focusmedia Search This Blog
Monday, January 23, 2023
SIASA ZA KIISTARABU ZA RAISI SAMIA NA KUMBUKUMBU YA TUKIO LA " DINNER TABLE BARGAIN 1790 " NCHINI MAREKANI
Na Kassim Mpingi Rufiji-Pwani
Bila Shaka Taifa Linaunganishwa Na Siasa Za Umoja,Mshikamano,Kusameheana Na Kujenga Nchi Kwa Pamoja(4R).
Vyama Pinzani Baada Miaka Saba Vinaingia Tena Mtaani Kufanya Mikutano Na Kufurahi Matunda Ya Siasa Safi Na Za Kiistarabu Za Raisi Samia .
Aina Hii Ya Siasa Anayofanya Raisi Samia Imenifanya Nikumbuke Tukio Muhimu Katika Historia Ya Siasa Za Kiistarabu Duniani Lililotokea Nchini Marekani Mwaka 1790 Lijulikanalo Kama " Dinner Table Bargain " Au " Great Compromise Of 1790 "
Ilikuwa Usiku Wa June 20, 1790 Wakati Mikutano Ya " Congress " Inafanyika Jijini Newyork .Thomas Jefferson Wakati Huo Akiwa Secretary Of The State( Baadae Raisi Wa Tatu Wa Marekani) Alipoamua Kuwaalika Chakula Cha Usiku Watu Wawili Alexander Hamilton Wakati Huo Akiwa Secretary Of Treasure Na James Madison Mwakilishi Wa Jimbo La Virginia( Baadae Raisi Wa Nne Wa Marekani).
Mualiko Huu Ulisukumwa Na Tofauti Kubwa Na Uhasama Uliokuwa Wakati Huo Katika Ujenzi Wa Taifa La Marekani .
Tofauti Kubwa Iliyopelekea Kugawanyika Kwa Taifa Lao Ni Hoja Ya Hamilton Na Wenzake Kuwa Serikali Ya Shirikisho (F.G) Ibebe Madeni Ya Majimbo Yatokanayo Na Vita Vya Mapinduzi .Hoja Hii Ililigawa "Congress" Majimbo Ya Kaskani Yaliunga Mkono Hoja Hii Kwa Vile Madeni Yao Yalikuwa Ni Makubwa Na Wasingeweza Kuyalipa Huku Majimbo Ya Kusini Akiwemo Madison Wakipinga Kwa Kuwa Wao Walishalipa Madeni Yao.
Na Hoja Ya Pili Ilikuwa Wapi Yawe Makao Makuu Ya Taifa Lao La Marekani .
Ni Majadiliani Katika Kikao Hiki "Dinner Table Bargain Of 1790" Kilichoitishwa Na Jafferson Ndicho Kilicholeta Suluhu Hasa Baada Ya Madison Kukubali Hoja Ya Hamilton Na Kushawishi Majimbo Ya Kusini Kuunga Mkono Hoja Na Kwa Pamoja Kulijenga Taifa Lao Ambalo Leo Ni Moja Ya Mataifa Makubwa Na Yenye Nguvu Duniani.
Na Ni Katika Kikao Hii Ndio Maamuzi Ya Kuwa Makao Makuu Ya Taifa Lao Kuwa Newyork Yalifikiwa |
Ndio Maana Tunasema Wakati Huu Nchi Inaunganishwa Na Siasa Za Kiistarabu Za Samia Kupitia Sera Yake Ya "4R" Ni Vyema Kukumbuka Moja Ya Tukio Muhimu Katika Historia Ya Siasa Za Kiistarabu Ulimwenguni.
" The Great Compromise of 1790
Thursday, January 12, 2023
HISTORIA PANA YA ZANZIBAR NA TAWALA MBALI MBALI ZA KIFALME - SAYYID KHALIFA BIN HARUBU
Syd Khalifa alifanya mambo mengi ikiwemo michezo kama ya sailing, polo, tennis na mambo ya kidunia na ya kiakhera [Dini] alimradi aliishi. Alihudhuria mabaraza mengi sana akiwa bado mtoto, kitu kilompelekea kuwa kiongozi mzuri baadae, na kumudu kukaa kwenye kiti cha usultani kwa muda mrefu zaidi. |
Syd Khalifa alipata watoto wawili, baada ya kufa mmoja alizaliwa Syd Prince Sir Abdalla 12 feb 1910. na alipokufa Bi Matuka Ndipo alipomuowa Bi Nunuu binti Ahmed. lakini Bwana huyu alikataa kata kata kutawala na akajitia maradhi. Wingereza inamtambua kama kiongo mshirika wa vita zoto miili za Dunia dhidi ya Wajerumani,Wamarekani wanamjua alipowaruhusu kujenga kituo kikubwa cha kuongozea safari za Anga pale Tunguu |
Saturday, January 7, 2023
HOSPITALI YA KISASA KITOGANI,WILAYA YA KUSINI UNGUJA YAFUNGULIWA NA RAIS MWINYI
Na Mwandishi wetu Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi afungua Hospitali ya Kisasa ya Kitogani Wilaya ya Kusini ,Mkoa wa Kusini Unguja.
Kufunguliwa kwa Hospitali hii pia imeambatana na kufungwa kwa Vifaa tiba vipya,Gari la kubebea wagonjwa,hospitali ipo tayari kutoa huduma tofauti,ikiwemo huduma za wagonjwa wa nje(OPD),Mama na Mtoto ,huduma za kliniki mbalimbali zikiwemo za Pua,Koo,Masikio ,Macho,Magonjwa yasio ya kuambukiza kama Sukari,shinikizo la damu ,huduma za madawa(pharmacy),huduma za Wagonjwa wanaolazwa ikiwemo ,Wodi za Watoto,Mama Wajawazito kabla na baada ya kujifungua,Watu wazima Wanawake na Wanaume,huduma za wagonjwa wa dharura na ajali,Wagonjwa mahututi(ICU),huduma za watoto njiti ,Wodi tatu za wagonjwa wenye mahitaji maalum ya kujitenga(isolation) pia Kuna Theatres mbili (2)za kisasa, huduma za ushauri nasaha na kupiga vita vitendo vya udhalilishaji na huduma za uchunguzi ikiwemo Maabara ,Ultrasound,ECG na XRAYS.Kuna huduma za kisasa za Mfumo wa Tehama zikiwemo huduma za data,sauti na picha zitakazotumika katika kutoa elimu ya afya kwa wagonjwa na wananchi wanaofika katika hospitali hii,usajili wa mahudhurio ya wafanyakazi ,mifumo ya tahadhari ya moto ,Mfumo wa Nursing call System na Mfumo wa kutunza taarifa za wagonjwa kieletroniki(EMR).
Hospitali itawahudumia Wananchi zaidi ya 52,850 wakaazi wa Wilaya ya Kusini na maeneo jirani,