ubora na kuhamasisha matumizi ya bidhaa zinazozalishwa nchini.

Kuhusiana na ujenzi wa viwanda Suluhu amesema kuwa azma ya serikali katika ujenzi wa viwanda bado ipo palepale na hiyo ni pamoja na utafutaji wa masoko ya ndani na nje.

Kwa upande wake Katibu mkuu wa chama Cha mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally amewapongeza bodi, baraza na wafanyakazi wa tantrade kwa kuyatendea haki maonesho hayo mwaka hadi mwaka.

Amesema kuwa maonesho ya namna hayo ni kisiwa Cha kuboresha nyaraka za kisera zinazosaidia katika maendeleo.

Pia Waziri wa viwanda na biashara Innocent Bashungwa amesema kuwa gurudumu la maendeleo linaenda vyema na hiyo ni kutokana na uongozi Bora wa serikali ya awamu ya tano na kusema kuwa wizara za biashara na viwanda pamoja na uvuvi na kilimo  zinategemewa na watanzania wengi hivyo zitazidi kusimamiwa ili kuongea kipato zaidi.

Bashungwa amehaidi ushirikiano baina yao na wawekezaji na ndani na nje ya nchi na kuwahimiza watanzania kushiriki katika ujenzi wa taifa kwa kujihusisha na viwanda hasa vidogo na vya Kati.

Aidha amezitaka halmashauri zote nchini kutenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji na wao Kama wizara watahakikisha uwepo wamaeneo ya usindikaji. 

Ufunguzi huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo mawaziri, wakuu wa Wilaya, wabunge pamoja na wajumbe wa baraza la wawakilishi.
F87A0199

F87A0236

F87A0216
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza wakati wa uzindua rasmi wa maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara katika Viwanja vya Sabasaba Barabara ya kilwarod jijini Dar es salaam leo Julai 02, 2019. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
F87A0278
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizindua rasmi kwa kubonyeza kitufe maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara katika Viwanja vya Sabasaba Barabara ya kilwarod jijini Dar es salaam Julai 02, 2019. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
F87A0162

F87A0292
F87A0304
F87A0305
F87A0324
F87A0402
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa zawadi kwa washindi wakati wa uzinduzi rasmi na kutembelea maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara katika Viwanja vya Sabasaba Barabara ya kilwarod jijini Dar es salaam Julai 02, 2019. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
F87A0490
F87A0533
F87A0727
F87A0749
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,  akitembelea mabanda mablimbali mara baada ya kuzindua rasmi maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara katika Viwanja vya Sabasaba Barabara ya kilwarod jijini Dar es salaam Julai 02, 2019. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)