focusmedia Search This Blog
Thursday, November 10, 2022
Tuesday, November 8, 2022
WANAZUONI WA CHUO CHA DIPLOMASIA WAJADILI JUU YA SENSA YA WATU NA MAKAZI INAVYOWEZA KUTUMIKA KATIKA UTEKELEZAJI WA DIPLOMASIA YA UCHUMI. TAREHE 8 NOVEMBA 2022
Desderia Sabuni- Mkuu wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa Chuo cha Diplomasia akijadili juu ya Sensa ya watu na makazi (2022) inavyoweza kutumika katika Diplomasia ya Uchumi Tanzania. |
Seif Ahmad Kushengo Mratibu wa Sensa Kitaifa akitoa maelezo ya awali juu ya Zoezi zima la Sensa livyofanyika kitaifa |
Balozi Mstaafu Modest Jonathan Mero akijadili Sensa ya Watu na Makazi inavyoweza kutumika katika Utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi. Tarehe 8 Novemba 2022 |
Desderia Sabuni mhadhiri msaidizi na mkuu wa idara ya Uhusiano wa kimataifa na Diplomasia,mbobezi katika diplomasia ya uchumi
"Sensa inatoa dira ya uvutiaji wa wawekezaji,kiwango cha watu walioko nchini inaweza ikawa chachu ya fursa za uwekezaji nchini katika upatikanaji wa ajira,uwepo wa mitaji na uwepo wa soko."
Wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia wakifuatilia mjadala wa Sensa ya Watu na Makazi inavyoweza kutumika katika Utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi. |
Symphrosa Chaha Mratibu wa Mjadala wa Sensa ya Watu na Makazi inavyoweza kutumika katika Utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi. |
Bi. Precious Obed Moshi- Mwanachuo Chuo Cha Diploamsia akijadili Matumizi ya Takwimu za Sensa ya Watu na Makazi (2022) kwa maendeleo ya Jamii. |
Wahadhili na wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia wakifuatilia kwa makini mjadala waSensa ya Watu na Makazi inavyoweza kutumika katika Utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi. |
Wednesday, November 2, 2022
WATAALAMU WA CHINA NA TANZANIA: ZIARA YA RAIS SAMIA NCHINI CHINA KUINUA UHUSIANO WA NCHI HIZI MBILI KWENYE NGAZI MPYA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufanya ziara rasmi nchini China kuanzia kesho tarehe 2 hadi tarehe 4 mwezi Novemba, akiwa ni mkuu wa kwanza wa nchi ya Afrika kuizuru China baada ya Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC). Kwenye semina ya kimataifa kuhusu ziara ya rais Samia nchini China na mustakbali wa uhusiano kati ya China na Tanzania iliyoandaliwa Oktoba 31 na Taasisi ya Utafiti wa Afrika ya Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang, wataalamu na wasomi wa China na Tanzania wote wanaona kuwa ziara ya Rais Samia itainua uhusiano wa nchi hizo mbili kwenye ngazi mpya.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa China katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. Humphrey Moshi amepongeza mafanikio ya Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC. Amesema ziara ya Rais Samia nchini China ni alama ya kuimarika kwa uhusiano kati ya Tanzania na China, na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili una mustakbali mkubwa kwenye miradi mbalimbali ya miundombinu, ikiwemo maboresho ya Reli ya TAZARA na muunganiko kati ya bara la Afrika na kisiwa cha Zanzibar. Anaamini kuwa uhusiano na urafiki kati ya Tanzania na China hakika utapanda hadi kwenye ngazi mpya kutokana na juhudi za pamoja za pande hizo mbili.
Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Prof. Aldin Mutembei, ambaye pia ni mkurugenzi mgeni wa Taasisi ya Confucius ya UDSM, amesema mawasiliano ya kielimu yanatoa mchango muhimu katika kukuza ushirikiano kati ya Tanzania na China. Lugha ya Kiswahili imeanza kutumika kwenye mashirika ya kitaaluma ya China, hali iliyotandika njia kwa ushirikiano wa uchumi na uwekezaji kati ya nchi hizo mbili. Amesema kwa upande wa Tanzania Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimesukuma mbele ushirikiano kati ya pande hizo mbili kwenye nyanja mbalimbali kupitia taasisi ya Confucius. Pia ameeleza matumaini yake kuwa ziara hiyo ya Rais Samia nchini China itatoa fursa nyingi kwa maendeleo ya uhusiano kati ya Tanzania na China, na kupanua zaidi ushirikiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili.
- 6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
- 12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
- 20:00-22:00 (Afrika Mashariki)